Kuhusu maandamano ya Mwabukusi na Mdude 9/11/2023, wasizuiwe waachwe maana hayana maana, watapuuzwa na wananchi

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,603
Kinachokwendwa kufanywa na wakili Mwabukusi na mwanaharakati Mdude tarehe 9/11/2023 juu ya maandamano waliyopanga ni kujaribu kuficha aibu ya kuumbuka kwa upotoshaji wao.

Maandamano hayo ya tarehe 9/11/2023 awali yalipangwa kufanyika 30/09/2023 na kama yangefanyika kipindi hiko na hoja walizonazo walikuwa na sababu lakini kwa kuwa hoja zao ni zile zile basi maandamano ya 9/11/2023 ni kutafuta kichaka Cha kujificha na aibu.

Kama wataenda na hoja za makubaliano IGA wakati kuna mikataba tayari imesainiwa na imeonesha maboresho makubwa kwenye hoja za IGA kama ukomo wa mkataba na mengineyo, narudia tena wanaenda kutafuta kichaka Cha kuficha aibu. Sote tunajua mikataba ilivyoleta Imani kwa Serikali na kupongezwa kila Kona na hili nafikiri Mwabukusi na Mdude wanatambua.

Kwa kuwa tumeiona nia njema ya Serikali kwenye uwekezaji wa bandari basi ushauri wangu ni kuwaacha Mwabukusi na Mdude waendelee na maandamano hayo.

Kuzuia maandamano yao ni kuwapa umuhimu mkubwa ambao hawatakiwi kuwa nao. Nia yao kubwa ni kutaka kuelezea dunia stori wanayotunga na stori hiyo si kuhusu uwekezaji wa bandari basi ni ukosefu wa haki ya demokrasia. Tunajua Mwabukusi na Mdude si wazalendo wa kiwango hiko cha kujitoa ila Kwa sababu ya maslahi binafsi wapo tayari kufanya hivyo.

Tafadhali Serikali ya Mkoa wa Mbeya waruhusuni wafanye maandamano hayo ili aibu watakayopata kwa wananchi wasiisahau maana wataambulia aibu ya mwaka. Wananchi wameamua kwenda na Serikali ya Rais Samia kwenye uwekezaji wa Babdari.
 
Hata kama yakipata Watu wengi kweni kuna ubaya gani kuwaacha Wananchi waonyeshe hisia kwenye mambo yanayowahusu?

Kutishia kuwaua au kuwavunja Miguu ni kosa la Jinai.
 
Back
Top Bottom