Kuhusu mifuko inayoitwa "Shangazi Kaja"

Kuhusu mifuko inayoitwa "Shangazi Kaja"

Reli ya Tazara haiishii stesheni! Nawe hauna tofauti na huyo asiyejua reli ya Kigoma ni ipi.
RELI YA KIGOMA INAISHIA STATION SIO TAZARA

Hebu soma tena nilichoandika. Rudi pale juu kasome tena pia. Unakurupuka kama unaoga nje.
 
Habari zenu wakuu.

Kuna mifuko fulani mikubwa inafanana na viroba vile vya kuhifadhia unga wa mahindi ila yenyewe inakuwa na rangi na michoro au picha kutia nakshi na urembo; maarufu SHANGAZI KAJA.

Nimekaa nikatafakari, ina maana shangazi zetu wanapotoka vijijini kuja mjini ndo hubeba humo nguo zao? Kwa hiyo ukiliona tu ndani fuko hilo kubwa unajua leo SHANGAZI KAJA.

Yaani shangazi, dada yake baba. Mtu wa heshima kabisa. Amedhalilika kabisa kiasi mfuko wake wa kubebea mazaga tumeupa jina hilo. Maskini shangazi.

Asee dada huko kijijini, ukitaka kuja mjini usiniombe nauli tu. Omba na pesa ununue bag zuri ili ukija uweke heshima. Hii itawafanya wapwa zako (wanangu) wakose cha kusema.

Au kuna sababu zingine za jina hilo. Kwanini shangazi kaja?

View attachment 1202793
Sisi kwetu yanaitwa Tukuyu kyela na jina hili lilikuja ukibeba hilo bag ukafika stand makonda wanakwambia wewe lazima unaenda Tukuyu au kyela
 
Mm nikadhani unamzungumzia Shangazi yule rais mstaafu wa wana sheria kumbe Shangazi huyo bhana..[emoji23][emoji23]

Mungu Ibariki Tanzania[emoji1241][emoji1241][emoji1241]
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Gairo
Mungu Ibariki Morogoro
 
Akina shangazi mara nyingi hatupendwi na hatukaribishwi vizuri kwenye nyumba za kaka zetu, tukiienda tunaonekana kero ndio maana mimi siendagi kwa bro
sio uongo kina shangazi mna wivu na wake wa kaka zenu
 
sio uongo kina shangazi mna wivu na wake wa kaka zenu
[emoji12][emoji12][emoji23][emoji23] eti Shangazi Khantwe ni ya kweli hayo kuwa Wivu huwa unawasumbua??

Mungu Ibariki Tanzania[emoji1241][emoji1241][emoji1241]
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Gairo
Mungu Ibariki Morogoro
 
Hiyo mifuko niliiona kwenye movie moja ya kizungu,wazee wamepiga hela bank ndio wakawa wanatia hela kwenye mifuko ya shangazi kaja.
 
[emoji12][emoji12][emoji23][emoji23] eti Shangazi Khantwe ni ya kweli hayo kuwa Wivu huwa unawasumbua??

Mungu Ibariki Tanzania[emoji1241][emoji1241][emoji1241]
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Gairo
Mungu Ibariki Morogoro
Huyo ni yeye sio mimi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wifa kaja, dada kaja, shangazi kaja inategemea ni nani anayesema?

Ila nyie wakina dada hamuwapendi wifi zenu. Kwanini?
Wewe ukifika nyumbani kuna mtu anasema mume wangu karudi, kuna mtu anasema baba karudi, mwingine bro karudi n.k, the feeling is the same? Jibu ni hapana. Kuhusu kuwapenda mimi wifi zangu nawapenda labda tuwaulize wasiowapenda
 
Nyinyi si ndio wale mkiwa mnapewa mavitu na waume zenu mnaita mahaba. Sisi tukiwapa wake zetu (wifi zenu) ooh limbwata...kaka kakamatwa....oooh mwanamke anamchuna bro...eeeh maneno kibao.
 
Nyinyi si ndio wale mkiwa mnapewa mavitu na waume zenu mnaita mahaba. Sisi tukiwapa wake zetu (wifi zenu) ooh limbwata...kaka kakamatwa....oooh mwanamke anamchuna bro...eeeh maneno kibao.
Mkuu mbona maneno yanakutoka hivyo, au hujaelewa huo mfano?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom