Kuhusu Afya; Ahadi ya CCM kwa wananchi

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
34,352
2,000
ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020


Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Chama Cha Mapinduzi
kitaendelea kutoa kipaumbele katika sekta ya afya kwa kuwa inagusa
maisha ya Watanzania na ustawi wa Taifa letu. Lengo la Chama ni
kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya na siha bora ili kuwawezesha
kushiriki katika shughulli za ujenzi wa Taifa na kuboresha maisha yao.
Katika kipindi hicho, Chama kitasimamia Serikali katika kutekeleza
yafuatayo:
(a) Kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto na kuzitoa bila malipo
ili kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto wenye umri
chini ya miaka mitano;
(b) Kuimarisha upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba, vifaa saidizi na
vitendanishi kulingana na mahitaji katika ngazi zote za utoaji wa
huduma za afya nchini;
(c) Kuweka mazingira kwa wawekezaji/sekta binafsi kujenga viwanda
vya kuzalisha dawa, vifaa, vifaa tiba, vifaa saidizi na vitendanishi kwa
kutumia malighafi zinazopatikana ndani ya nchi ili kupunguza mzigo
kwa Serikali wa kuagiza mahitaji hayo kutoka nje ya nchi;
(d) Kujenga na kuimarisha vituo vya kutolea huduma za afya ili viweze
kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi. Hadi kufikia 2025 Serikali
itaongeza vituo vya kutolea huduma za afya kwa asilimia 20 ya vituo
8,446 vilivyopo sasa; vipaumbele vitawekwa katika ujenzi wa vituo
vya afya na ukamilishwaji wa maboma kwa kuzingatia uwiano wa
kijiografia, idadi ya watu na wingi wa magonjwa;
(e) Kuimarisha mfumo wa bima ya afya nchini ikiwemo mifuko ya bima
za afya (NHIF na CHF) ili kufikia lengo la Serikali la kuwa na bima ya afya.


Mapambano Dhidi ya Magonjwa ya Mlipuko ikiwemo Corona
84. Magonjwa ya mlipuko na yanayosambaa kwa kasi ni hatari kwa maisha ya
wananchi na ulinzi na usalama wa Taifa. CCM itahakikisha nchi inakuwa
na utayari wakati wote wa kuzuia, kudhibiti na kukabiliana na majanga
haya kwa kushirikiana na wadau wengine. Janga la Corona lililoikumba
dunia ikiwemo Tanzania limetupa funzo kubwa kuhusu umuhimu wa
kujipanga kikamilifu katika kukabiliana na majanga ya aina hii punde
yanapojitokeza. Katika kufikia azma hii, CCM itahakikisha Serikali
inatekeleza yafuatayo:-
(a) Kuweka na kuimarisha mifumo na miundombinu ya kutambua,
kudhibiti na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na yanayoenea
kwa kasi;

(b) Kuimarisha mpango wa Taifa wa utayari wa kukabiliana na magonjwa
ya mlipuko, ajali na majanga kwa kuboresha huduma za dharura na
uokoaji ikiwemo miundombinu, na vitendea kazi;

(c) Kuimarisha na kujenga uwezo wa kufanya utafiti kuhusu magonjwa
ya mlipuko katika taasisi ya NIMR, vyuo vikuu na taasisi nyingine za
utafiti nchini;

(d) Kuanzisha kituo kikubwa cha utafiti na uchunguzi wa mimea dawa
na kuanzisha kiwanda cha kimkakati cha kuzalisha dawa zitokanazo
na mimea yetu;

(e) Kuimarisha uwezo wa wataalam wetu katika kuzuia na kutibu
magonjwa ya mlipuko kwa kupatiwa vifaa na mafunzo ndani na nje
ya nchi; na

(f) Kujenga na kuimarisha maabara za uchunguzi wa magonjwa ya
mlipuko, vituo vya kisasa vya kuwatenga wahisiwa (isolation centres)
na kutoa tiba kwa wagonjwa.


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom