Kuhusu mgomo wa madaktari: John Mnyika

sasa kutoenda kwenye kikao ndio umesaidia nn ? au ndio kujijenga kisiasa?

hopeless moving figure,hivi utenda kwenye kikao cha kamati kwa mgomo huu wa madaktari?au unakurupuka tu kutoka usingizini?soma tena hilo tamko,halafu oanisha na tukio linaloendelea sio tu uonekane umepost kitu
 
Kila kitu Rais jamani hivi nchi hii hatuwezi kuwawajibisha hata wale ambao Rais akiwa safarini na wao wanalala. Je Tutafika
CCM wamezoe porojo kama wewe mama porojo hata rais amezoea porojo na ndio maana hakuona umuhimu wa kumaliza kwanza tatizo la mgomo huu ulioko kwenye sekta nyeti inayogusa moja kwa moja uhai wa watu.acha porojo,unawezaje kwenda kutalii huku watu wako wanakufa?shame on you mama porojo na magamba wote
 
updates: kikaoni mawaziri mponda,ghasia,nkya pia nyoni na mtasiwa wapo kikaoni. Mwenyekiti anawasomea madai ya madaktari. Pinda amekwepa.!

kazeni buti na muongee kwa confidence,shusheni point hasa na wala msikubali majibu ya kisiasa za uongo,msikubali kuambiwa,Serikali iko kwenye mchakato,tunalifanyia uchambuzi yakinifu,tuko kwenye hatua za utekelezaji,Serikali imeyachukua mapendekezo yenu na itayafanyia kazi,tutaunda tume kuchunguza madai yenu,na mengine ya aina hiyo.majibu hayo msiyapokee.wazungumze kwa fact na ikibindi ahadi ziwe na commitment,ya kwamba akishindwa apelekwe mahakamani na ajiuhuzulu ubunge.
 
Nashanga!!! Waziri kivuli wa Afya ni nani vile?

huyo mnyika ndo msemaji wa chama, si kila mtu anaweza toa tamko kama kwenye chama changu cha ccm. nimeipenda ni utaratibu mzuri, chadema c kwa mwanshonzi a.k.a mwa kambale kila mmoja ana ndevu
 
Kila kitu Rais jamani hivi nchi hii hatuwezi kuwawajibisha hata wale ambao Rais akiwa safarini na wao wanalala. Je Tutafika

ni kwa sababu ameteua washikaji zake kuvuna mali za watanzania. Hawana maamuzi ndo maana kila mtu anasema raisi akija atatoa maamuzi- kwa nini asilaumiwe? anyway waziri wa afya amekataliwa, ghasia anawasilisha kwa niaba yake. Amesema intern watarudishwa muhimbili, suala la nyumba wameahi kujenga,kama kawaida yao! They are just talking politics. Hakuna maboresho ya hospitali,
 
Tamko lina mashiko,japo amekosea tu kumtaja Makamu wa Rais. Kwani ana mamlaka yule c ni ceremonial tu?
 
Friday, January 27, 2012

KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI
....

Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye mwenye dhamana kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 33 ndiye kiongozi wa shughuli za serikali na ibara ya 35 shughuli zote za utendaji wa serikali zinatekelezwa na watumishi wa serikali kwa niaba ya Rais; ameondoka kwenda nje ya nchi mgomo ulipoanza na hakuna kauli yoyote mpaka sasa toka kwa Makamu wa Rais wala kwa Ikulu.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda badala ya kwenda kwenye eneo la mgomo na kuzungumza na madaktari naye ameishia kuzungumza na vyombo vya habari. Waziri wa Afya Dk. Haji Mponda na Naibu Waziri Dk. Lucy Nkya nao jana wamezungumza na waandishi wa habari badala ya kwenda kukutana na madaktari na kuzungumza nao kuhusu madai yao ya msingi.

....

Wenu katika utumishi wa umma,

John Mnyika (Mb)

Hapo nadhani amemaliza kila kitu....
 
Alie post ni Osokoni lakini mwisho jina la John Mnyika,hapo sielewi kidogo.
shughuli pevu...

Hongera CDM, umma wa watanzania upo pamoja nanyi -- nyie ndiyo tumaini letu. acheni watu wapande mindege wakati watu wao walioapa kuwatumikia wakiwa wanateketea, tena si kwa mafuriko bali kwa vitu ambavyo vinaongeleka. Madaktari tupo pamoja nanyi, tunajua taaluma ya Udaktari ni WITO ila wito huo usigeuke kuwa kitanzi kwenu.
 
kuhamasisha mgomo wa madaktari ni upu.mbavu uliopitiliza....madaktari wanapata mshahara mwingi kuliko wafanya kazi wengine...madaktari sio ndo watu muhimu kuliko wafanyakazi wengine wa kitanzania...bila watu wengine hapa tz madaktari pia wanaweza kupata matatizo mengi,namaanisha kuwa tunaishi kwa kufaidiana na kutegemeana...mimi sio daktari lakini kwa huduma yangu daktari anaihitaji sana bila hiyo anaweza kuishi vibaya na hata kupoteza maisha...mwalimu, polisi, na mfanya kazi yeyote anacho kitu ana contribute kwa taifa na kwa wananchi kwa namna moja au nyingine, aina fulani ya wafanyakazi ikijiona wao ni wa muhimu kuliko wengine hapa nchini ni ujinga usio na dawa....

kwa sasa hivi ninavyoongea serikali haina hela, kila mtu hilo analijua, magari mengi tu ya serikali yamepaki, hawana mafuta kuendesha....katika wakati mgumu kama huu, tunatakiwa kushare poverty, kidogo tulichonacho tunatakiwa tugawane ichoicho hata kama ni kidogokidogo...kundi moja lisitake kupata kikubwa kwa imani kwamba wao ni wa muhimu kuliko wengine....je? daktari ni wa muhimu kuliko walimu na polisi? polisi wanapata sh ngapi, walimu wanapata sh ngapi? secta zingine zinapata sh ngapi?...ujinga huu nimeulaani vibaya sana, kwasababunimeshuhudia kwa macho yangu wagonjwa wakifariki hospitali kwasababu ya mgomo huu..

dhambi hii madaktari wanafanya itawarudia, kama wamesababisha watu wamekufa, wao pia watakufa tu siku moja na watakosa hata wa kuwazika...Mungu ibariki |Tanzania.....
 
mkuu umetowa changamoto nzuri sana! Wasi wasi wangu humu ndani watakuita wewe ni gamba! Hata hivyo ukweli utabaki pale pale! Pamoja na dhamira "nzuri" ya CHADEMA kujaribu kuikomboa nchi yetu kutoka mikononi mwa warafi wachache, bado chama hiki kinaupungufu watu wenye uzoefu wa kuendesha serikali!

Wakati huu wa mgomo wa madaktari ambapo waziri wa afya na timu yake wameudhihirishia umma kwamba hawana uwezo wakuongoza wizara tulitegemea kuona waziri kivuli akitueleza yeye na seikali yake ya chadema wangefanya nini kutatua mgogoro huu! Badala yake tamko linatolewa na kiongozi wa chama!!

Mkuu, mimi sioni tatizo la Mhe. Mnyika kulizungumzia tatizo hilo badala ya waziri kivuli wa afya.
Ni imani yangu kuwa Mhe. Mnyika hakukurupuka kiuliongelea bila kwanza kupata baraka za chama chake, CHADEMA wako makini sana.
Tatizo la madaktari na suluhisho lake linajulikana, ni kutimiza madai yao tu basi (pesa).
Waziri kivuli wa afya angeweza kuingilia kati kama yangekuwa ni masuala ya kisera au kiutawala.
Kwa sababu hiyo mimi ninaona Mhe. Mnyika alichokifanya ni sahihi kabisa.
Naruhusu kukosolewa kama unadhani maoni yangu si sahihi.
 
