Kuhusu Joseph Mungai

Kwanza hii ni habari imekaa ki udaku udaku. Pili, Jengo ni la Zaid Baraka ambaye anadaiwa na TRA, hivyo jengo lake limepigwa mnada ili kulipa deni la TRA. Mhe.Mungai ndiye aliyenunua jengo la Zaid Baraka lililouzwa kwa mnada. Mungai amelinunua jengo hilo kwa bei hiyo, kupitia kwa wakala wake, Vitus Mushi, hivyo risiti imeandikwa jina lake.
Jamaa Iringa ni deal sana kununua Jengo kwa Milioni 315.
Hii siyo issue ila labda ni uthibitisho wa kuwa Mhe. Hajaikimbia nchi ndio maaana anazidi kuwekeza.
 
Uwakala sitatizo kabisa, kwani watu huaminiana hata kumtuma rafiki yake kwenda Unguja kumwolea, halafu akaletewa mke tayari ndoa imeshafungwa ati!!!

Hayo mengine nimekuelewa vizuri, ila Dah!, huo mfano niliowekea rangi kweli ni mgumu sana kueleweka; teh!!! teh!! teh!!! teh!!! ati rafiki yake akafanye nini?
 

Pamoja na kwamba hapa kila mtu anao uhuru wa kutoa hoja ,lakini tafadhali tusiiaibishe hii forum. Kama hujui lugha omba usaidiwe na jirani yako hapo cafe , au stop posting zile ambazo ni non sense language wise etc. Mtu kununua kitu manadani kwa bei ya juu sio issue. Mtoa mada ulitaka anunue kwa bei wakati ni mnada?
 
Hayo mengine nimekuelewa vizuri, ila Dah!, huo mfano niliowekea rangi kweli ni mgumu sana kueleweka; teh!!! teh!! teh!!! teh!!! ati rafiki yake akafanye nini?

Kichuguu,

Mbona hii ni common sana, kwa Mfano wewe unataka mke na siku ya kuoa labda una shughuli nyingi basi unamtuma rafiki yako akakuolee then anakuletea mkeo nyumbani.

Au wengine siku ya harusi kama bi Mkubwa kapiga bit kuwa huoi, basi simu ya kiganjani tu huweza kumaliza kila kitu, ni kiasi cha kuingia chooni na kumtaarifu rafiki yako akuwakilishe, afunge ndoa kwa niaba yako.
Nadhani huko tunakokwenda huenda tutaweza kufunga ndoa kwa kutumia internet labda.
 
Naona Sir Leem alikuwa akimaanisha kuwa Mungai amelinunua ilo jengo kwa mil315 wakati thani halisi ni mil200.
Na kwa upande mwingine Sir Leem atakuwa anashangazwa na izo senti toka kwa huyu mwekezaji mwenye asili ya Kikenya.
Ndivyo nilivyomuelewa sisi ambao tuna background za ualimu na kuzoea kumark essays mbalimbali.
Kwa upande wangu huyu mzee ana hamu na keko hasa ktk vugu vugu la sasa na hawa mafisadi laweza mkumba bure.Mil 315 ni hela nyingi kwa kada wa chama kama huyu na aliyekuwa wazili zamani tena wa Elimu?
 

Uuuh yeah, I have no comments!
 
Mkuu
Sasa nakubali Kiswahili nacho Watanzania kinatupa shida. Kunadi vs kununua, wakala vs mdaiwa. Sir Leem, unaweza kutueleza kwa lugha nyingine tukaelewa hata kama tutahitaji mkalimani?

Mkuu, sidhani JF ina members Watanzania pekee. You may never know!
 
Nahisi mtoa bandiko ana wasi na utajiri wa mungai au hajui mungai ana utajiri kiasi gani.....pia mungai ana madhumuni ya hilo jengo ndio maana amepanda dau ili wengine wasimpiku....nadhani ni kawaida tu kama muwekezaji mzalendo...na kama pesa yake ni halali maana sio ya kifisadi ruksa kuwekeza.....
 
Mkuu, sidhani JF ina members Watanzania pekee. You may never know!

Amin Mkuu
Basi kama si Mtanzania au Kiswahili kinampa shida atumie lugha anayoijua yeye halafu hapa JF tutapata mkalimani, JF familia kubwa! Ametumia Kiswahili na sijaelewa, labda mimi ndio sio Mswahili lol
cheers Mkuu Sinkala, hata hivyo tuko pamoja.
No P, nimeelewa kupitia ufafanuzi wa wanaJF wengine
 
mungai amesharudi wakuu ni miaka mitano sasa.
 
Mmeacha mambo ya msingi mnaleta habari za mungai/udaku..vip loliondo na ngorongoro mgogoro wa ardhi umeisha?
 
mkuu kumbe ulimuombea mabaya marehem siku nyingi tu duh!!
 
mkuu kumbe ulimuombea mabaya marehem siku nyingi tu duh!!
Mkuu Mwalla, mtu akiishatangulia mbele ya haki, sio busara kuanza kufukua makaburi ya watu walifanya nini au walisema nini huko nyuma. Mtu akiishatangulia mbele ya haki, tumzungumze kwa wema kwa kukumbuka tuu yale mazuri ya merehemu.

RIP Joseph Mungai.
Paskali
 
Haya makaburi mengine yanatisha. Ukifukua mchanga wa kurudishia hautoshi
 
Haya makaburi mengine yanatisha. Ukifukua mchanga wa kurudishia hautoshi
DAWA YA KABURI NI KULIJENGEA NA IKIWEZEKANA UNAJENGA NA KA MNARA KAMA LILE KABURI LA NYUNDO PALE LUNDAMATWE FAIDA YAKE WANAOHUSIANA NA MAREHEMU WAKIONA MAMBO YANAWAENDEA SIVYO WATAKWENDA KUSEMBUA KABURI KWA HIYO CCM WAACHENI WASIFUKUE ILA TUKIWABANA UTAONA WANAKWENDA KUSAFISHA AU KUSEMBUA ILI MAREHEMU AKAWAPIGIE MZINGA KWA MUNGU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…