Kuhusu mgomo wa madaktari: John Mnyika

Huna lolote wewe kijana usiingize siasa ktk uhai wa watu,Serikali inashughulikia matatizo ya madaktari kwani ni mazito na yanahitaji upembuzi yakinifu.mbona mnajitia kimbelembele ktk mambo ya watu baada ya kuimarisha chama chenu kiwe cha Kitaifa kwa kupata wawakilishi Tanzania Zanzibar.jengeni Chama kwa kufungua matawi wete pemba,mbona mnashindwa na cuf wenzenu wana wabunge Tz bara na Tz Zanzibar chama chao ni cha Kitaifa kipo pemba Mpaka Tarime.Si umepewa Uenezi we kijana eneza chama chako Zanzibar.
 
iki kimnyika na sura yake ya kike wakati mwingine kinakera kiasi kwamba naanza kuichukia na chadema yake...angekuwa amefiwa na ndugu hata mmoja tu angekuwa na cha kuongea kingine hapo...hopless boy/tomboy...
 
Friday, January 27, 2012

KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI



Mgomo wa madaktari unaoendelea hivi sasa umedhihirisha kwamba tuna serikali dhaifu yenye ombwe la uongozi. Haiwezekani wananchi wakawa wanakufa kwa kukosa matibabu stahiki na wengine wakipata madhara kutokana na kuchelewa kupata matibabu sababu ya mgomo wa madaktari halafu viongozi wenye dhamana hawachukui hatua sahihi.


Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye mwenye dhamana kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 33 ndiye kiongozi wa shughuli za serikali na ibara ya 35 shughuli zote za utendaji wa serikali zinatekelezwa na watumishi wa serikali kwa niaba ya Rais; ameondoka kwenda nje ya nchi mgomo ulipoanza na hakuna kauli yoyote mpaka sasa toka kwa Makamu wa Rais wala kwa Ikulu.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda badala ya kwenda kwenye eneo la mgomo na kuzungumza na madaktari naye ameishia kuzungumza na vyombo vya habari. Waziri wa Afya Dk. Haji Mponda na Naibu Waziri Dk. Lucy Nkya nao jana wamezungumza na waandishi wa habari badala ya kwenda kukutana na madaktari na kuzungumza nao kuhusu madai yao ya msingi.

Kwa upande wetu CHADEMA tulitoa kauli tarehe 25 Januari 2012 ya kutaka serikali ichukue hatua na tuliona tuipe serikali nafasi ifanye kazi yake hata hivyo serikali haionyeshi kuupa uzito unaostahili mgogoro huu wenye kuathiri hali za wagonjwa na maisha ya wananchi katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Tuliacha kwenda katika eneo la mgomo kukutana na madaktari katika siku za awali kuepusha suala hili kutafsiriwa kuwa ni la kisiasa.
Madai ya madaktari na watumishi wengine wa sekta ya afya nchini yasiposhughulikiwa kwa wakati na kwa ukamilifu watumishi husika wanaweza wasiwe kwenye mgomo wa wazi kama ilivyo kwa baadhi ya hospitali na zahanati nchini lakini wataendelea na migomo baridi kwa kutoa huduma mbovu au kuacha kazi kwenye maeneo ya umma na wengine kwenda kufanya kazi nje ya nchi wakati kukiwa na uhaba wa watumishi nchini.

Aidha, pamoja na migomo inayoendelea, naendelea kutoa rai kwa madaktari na watumishi wengine wa umma kuhakikisha maisha ya wagonjwa walio katika hali ya hatari yanaokolewa.

Nimezungumza na viongozi wetu wakuu kuhusu suala hili na natoa mwito kwa wadau wote kuunganisha nguvu katika kuisimamia serikali kushughulikia madai ya madaktari na wafanyakazi wengine wa sekta ya afya kwa haraka ili kuepusha madhara zaidi kwa umma.



John Mnyika (Mb)

Imekula kwenu, JK amenyamaza kimya kazi yote ameimaliza Pinda tena bila hata kuonana nao, ni amri tu kwenye vyombo vya habari madaktari wamefyata mkia. Warudi sasa mahospitalini wakaendelee na kazi. Pinda ameonyesha kwamba serikali sio dhaifu na ameonyesha uongozi

......ndiyohiyo
 
Back
Top Bottom