Kuhusu kuingiza trekta Tanzania

Kuhusu kuingiza trekta Tanzania

Ndamwe

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2008
Posts
244
Reaction score
177
Jamani wana JF heshima kwenu wote. Mimi naomba kuuliza kuhusu uingizaji wa zana za kilimo Tanzania hususani trekta na viambatisho vyake (jembe na harrow) kutoka Ulaya. Kuna gharama ya ushuru wowote? au kuna gharama gani kuhusiana na TRA au bandarini? Naomba mwenye taarifa na ushauri wa kunisaidia ili nione katika kujibana kwangu naweza kufanikisha hitaji langu.
Natanguliza shukrani za dhati kwenu.
 
Tangazo la mwisho la serikali baada ya kikao cha bunge la budget 2008/2009 lilisomeka kwamba zana za kilimo hasa trekta na vikorokoro vyake havitalipiwa ushuru.
 
Asante sana mkuu wangu kwa taarifa hii, ubarikiwe!
Salute!
 
Back
Top Bottom