Kuhusu data: Zitto "ambishia" Rais Magufuli

Kuhusu data: Zitto "ambishia" Rais Magufuli

Sure mkuu. Zitto yupo vizuri sana up stairs. Huwezi kubishana naye kama hujajipanga. Natamani kama pangekuwa na mdahalo kati yake na mkulu kuhusu hii issue, halafu uwe live . Hapo tungemaliza ubishi kiroho safi.

Mkuu kua makini maana wazee wa Lumumba hawachoki kufungua kesi za uchochezi
 
Anaandika kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe

Taarifa yetu kuhusu ' kupikwa ' Kwa takwimu za Pato la Taifa tutaitoa mara baada ya kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Act Wazalendo kitakachoketi 28/10/2017. Sheria ya Takwimu aliyotaja Rais kutaka itumike kuziba watu midomo haizuii tafsiri za Takwimu zinazotolewa na Serikali.

Tunatumia takwimu za Serikali kuonyesha kuwa Serikali inadanganya Kwa kutokusema ukweli wote wa uhalisia wa uchumi na kuporomoka Kwa mapato. Ni sawa na mtu anayesema Glasi ni ' half empty or half full ' kwani anasema kitu kile kile.

Kwa mfano, Rais anaposema kuwa Serikali inatekeleza miradi mikubwa Kwa kutumia ongezeko la kodi anakuwa anadanganya Wananchi na anafanya hivyo akijua anadanganya. Rais anajua kuwa Deni la Taifa limeongezeka Kwa TZS 6.5trn katika miaka yake miwili ya urais. ( Deni la Nje limeongezeka Kwa US$1.5bn ( TZS 4.5trn) kati ya July 2016-July 2017. Deni la ndani limeongezeka Kwa TZS 2trn katika kipindi hicho.

Soma . http://www.bot.go.tz/Publications/MonthlyEconomicReviews/MER August 2017 Final.pdf ).

Pia Rais anajua kuwa Serikali inatumia, bila kufuata sheria, Fedha za Mashirika ya Umma zilizopo Benki Kuu kulipia baadhi ya Miradi yake. Kukiuka sheria za Fedha ni kosa la jinai na wakati mwengine kosa la kikatiba kwani Katiba imeweka utaratibu wa masuala ya Fedha za Umma.

Kodi inayokusanywa na TRA inaweza kulipa mishahara na kuhudumia Deni la Taifa tu. Kwanini Rais wetu hasemi kuwa tunakopa? Kukopa sio dhambi, kwanini aaminishe watu kuwa anatekeleza miradi Kwa kuwa kodi zimeongezeka? Kama Rais anaamini kuwa Mapato hayajaporomoka, aruhusu ukaguzi maalumu wa CAG kwenye Mapato ya July na Agosti 2017 na ukaguzi huo uwekwe wazi Kwa umma.

Rais akifanya hivyo NITAWAJIBIKA
Hivi wewe Kabwe jiulize mara mbili, Sio kila kitu kupinga tu.
Madini yapo hata tandale, embu mlete muwekezaji ambaye yupo tayali kufuata unachosema.
Alafu rudi uandike kuwa hakupewa ushilikiano.
Sio mboga apike mwingi ne kazi yako kusema haina bizali haifai kuliwa na ugali wakati wenzako wanaitisha sahani ya pili ya ugali.

Jifunze kuwa mbunifu, usipande kuwa mwendelezaji.
 
Ukiwa na ligi na zitto uwe na takwimu za kutosha sasa kwa huyu kiongozi wetu nina mashaka naye na takwimu zake. Msema kweli mpenzi wa Mungu. Mara zote Zitto ni Mkweli.
Maprofesa wapo wa kuunda timu kumjibu Zitto
 
Zito hajasema kukopa ni Dhambi, amesema kukopa lazima ipitishwe na Bunge na hio ndio sheria, sio kukopa kisiri halafu ukadanganya
Bunge pamoja na Kutunga sheria za nchi lipo kuisimamia Serikali.
Sasa kunamaana gani kuwa na wabunge na wakalipwa mishahara minono na Mashangingi ikiwa hawawezi kufanya ile kazi walioajiriwa. Bora afute Bunge hizo Pesa zielekezwe kwenye Miradi tu
Mkuu Mtambwe nimekuelewa sana,
Wewe ni Great Thinker hilo halina ubishi kabsaaaaa.
 
