JULIUS MBIAJI
Member
- Dec 13, 2011
- 76
- 11
Nimesikitishwa sana na tabia ya viongozi wa Idara ya elimu idara ya sekondari ya kupunguza baadhi ya wasimamizi wa mitihani kwa kisingizio cha mitihani kupungua.Halmashauri nyingine hakuna mambo kama haya na once mtu ameteuliwa kusimamia mtihani basi ni hadi mitihani yote ikamilike sasa kinachofanyika huku ni tofauti.Je BARAZA MNATUSAIDIAJE?Pia mwaka jana waliita watu wengi kwenye semina ili waombe fedha nyingi kutoka baraza na baada ya watu kufika vituoni walipunguzwa kwa kisingizio cha kuzidi idadi ya vyumba haliyakuwa wenyewe ndiyo wanaokagua vyumba vya mitihani.Wakuu naomba mawazo yenu ili tuweze kutatua matatizo haya.Natanguliza shukrani za dhati kwa ushauri wenu na taarifa zaidi kama nitapata kupitia jukwaa hili adhimu.