Kwanza kabisa, kuhonga si kumhudumia mpenzi wako.
Mpenzi wako akiumwa na kuhitaji kuhudumiwa nawe, kumhonga hakuwezi kumsaidia kupata anachotaka.
Pili, kumhudumia mpenzi wako kuko kwa namna nyingi sana. Kuhonga ni njia rahisi sana na ya kimasikini kabisa ya kumhudumia mpenzi wako.
Ni kitu unaweza kufanya bila hata kuwa naye, si unamtumia hela tu.
Kumhudumia mpenzi wako kiukweli kabisa kunataka zaidi ya hela, kunataka kutumia muda wako naye.
Mambo haya watu wengi wa jamii zilizojaa umasikini ambao mawazo yao yamekaa kwenye kufanya mapenzi kuwa ni transactional kwenye kuhonga hela na material things hawawezi kuelewa.
Kwa sababu umasikini na tamaa vimewaziba uwezo wa kuelewa.