Steph Curry
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 5,936
- 4,713
Anasa kivipi mkuu?? Kwani tunanunua ili zibebe watu bure au tunazifanyia biashara...Usafiri wa ndege bado ni anasa. Waimarishe miundombinu ya barabara kwanza
Ethiopian Airlines mwaka jana ilipiga faida ya karibia Trillion 7 za Tanzania... Hatujachelewa, tukianza sasa baada ya miaka 10, 20 mbele tutakuwa tushafikia hapo... Habari njema ni kwamba nchi yetu inatembelewa na watalii zaidi ya million na nusu kwa mwaka, tukiwa na Shirika letu imara, tukatangaza vivutio vyetu vizuri naamini tutapokea mpaka zaidi ya watalii million 2 na nusu ndani ya miaka hii mitano tu... Nchi nyingi za Asia zina mashirika yake Imara na wanajitangaza sana na ndio maana kwao kupokea zaidi watalii million 10 kwa mwaka sio ajabu na wakati huo wala hawana vivutio vya kutupita sisi...
Kumbuka tu, Utalii sio kitu cha kupuuza kabisa hapa kwetu maana zinachangia 26% ya GDP yetu na ndio chanzo kikuu cha fedha za kigeni hapa nchini... Hatuwezi sasa kurahisisha ufikaji wa watalii kirahisi hapa kwetu bila ya kuwa na Shirika letu ambalo linaweza likaweka bei nzuri hivyo kuwavutia zaidi watalii kutembelea nchini na pia kupanda ndege zetu... Tukisimama hapa kiukweli na kutia mkazo kabisa naona ndani ya miaka kadhaa tutaingiza fedha nyingi mno ambazo sasa ndizo zitatumika kujenga hivyo vitu unavyosema...