Carnivora
JF-Expert Member
- Jan 26, 2018
- 3,650
- 6,028
Habari zenu wakuu.
Kuna mifuko fulani mikubwa inafanana na viroba vile vya kuhifadhia unga wa mahindi ila yenyewe inakuwa na rangi na michoro au picha kutia nakshi na urembo; maarufu SHANGAZI KAJA.
Nimekaa nikatafakari, ina maana shangazi zetu wanapotoka vijijini kuja mjini ndo hubeba humo nguo zao? Kwa hiyo ukiliona tu ndani fuko hilo kubwa unajua leo SHANGAZI KAJA.
Yaani shangazi, dada yake baba. Mtu wa heshima kabisa. Amedhalilika kabisa kiasi mfuko wake wa kubebea mazaga tumeupa jina hilo. Maskini shangazi.
Asee dada huko kijijini, ukitaka kuja mjini usiniombe nauli tu. Omba na pesa ununue bag zuri ili ukija uweke heshima. Hii itawafanya wapwa zako (wanangu) wakose cha kusema.
Au kuna sababu zingine za jina hilo. Kwanini shangazi kaja?