Wana JF,
Napenda kujadili hii hoja ya kufutwa kwa kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma (POAC) kwa sababu mazingira ya kufutwa kwake yana utata pamoja na kamati ya ulinzi. Kufutwa kwa POAC kwa harakaharaka naona kama ni maandalizi ya EPA nyingine kuelekea 2015.
Nasema hivyo kwa sababu hii kamati imekuwa kamati muhiomu sana ndani ya bunge kwa kujadili matumizi ya pesa katika mashirika ya umma. kufutwa kwake kutatoa mwanya wa matumizi mabaya ya pesa za wananchi katika mashirika ya umma na kama imefutwa kwa makusudi na serikali taafsiri yake ni kuwa serikali inampango wa kufanya ufisadi katika mashirika ya umma na hii moja kwa moja ni mbinu teule kuelekea 2015.
Spika Anna Makinda wakati akifuta hii kamati alisema kazi hiyo itafanywa na PAC jambo ambalo aliyekuwa mwenyekiti wa poac, ZZK amepinga akisema PAC haitaweza kusimamia wizara za serikali na mikoa pamoja na mashirika ya umma kwani hata POAC yenyewe ilikuwa inashindwa kupitia taarifa za mashirika yote 258 ya umma kwa mwaka. Kwa maana hiyo hapa kinachoonekana ni kufanya PAC kushindwa kukagua hesabu hizo za mashirika ya umma hivyo kutoa mwanya wa kupiga EPA nyingine.
Kwa viongozi wapenda maendeleo POAC ingeboreshwa zaidi ili kupunguza matumizi mabaya ya pesa za umma.
Yangu macho ebu tusubiri tuone.
=============
Kuna uchambuzi mwingine umefanywa na Petro E. Mselewa hapa -> https://www.jamiiforums.com/great-t...ipi-kosa-la-zitto-na-kamati-yake-ya-poac.html unafaa kusomwa pia

Napenda kuuliza swali hili ili kuweka kumbukumbu vizuri:
Hapo nyuma tuliambiwa kuwa POAC iligundua kuwa wakorea wako hatarini kufuta mkopo wao walioahidi kwa Tanzania uliokuwa utumike kujenga chuo kikuu cha afya Muhimbili katika ardhi yenye utata huko Mlongazila. Baadae tuliona michoro ya ujenzi wa chuo hiki ikitolewa kama mafanikio ya serikali ya CCM.
Kwa sasa sina uhakika ni fedha zipi zitatumika kujenga chuo hiki!
Walioibuwa hoja hii ya kupokonywa mkopo huu ni POAC chini ya Zitto na sasa tunaambiwa POAC imefutwa na Makinda.
Swali langu ni hili: Je, wakorea wameshaufuta huu mkopo wao? Kama ni hivyo nini kinaendelea?
Je, maazimio ya POAC yatatekelezwa au yatafutika kama ilivyofutika POAC?
ALIYELETA THREAD HII NI MUHITIMU WA FANI YA UDAKTARI MUHIMBILI!