Kuhusu Corona, kwa ukimya huu kwenye social media, hakuna sababu ya kutilia shaka taarifa za serikali

Kingjr2

JF-Expert Member
Sep 8, 2018
622
1,000
Wasalaam,

Niende kwenye mada moja kwa moja

Kipindi kile serikali inatoa takwimu za maambukizi na vifo vya Covid-19 mara kwa mara huku kwenye mitandao ya
kijamii yaliibuka mengi ambayo kwa asilimia kubwa yaliaminika:

Wengi tulitilia shaka takwimu zilizotolewa na serikali hivyo mitandao ya jamii ilisheheni:-

Shuhuda za jinsi wapendwa wetu wanavyozikwa usiku na ndugu kupigwa mkwara wasisambaze taarifa

Wengine walikuja na taarifa za uwepo wa wagonjwa wengi mahospitalini.

Wengine walikuja na shuhuda za wapendwa wao kukosa huduma hospitali.

Tangu serikali isitishe kutoa takwimu na kusisitiza maambukizi yamepungua hayo yote hayapo tena kwenye mitandao

Kwasababu watu hawalalamiki kama zamani, hii ni indicator mojawapo kwamba yanayosemwa na serikali ni sahihi maana hakuna malalamiko tena huku mitandaoni.
 
Administer

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
344
500
Wasalaam,

Niende kwenye mada moja kwa moja

Kipindi kile serikali inatoa takwimu za maambukizi na vifo vya Covid-19 mara kwa mara huku kwenye mitandao ya kijamii yaliibuka mengi ambayo kwa asilimia kubwa yaliaminika:

Wengi tulitilia shaka takwimu zilizotolewa na serikali hivyo mitandao ya jamii ilisheheni:-

Shuhuda za jinsi wapendwa wetu wanavyozikwa usiku na ndugu kupigwa mkwara wasisambaze taarifa

Wengine walikuja na taarifa za uwepo wa wagonjwa wengi mahospitalini

Wengine walikuja na shuhuda za wapendwa wao kukosa huduma hospitali

Tangu serikali isitishe kutoa takwimu na kusisitiza maambukizi yamepungua hayo yote hayapo tena kwenye mitandao

Kwasababu watu hawalalamiki kama zamani, hii ni indicator mojawapo kwamba yanayosemwa na serikali ni sahihi maana hakuna malalamiko tena huku mitandaoni
IPO INAUWA
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
5,974
2,000
Kigogo keshatoa update jana nenda kacheki.

Labda kama hudhani twitter nayo ni social media

Kwenye Korona serikali imejitoa, Ukifikwa you are on your own, serikali imeshajitoa, hata kuzika sasa utazika mwenyewe tena bila wale jamaa wavaa PPE kuwepo, ukijicontaminate shauri yako!

Ukienda hospitali ukionyesha dalili za Korona hupokelewi

Ukifia nyumbani kwa dalili zote za Korona hakuna postmortem kwa hiyo hutopata ushahidi wa kusema mtu wako kafa kwa korona

Mgonjwa akibahatika akapata hospitali na akafa kwa korona, madaktari "wanashauriwa" waandike magonjwa mtambuka kama sababu ya kifo

Kwa hiyo njia zote za kupata taarifa official zimezibwa!

Hata madereva wetu wa Malori wanaokutwa na Korona tumeomba nchi jirani isitaje uraia wao

Kwa hiyo hata hao wanaosema Imepungua haijaisha ni kwa sababu wanaona aibu kusema imeisha maana hata wao data za kuwaambia kuwa imepungua hawana wanatumia tu instincts zao

Nakushauri usiwe kama mbayuwayu, za kuambiwa changanya na zako!
 
Hii nimeielewa hasa hapo kwa madaktari
 
troublemaker

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
14,740
2,000
Hii ndio bongo bana😀😀
"Tuchapeni kazi kujenga uchumi wetu"(Bashite) Huu upepo utapita na tutasahau, na hivi ni wepesi kusahau.
 
crocodile

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,749
2,000
Kigogo keshatoa update jana nenda kacheki.

Labda kama hudhani twitter nayo ni social media

Kwenye Korona serikali imejitoa, Ukifikwa you are on your own, serikali imeshajitoa, hata kuzika sasa utazika mwenyewe tena bila wale jamaa wavaa PPE kuwepo, ukijicontaminate shauri yako!

Ukienda hospitali ukionyesha dalili za Korona hupokelewi

Ukifia nyumbani kwa dalili zote za Korona hakuna postmortem kwa hiyo hutopata ushahidi wa kusema mtu wako kafa kwa korona

Mgonjwa akibahatika akapata hospitali na akafa kwa korona, madaktari "wanashauriwa" waandike magonjwa mtambuka kama sababu ya kifo

Kwa hiyo njia zote za kupata taarifa official zimezibwa!

Hata madereva wetu wa Malori wanaokutwa na Korona tumeomba nchi jirani isitaje uraia wao

Kwa hiyo hata hao wanaosema Imepungua haijaisha ni kwa sababu wanaona aibu kusema imeisha maana hata wao data za kuwaambia kuwa imepungua hawana wanatumia tu instincts zao

Nakushauri usiwe kama mbayuwayu, za kuambiwa changanya na zako!
Na nchi zingine nako imepungua sana, sasa bwana akili nyingi tuambie na wao pia wanafanya hivi?!
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
5,974
2,000
Na nchi zingine nako imepungua sana, sasa bwana akili nyingi tuambie na wao pia wanafanya hivi?!
Hujaona South Korea wamefunga tena shule baada ya ishu kuibuka upya?

Kule Brazil ambako rais wao alikuwa na mawazo kama ya Magufuli huoni korona imepamba kasi?

Kule Urusi kwa Putin waliojifanya kuwa wako salama huoni sasa hivi korona imechachamaa kama pilipili?
 
crocodile

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,749
2,000
Hujaona South Korea wamefunga tena shule baada ya ishu kuibuka upya?

Kule Brazil ambako rais wao alikuwa na mawazo kama ya Magufuli huoni korona imepamba kasi?

Kule Urusi kwa Putin waliojifanya kuwa wako salama huoni sasa hivi korona imechachamaa kama pilipili?
Kwa mifano hiyo ndio tuseme na sisi imepamba moto? Asante na kwa mifano na wewe nakupa mmoja. Vietnam; population 97,000,000. Inapakana na China, wagonjwa wamepungua mpaka zero na hamna kifo. Vipi hao na wako Dunia moja na akina Brazil?!
 
Ngatele

JF-Expert Member
Jan 25, 2011
613
500
Kila mtu anapambana kivyake. Corona ipo, nawa mikono na maji tililika na vaa barakoa.

Naona watu wengi sasa hawavai barakoa wala kunawa mikono. Naona hata mikusanyiko ya wakuu hakuna hata mtu mmoja mwenye barakoa na hakuna umbali unaotakiwa kati ya mtu na mtu, mambo ni kama hakuna Corona.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom