Kuhusu data: Zitto "ambishia" Rais Magufuli

Kuhusu data: Zitto "ambishia" Rais Magufuli

Hivi nikabila gani wanaongoza kwa ubishi hapa Tanzania.
 
Ukiwa na ligi na zitto uwe na takwimu za kutosha sasa kwa huyu kiongozi wetu nina mashaka naye na takwimu zake. Msema kweli mpenzi wa Mungu. Mara zote Zitto ni Mkweli.
Sure mkuu. Zitto yupo vizuri sana up stairs. Huwezi kubishana naye kama hujajipanga. Natamani kama pangekuwa na mdahalo kati yake na mkulu kuhusu hii issue, halafu uwe live . Hapo tungemaliza ubishi kiroho safi.
 
Zito hujui kuwa bajeti ya serikali mapato yake hutokana na makusanyo ya ndani na mapato ya Nje?

Kosa la rais kutekeleza kwa pesa za kukopa si kuvunja Sheria. Uchumi wa Nchi yetu bado haujafikia hatua ya kujitosheleza kulipia bajeti yote.
Kauli ya Mhe rais kuhusu kuongezeka kwa makusanyo ya ndani ni kweli acha kupotosha takwimu za serikali.
Naamini sasa umebaki unalia kama debe tupu huku ukidhani utaendelea kuwadanganya watanzania hutaweza

hebu soma vizuri uelewe .... alimaanisha nini.. ????
 
Anaandika kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe

Taarifa yetu kuhusu ' kupikwa ' Kwa takwimu za Pato la Taifa tutaitoa mara baada ya kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Act Wazalendo kitakachoketi 28/10/2017. Sheria ya Takwimu aliyotaja Rais kutaka itumike kuziba watu midomo haizuii tafsiri za Takwimu zinazotolewa na Serikali.

Tunatumia takwimu za Serikali kuonyesha kuwa Serikali inadanganya Kwa kutokusema ukweli wote wa uhalisia wa uchumi na kuporomoka Kwa mapato. Ni sawa na mtu anayesema Glasi ni ' half empty or half full ' kwani anasema kitu kile kile.

Kwa mfano, Rais anaposema kuwa Serikali inatekeleza miradi mikubwa Kwa kutumia ongezeko la kodi anakuwa anadanganya Wananchi na anafanya hivyo akijua anadanganya. Rais anajua kuwa Deni la Taifa limeongezeka Kwa TZS 6.5trn katika miaka yake miwili ya urais. ( Deni la Nje limeongezeka Kwa US$1.5bn ( TZS 4.5trn) kati ya July 2016-July 2017. Deni la ndani limeongezeka Kwa TZS 2trn katika kipindi hicho.

Soma . http://www.bot.go.tz/Publications/MonthlyEconomicReviews/MER August 2017 Final.pdf ).

Pia Rais anajua kuwa Serikali inatumia, bila kufuata sheria, Fedha za Mashirika ya Umma zilizopo Benki Kuu kulipia baadhi ya Miradi yake. Kukiuka sheria za Fedha ni kosa la jinai na wakati mwengine kosa la kikatiba kwani Katiba imeweka utaratibu wa masuala ya Fedha za Umma.

Kodi inayokusanywa na TRA inaweza kulipa mishahara na kuhudumia Deni la Taifa tu. Kwanini Rais wetu hasemi kuwa tunakopa? Kukopa sio dhambi, kwanini aaminishe watu kuwa anatekeleza miradi Kwa kuwa kodi zimeongezeka? Kama Rais anaamini kuwa Mapato hayajaporomoka, aruhusu ukaguzi maalumu wa CAG kwenye Mapato ya July na Agosti 2017 na ukaguzi huo uwekwe wazi Kwa umma.

Rais akifanya hivyo NITAWAJIBIKA
Zitto yuko sahihi, na amejibu sahihi kabisa. amefanya vizuri kutoogopa vitisho. maana tatizo la JPM huwa hawezi kabisa kujenga hoja bila vitisho kwa wale wanaompinga au kumkosoa, au kujionesha kwamba yeye yuko sahihi asilimia miamoja na kuomba watu wamwombee. Zitto amekaa kwenye kamati ya bunge ya hesabu za mashirika, anajua anachoongea. Bravo Zitto!! Japokuwa sipendi sana siasa zako, lakini kwa hili nakuunga mkono bila chenga!
 
Zito hujui kuwa bajeti ya serikali mapato yake hutokana na makusanyo ya ndani na mapato ya Nje?

Kosa la rais kutekeleza kwa pesa za kukopa si kuvunja Sheria. Uchumi wa Nchi yetu bado haujafikia hatua ya kujitosheleza kulipia bajeti yote.
Kauli ya Mhe rais kuhusu kuongezeka kwa makusanyo ya ndani ni kweli acha kupotosha takwimu za serikali.
Naamini sasa umebaki unalia kama debe tupu huku ukidhani utaendelea kuwadanganya watanzania hutaweza
Zito hajasema kukopa ni Dhambi, amesema kukopa lazima ipitishwe na Bunge na hio ndio sheria, sio kukopa kisiri halafu ukadanganya
Bunge pamoja na Kutunga sheria za nchi lipo kuisimamia Serikali.
Sasa kunamaana gani kuwa na wabunge na wakalipwa mishahara minono na Mashangingi ikiwa hawawezi kufanya ile kazi walioajiriwa. Bora afute Bunge hizo Pesa zielekezwe kwenye Miradi tu
 
Ila swali la msingi ni kwa nini Zitto hakamatwi kwa uchochezi?

Naomba nisaidiwe hapo, huyu jamaa hajawahi kulala Polisi na wala hana hata kesi moja mahakamani.

Hiki ni kitengo.
Kitengo kinachopopoa
Nyinyi akili stagnant mna matatizo sana
 
Zito hujui kuwa bajeti ya serikali mapato yake hutokana na makusanyo ya ndani na mapato ya Nje?

Kosa la rais kutekeleza kwa pesa za kukopa si kuvunja Sheria. Uchumi wa Nchi yetu bado haujafikia hatua ya kujitosheleza kulipia bajeti yote.
Kauli ya Mhe rais kuhusu kuongezeka kwa makusanyo ya ndani ni kweli acha kupotosha takwimu za serikali.
Naamini sasa umebaki unalia kama debe tupu huku ukidhani utaendelea kuwadanganya watanzania hutaweza
Umemuelewa?
 
Hujamwelewa Zitto. Serikali inatumia fedha za mashirika zilizowekwa benki kuu, kinyume cha utaratibu. hiyo ndiyo hoja yenyewe.
 
Back
Top Bottom