Unajua ule ujanja ujanja kuna siku unashtukia mguu umetelezea shimoni kama ndege mjanja anavyonaswa kwenye tundu bovu. Zitto inawezekana matukio haya yanaweza kumkomaza aonekana kama mtu mzima mwenye kujituma katika mambo makubwa ya kichama kama wenzake. Kwani alionekana kuegemea hoja ya kuikosoa serikali kwa kuibua madhifu kwenye mashirika ya umma, lakini wenzake wamemshtukia.
Alimwambia Anna Makinda hamwezi kwani yeye atatumia ujanja wa chuoni, lakini mwezake amepata darasa kwa Ze-komedi na amefanikiwa kumpiga ngwara Zitto, chezea Makinda weye!
Nimeelewa sasa kama unavyoainisha Chadema ya mhitaji Zitto ndio maana matatizo ya masalia yeye pekee hakuguswa na fagio, lakini sasa Zuberi Mwenye sasa anaonyesha dalili ya kuhitaji chama baada ya kiwingu kilichomhifadhi kuenguliwa kiaina kwa mtindo wa mchezo wa sarakasi za siasa.