Kuhama Tahsusi

Kuhama Tahsusi

Monda kubwa

Senior Member
Joined
Jun 20, 2019
Posts
121
Reaction score
157
Natamani kufahamu, kuna mdogo wangu alimaliza Form 4. Alipata division 2 ya point 19. Nilitaka asome PCM au PCB lakini selection zimekuja wamemchagua EGM. Na shule anayoenda hakuna hizo tahsusi mbili (PCM na PCB). Kuna PGM tu.

Naomba mnieleweshe kidogo kuhusu hii tahasusi ya (EGM). Je, akiisoma anaweza kuwa na future nzuri. Ni kazi zipi mtu anaweza kufanya mtu akiwa kasoma EGM?
 
Ww soma yoyote unaweza kusoma pcm au pgm au PCB lakn ukaishia kuwa Konda au mpga debe. Kusoma sio ishu, ishu ni kuigeuza elimu kuwa pesa
 
Kwa upendo, kama dogo anataka(sio wewe) mwambie akapige pcb au cbg kama anataka kuajiriwa fasta hapo baadae. Maana humo atasoma mambo ya afya na haya kila siku watu wanasurvive kirahisi.

Lakini kama anataka kuwa mpambanaji basi mwambie akasome hayo mengine.
 
Watu bhana hakuna elimu isiyo na faida,hakuna ujuzi usiolipa, hahaa soma pambana na soko,geuza elimu kuwa hela,weka malengo na uyapambanie sana,tengeneza network yenye faida ya watu,nidhamu,bidii n kujituma, sala na maombi...nk YAANI MPAKA LEO HUYO DOGO HAJUI ANATAKA KUWA NANI/ANA MALENGO GANI KWENYE MAISHA?? Any way apige pcb aje kuwa dr ina soko town kwa ushauri lkn....
 
Yaan wee ndio unapenda na sio yeye? But anyway kila kheri ktk kutimiza ndoto zake.
 
Back
Top Bottom