Kufutwa mbio za Mwenge mwanzo wa anguko la CCM

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,926
31,169
Tangu enzi za Mwl. Nyerere hadi utawala wa Rais Magufuli Mwenge umekuwa ukikimbizwa maeneo yote ya Tanganyika na Zanzibar.

Mbio za Mwenge ni ibada kama zilivyo ibada za imani nyingine. Unaposhiriki mbio za Mwenge unafanya Ibada usiniulize kama ni sahihi au batili inategemea mtazamo wako.

Ninaamini Mwenge umekuwa ukipumbaza waTanzania namna ya kufikiri na kuamua kwa miongo mingi.

Mwaka huu mbio za Mwenge zilisitishwa kwasababu ya mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19. Mwaka huu Tanzania inatarajiwa kufanya Uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba kafara la Mwenge halitakuwepo hivyo kupelekea wapiga kura wengi kutumia akili zao sawa sawa na mapenzi ya Mungu.

Ngongo safarini Kilombero
 
Fedha zilizokua zinaufadhili huo mwenge kuzunguka zilipangiwa kazi nyingine?
 
Miaka ya nyuma siku moja kulikua namkesha wa mwenge karibu na makaaxzi yangu. Ilikua ktk uwanja wa Halmashauri. Asubuhi nikawa napita zangu kukatisha uwanjani. Kila hatua kadhaa, mbele yangu, kulia nakushoto kulikua na condom zilizo tumika. Nikawaza: kuna hawa waliotumia hizi zana, lakini kuna wengine wengi walingonoka bila zana. Tangu siku hiyo mimi na mwenge mbalimbali
 
Kafara la Mwenge si lakitoto,Viongozi wazi na PhD za hawalali wanakesha usiku kucha,ukiwauliza nini faida za Mwenge watakujibu unaleta upendo sijui mshikamano na blah blah kibao ambazo ukizichunguza hazina uhusiano na Mwenge.
Nami sijawahi kueewa mantiki ya kukimbiza mwenge kabisa. Wanasema unazindua miradi ya maendeleo, kwani bila mwenge miradi hii haiwezi kuzinduliwa? Mbona mzee baba kazindua miradi kadhaa Dodoma bila mbio za mwenge?
 
Nisaidieni jamani: (Think critically) Faida za mwenge ni zipi? Hasara nazijua baadhi:-
1. matumizi mabaya ya fedha na rasilimali.
2. Mwenge una mchango mkubwa sana kueneza ukimwi.
3. Moshi ule unachangia sana ongezeko wagonjwa wa T.B.
 
Hata mimi sijui. Lakini je! tuwe na mwenge kwakigezo kwamba hata wengine wannao? Au tusiwe nao kwa vile wengine hawana?
Kama mwenge ni utamaduni basi hasara yake ni kuukana huo utamaduni, kwa ninavyojua utamaduni hulindwa kwa gharama kubwa.
 
Kimsingi inabidi unifundishe sana na pengine nisome vitabu vyote duniani ndiyo naweza nikahisi naelewa dhana ya kukimbiza mwenge, labda ungekua ni mchezo kama riadha
 
Ni ninyi mlikua mkipinga mbio za mwenge na kudai hazina tija na ni ubadhilifu wa fedha za walipa kodi
 
Back
Top Bottom