Alie post ni Osokoni lakini mwisho jina la John Mnyika,hapo sielewi kidogo.

Pengine Osokoni atatoa ufafanuzi.Akitia mgomo tutajiuliza zaidi na kuanza kuwa na picha whenever we see Osokoni, then that is John Mnyika.
 
Hivi hatuwezi kumpiga stop mkuu wa kaya kutoa bongoland abaki uko hewani au akatafute hifadhi popote?
 
Ni sahihi kwa Mh Mnyika kutoa kauli hii, kwani mbali ya uwaziri kivuli nishati na madini, na Ubunge Ubungo, yeye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, lakini muhimi zaidi, ni Mkurugenzi wa Siasa na Uenezi. So he has acted on his actual capacity. Katoa matamshi mazuri sana, kwani suala la msingi hapa ni maslahi ya taifa hili, hasa juu ya suala nyeti kama hili la sekta ya afya ambayo ni moja ya mihimili mikuu ya MTAJI WATU (human capital) wa taifa hili, mhimili mwingine ukiwa ni Sekta ya elimu, ambayo nayo imejaa madudu matupu. Job well done Mnyika.
 
Mchango mzuri Mnyika lakini nilitegema waziri kivuli wa Afya aitoe hii statement. CHADEMA jitahidini kwenye safu ya 'shadow cabinet' Waziri wa serikali iliyo madakarani akifanya/asipofanya jambo ni vema tena kwa haraka sana Waziri kivuli akasema CHADEMA wangefanya nini tofauti? Sasa Waziri kivuli yuko wapi?

Si hivyo basi, bali secretariat ya CDM ndio inatoa kauli kwanza halafu waziri kivuli anaingia kazini. CDM iko juu ya waziri kivuli. Ni kwa vile secretariat ya CCM ipo kijina tu ingeweza kutoa maagizo kwa mawaziri wake.
 
kuhamasisha mgomo wa madaktari ni upu.mbavu uliopitiliza....madaktari wanapata mshahara mwingi kuliko wafanya kazi wengine...madaktari sio ndo watu muhimu kuliko wafanyakazi wengine wa kitanzania...bila watu wengine hapa tz madaktari pia wanaweza kupata matatizo mengi,namaanisha kuwa tunaishi kwa kufaidiana na kutegemeana...mimi sio daktari lakini kwa huduma yangu daktari anaihitaji sana bila hiyo anaweza kuishi vibaya na hata kupoteza maisha...mwalimu, polisi, na mfanya kazi yeyote anacho kitu ana contribute kwa taifa na kwa wananchi kwa namna moja au nyingine, aina fulani ya wafanyakazi ikijiona wao ni wa muhimu kuliko wengine hapa nchini ni ujinga usio na dawa....

kwa sasa hivi ninavyoongea serikali haina hela, kila mtu hilo analijua, magari mengi tu ya serikali yamepaki, hawana mafuta kuendesha....katika wakati mgumu kama huu, tunatakiwa kushare poverty, kidogo tulichonacho tunatakiwa tugawane ichoicho hata kama ni kidogokidogo...kundi moja lisitake kupata kikubwa kwa imani kwamba wao ni wa muhimu kuliko wengine....je? daktari ni wa muhimu kuliko walimu na polisi? polisi wanapata sh ngapi, walimu wanapata sh ngapi? secta zingine zinapata sh ngapi?...ujinga huu nimeulaani vibaya sana, kwasababunimeshuhudia kwa macho yangu wagonjwa wakifariki hospitali kwasababu ya mgomo huu..

dhambi hii madaktari wanafanya itawarudia, kama wamesababisha watu wamekufa, wao pia watakufa tu siku moja na watakosa hata wa kuwazika...Mungu ibariki |Tanzania.....