Hivi wewe Kabwe jiulize mara mbili, Sio kila kitu kupinga tu.
Madini yapo hata tandale, embu mlete muwekezaji ambaye yupo tayali kufuata unachosema.
Alafu rudi uandike kuwa hakupewa ushilikiano.
Sio mboga apike mwingi ne kazi yako kusema haina bizali haifai kuliwa na ugali wakati wenzako wanaitisha sahani ya pili ya ugali.

Jifunze kuwa mbunifu, usipande kuwa mwendelezaji.

jufunze kwanza kiswahili fasaha....shubbbamit!!!
 
Hivi wewe Kabwe jiulize mara mbili, Sio kila kitu kupinga tu.
Madini yapo hata tandale, embu mlete muwekezaji ambaye yupo tayali kufuata unachosema.
Alafu rudi uandike kuwa hakupewa ushilikiano.
Sio mboga apike mwingi ne kazi yako kusema haina bizali haifai kuliwa na ugali wakati wenzako wanaitisha sahani ya pili ya ugali.

Jifunze kuwa mbunifu, usipande kuwa mwendelezaji.
Acha maneno weka data kupinga. Data hupingwa kwa data.
 
Haya Lumumba si mnataka Zitto awajibike kashatoa njia rahisi. Mchongoko ni mpishi wa data
 
Zitto na Lissu ilikuwa combination Nzuri sana. Basi tu shetani aliingilia kati. hatuwezi kuwa tunaburuzwa na mtu mmoja huyo huyo ana tumia pesa vibaya bila utaratibu, huyo huyo kila siku anavunjwa katiba, huyo huyo kila siku anafukuza na kuteua watu tena. shida ni yeye au anaowaongoza.
 
Zito hujui kuwa bajeti ya serikali mapato yake hutokana na makusanyo ya ndani na mapato ya Nje?

Kosa la rais kutekeleza kwa pesa za kukopa si kuvunja Sheria. Uchumi wa Nchi yetu bado haujafikia hatua ya kujitosheleza kulipia bajeti yote.
Kauli ya Mhe rais kuhusu kuongezeka kwa makusanyo ya ndani ni kweli acha kupotosha takwimu za serikali.
Naamini sasa umebaki unalia kama debe tupu huku ukidhani utaendelea kuwadanganya watanzania hutaweza
Ishu ni kwanini anadanganya na anakopa kwa siri?
 
Watanzania wote tukiwa na akili kama zako, hata kobe ataweza kutuongoza.
Zito hujui kuwa bajeti ya serikali mapato yake hutokana na makusanyo ya ndani na mapato ya Nje?

Kosa la rais kutekeleza kwa pesa za kukopa si kuvunja Sheria. Uchumi wa Nchi yetu bado haujafikia hatua ya kujitosheleza kulipia bajeti yote.
Kauli ya Mhe rais kuhusu kuongezeka kwa makusanyo ya ndani ni kweli acha kupotosha takwimu za serikali.
Naamini sasa umebaki unalia kama debe tupu huku ukidhani utaendelea kuwadanganya watanzania hutaweza
 
Ila swali la msingi ni kwa nini Zitto hakamatwi kwa uchochezi?

Naomba nisaidiwe hapo, huyu jamaa hajawahi kulala Polisi na wala hana hata kesi moja mahakamani.

Hiki ni kitengo.
hakika!
 
Zitto na Lissu ilikuwa combinaion Nzuri sana. Basi tu shetani aliingilia kati. hatuwezi kuwa tunaburuzwa na mtu mmoja huyo huyo ana tumia pesa vibaya bila utaratibu, huyo huyo kila siku anavunjwa katiba, huyo huyo kila siku anafukuza na kuteua watu tena. shida ni yeye au anaowaongoza.
Swadakta mkuu
 
Hana lolote kazimiss hizi safari za kufuja jasho la walipa kodi wa Tanzania chini ya msafara wa kikwete
IMG_20171024_145004.jpg
 
Back
Top Bottom