Kuhusu Mama...Hii imekaaje?

Kuhusu Mama...Hii imekaaje?

A Father

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2012
Posts
1,385
Reaction score
601
Habari zenu watumiaji wa JF wenzangu?
Tupeane uzoefu kama ishawahi kukutokea, kwa wale tuliojaliwa kuishi na Mama.
Mama anaomba kurudishiwa gharama zake anazotumia juu yangu, mf: kanitumia kitu niko mbali na home, anadai nimlipe, amenisafirishia vifaa vyangu nilivyoviacha nilikokuwa nikiishi before, anadai nimrudishie alichotumia.
==========================
NOTE: si kuwa hana kazi wala cha kumuingizia kipato.
==========================
Hii imekaaje??? Imewahi kukutokea???
Au kwa kuwa si Mama mzazi???
Je, Mama mzazi anaweza kufanya hivyo???
 
Shida iko wapi wewe kulipia gharama ya kusafirisha vitu hivyo?
Sioni tatizo besides ulitakiwa ulipokuwa unaomba utumiwe vitu hivyo utume na hela ya kusafirisha.

||"You were too young to understand"||
 
Ushakua mtu mzima
Mama yako anakutegemea wewe pia anakugindisha kujitegemea

Kuna tatizo gani ukimtumia hela ili utumiwe vitu vyako?

Yaani umtegemee mama hadi uzeeni?

Khaaa

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Habari zenu watumiaji wa JF wenzangu?
Tupeane uzoefu kama ishawahi kukutokea, kwa wale tuliojaliwa kuishi na Mama.
Mama anaomba kurudishiwa gharama zake anazotumia juu yangu, mf: kanitumia kitu niko mbali na home, anadai nimlipe, amenisafirishia vifaa vyangu nilivyoviacha nilikokuwa nikiishi before, anadai nimrudishie alichotumia.
Hii imekaaje??? Imewahi kukutokea???
Au kwa kuwa si Mama mzazi???
Je, Mama mzazi anaweza kufanya hivyo???
kama ni mzazi wako kamili kuna shida mahali
 
mama yako mzazi ungemwambia akusafirishie vitu vyako bila kumpa pesa ya usafiri?ni wajibu wako kujigharamia kama umri unakuhitaji kufanya hivyo
 
Yaani mamako alikulea na kukulisha ukiwa mdogo. Na bado unataka aendeleze malezi? Una tabia mbaya, kwanza kabla hata hajakuambia umrudiishie hela ungetuma na ya ziada kabisa asiingie mfukoni kutuma vitu vyako! Ukiambiwa gharama ya kutuma ni laki 2 unatuma tatu kabisa just in case. Na usisahau kumtumia mamako hela hata kama hajaomba wala kuwa na kazi ya kukufanyia.
 
..Halafu unajiita " a father" yaani we unadhani mama ana jukumu la kukufanyia we kila kitu bure bure tuu.. We mwanaume wa aina gani? Unatutia aibu! Mwanaume majukumu kaka sio unakuja kulia hapa jf eti mama anakudai hela ya kukutumia vitu vyako. Khaa!
 
kama ni mzazi wako kamili kuna shida mahali

Nami naona kuna shida.... ambayo ipo kwa mtoto. Inaonesha umri wa kujitegemea umeshafika ila anaendekeza utegemezi bila sababu za msingi. Unapaswa kuwa na shukrani kwa mama yako kwani amekulea mpaka umefikia umri wa kuishi mwenyewe bila ya yeye. Nahisi huwa anakerwa sana na tabia yako ya kusubiri uombwe pesa ya kutuma vifaa vyako. Ona aibu A Father!!
 
Dah! Hapa wewe huna budi kumlipa gharama zake isipokuwa wewe kumfanyia yeye ni bure. Acha ubahili kijana. Anyway wewe ni mwanaume au mvulana maana sioni unacholalamikia wakati ni wajibu wako
 
Toto kuuubwa la zamani bado unataka kuendelea kudeka? Tuwekee namba yako ya TIGOPESA tukulipie alafu tuone!
 
Next time hata kama ni ndugu yako kivipi unapohitaji kitu kutoka upande alipo ni vyema kutanguliza malipo kwani huwezi jua mipango yake ikovipi unless aseme mwenyewe. Ni haki kumrudishia gharama labda kunajukumu upande wake lilisimama ili afanikishe lako.
 
We ushakuwa kaka jenga tabia ya kujitegemea na sio kumlaum tu mama na kumtaftia vijisababu visivya na maana.Hamna analo kosea ila anafanya anachoona sahihi kwa muda huu.
 
Mmmh, haya mazito kwani ulitaka atumie hela yake kukutumia mizigo yako?yani ningekua wewe ninge shukuru mungu kua na mtu anae weza kunifanyia langu kwani sikuizi sio wote wanaojali la mtu, pili ulitaka na pesa pia ulipiwe ilitakiwa wewe ndio umuongeza hela ya asante kwani unasomeshwa na wazee au unajitegemea mwenyewe?
 
Habari zenu watumiaji wa JF wenzangu?
Tupeane uzoefu kama ishawahi kukutokea, kwa wale tuliojaliwa kuishi na Mama.
Mama anaomba kurudishiwa gharama zake anazotumia juu yangu, mf: kanitumia kitu niko mbali na home, anadai nimlipe, amenisafirishia vifaa vyangu nilivyoviacha nilikokuwa nikiishi before, anadai nimrudishie alichotumia.
==========================
NOTE: si kuwa hana kazi wala cha kumuingizia kipato.
==========================
Hii imekaaje??? Imewahi kukutokea???
Au kwa kuwa si Mama mzazi???
Je, Mama mzazi anaweza kufanya hivyo???

Kama umeshapata kazi mrudishie....ulitegemea akulee hadi una miaka mingapi
 
Back
Top Bottom