Mungu ubariki msafara wa wauza sura ulioenda Davos watumie hela kidogo kutoka kwenye hilo fungu na warudishe chenji tununue hata gloves. Amin!
 
nimemdharau mnyika kupita maelezo...hajawahi kuugua akaona uchungu wa kuugua, wala hajawahi kufiwa kwa kukosa daktari....ni mjinga kupita maelezo....na nikiona mtu anaongeahayo mbele yangu hakika yake nitampiga ngumi nyingi sana...inakera kusikiliza.
 
Ni sahihi kwa Mh Mnyika kutoa kauli hii, kwani mbali ya uwaziri kivuli nishati na madini, na Ubunge Ubungo, yeye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, lakini muhimi zaidi, ni Mkurugenzi wa Siasa na Uenezi. So he has acted on his actual capacity. Katoa matamshi mazuri sana, kwani suala la msingi hapa ni maslahi ya taifa hili, hasa juu ya suala nyeti kama hili la sekta ya afya ambayo ni moja ya mihimili mikuu ya MTAJI WATU (human capital) wa taifa hili, mhimili mwingine ukiwa ni Sekta ya elimu, ambayo nayo imejaa madudu matupu. Job well done Mnyika.

Hali hii imefanya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa na nakisi ya watumishi asilimia 48% na takwimu zinaonesha kuwa 18% ya wafamasia, 15% ya madaktari, 13% ya madaktari wasaidizi waliacha vituo vyao vya kazi na kwenda kutafuta kazi kwenye mashirika ambayo yanalipa mishahara mikubwa na mizuri. Nakisi hii itaongezeka zaidi iwapo madai ya msingi ya madaktari na watumishi wengine hayatashughulikiwa na serikali itaendelea kuchelewa kushughulikia migogoro na migomo mingine inayoendelea.

Ni imani yangu kwamba serikali ikiwa na dhamira inaweza kuongeza mishahara kwa watumishi wa sekta ya afya ili kuweza kuwavutia wataalamu kubakia nchini badala ya kwenda kugoma au kwenda kutafuta kazi nje ya nchi kutokana na malipo mazuri huko. Hii ni pamoja kuwezesha malipo ya mazingira magumu kutolewa kwa watumishi wa afya wanaofanya kazi katika maeneo na kada maalum.

Mchambuzi mim ni mmoja wa wataka mabadiiko na CDM ndio tumini letu. Nilikuwa natafuta kauli ya CDM sana. nashukuru nimeiona.

Lakini kun mambo inabidi tuangalie uhalisia . kuongeza mishara ya wafanyakazi wa sekta ya afya ni kauli too general kama tunavyogea mimi na wewe humu jamvini . Basi chadema na Mnyika waseme wao wanaona nyongezza ya % ngapi inafa au ingekuwa wao wafanya kazi wangekuwa na mishahara yenye % juu au chini zaidi ya sasa . Sometime inabdi tuwe Realistic

Na vile vile Myika akumbuke udaktari ni sekta muhimu sababu tu inacheza na uhai wa watu lakini Grievences zinazofanana madkatari ziko sehemu na sekta nyingi.

Mimi wakati naungana na madaktari kuishinikiza serikali madai yao napenda kujua altenavitve gani zmetumik kwa muda gani ziashindikana. Bado sivutiwi na kitendo cha madaktari kugoma katia hali hii . Na mgomo wao unaonekanani mgomo holela.....

tulitakiwa tusikiee
  • mazungumzo yamekwama ...... then kama hayakuzaa matunda
  • tuskie mgomo wa siku mbili tu mwezi january 2012......... tehen kama hakuna klichoendelea
  • Tusikie Mgom wa siku nnne february.............. then kama hakuna kilichoedela
  • Then ndio uwe mgmo rasmi usio na mwisho.
Mimi kwa kweli nashangaa mgomo wa ghafla bin vu.
 
serikali haina pesa...kugoma kwenu hakuna matunda na mtaumiza wananchi bureee, serikali ingekuwa na pesa ingehsawapa pesa mnazodai...nakwambia hawana pesa kabisa...
 
Back
Top Bottom