Kufunguliwa!!! - Kwanini wanavijiji wanaikimbia CCM kwa kasi kubwa kuliko watu wa mijini?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,997
Jibu: Kwa sababu watu wa vijijini wamefunguliwa na sasa wametambua kuwa hawana matumaini tena na CCM kwani haijalishi kama wako CCM au nje ya CCM maisha yao yako vile vile. Watu wa mijini - wasomi, wenye fedha na wenye raslimali zaidi za maisha BADO WENGI wana matumaini na CCM!

ELABORATE a.k.a EXPOUND!!
 
Deals zote kubwa ziko mijini na hasa jiji la Dar es Salaam, hivyo unaweza kuona watu wanaofaidika na uwepo wa CCM ni wa mijini. Vijijini ni wahanga mwanzo mwisho! Uliona nchi gani inayouza matreka ya kilimo mijini?

Mfano, Power Tillers- despite the fact that sio zana sahihi kwa kilimo cha watu wengi zinauzwa Dar es Salaam! Kuna wakulima gani Dar? Vivyo hivyo, bank iliyopewa hela za kuinua kilimo (TIB) iko Dar es Salaam, wakulima Mpanda au Karatu watapaje mikopo?

Sasa hivi kama watu wamegundua CCM wanakutana kwenye matawi yao kila Jumapili (karibu siku nzima)! Pengine wanaona kitumbua kinanyemelewa na mchanga sasa wanatafuta mbinu mbadala!
 
Kwa miongo kadhaa CCM imewadhalilisha na kuwadanganya watu wa vijijini!!

Hata pro- CCM mmoja hapa JF ana signature inayosema 'wasiosoma ni chakula cha waliosoma'

Udhalilrishaji huu uliendelea hadi katika mgawanyo wa rasilimali na huduma za muhimu za kijamii ambazo hazipelekwi kamwe vijijini!! Na hata zikipelekwa hupelekwa kwa uchache sana!

Tukizingatia mtizamo wa JK katika maendeleo ambapo yeye huamini kuwa Magorofa na foleni za magari katika miji ya Dar, Mwanza n.k ndio kipimo cha maendeleo, vijijini ambapo ndio kuna kapu la taifa la kulisha watu wote waishi mijini pamesahaulika na kudanganywa na kauli mbiu za MKUKUTA, KILIMO KWANZA n. k, huku wajanja kama kina Kigwangala na kampuni zao za Pamba wakipanga mbinu za kwenda kuwanyang'anya wakulima hata kile kidogo wanachopata..

Na jana tumeona wamefanya kikao pale Mwanza na kukubaliana kuwalazimisha wakulima wa pamba kuingia katika kilimo cha 'mkataba' sijui faida wala hasara za hii ila nahisi kuna mtego unatengenezwa..

Wananchi wa vijijini sasa wameamka, teknolojia imewafikia leo ukifika huko wana simu wanapashana habari, wana luninga wanatizama habari, bunge na maigizo ya Vichekesho, asubuhi wanaangalia chambuzi za magazeti na kusikiliza katika radio nini kinajili..

Unategemea nini hapo Mzee wakati M4C, haina huruma na imeshika kasi..???
 
...wanalima wao kwa taabu wanaofaidika ni wa mjini.
Hao ccm wanaonekana wakati wa kampeni tu vijijini.
Wamegundua wanaongopewa na kutumiwa tu.
Wameona mwamko wa maeneo mengine na kuona kile ambacho kilikuwa hakiwezekani (kwa sababu ya vitisho) kumbe yawezekana.
Walimpenda Nyerere, sasa wamegundua hayupo.
Vijana nao wameongezeka sana.
 
Mjini walioko ccm ni wale wafanya biashara na wafadhili wa ccm,na marafiki na familia za viongozi waliopo ktk uongozi,na hasa Dar,ila ukitoka nje ya dar miji mingi ni upinzani.na vijiji vinayo jua nini maana ya upinzani ni vile vilivyo elimika na sii vijiji vilivyo lala kama kusini.kwa hiyo kama tutafanikiwa kuelimisha vijijini na hasa kusini tutafanikiwa. kwa hiyo mjini kuwa upinzani wale ni kwa maslai yao binafsi,upinzani ukichukua madaraka wataanza kujipendekeza kwaajili ya kulinda na kutetea mali zao.
 
Jibu: Kwa sababu watu wa vijijini wamefunguliwa na sasa wametambua kuwa hawana matumaini tena na CCM kwani haijalishi kama wako CCM au nje ya CCM maisha yao yako vile vile. Watu wa mijini - wasomi, wenye fedha na wenye raslimali zaidi za maisha BADO WENGI wana matumaini na CCM!

ELABORATE a.k.a EXPOUND!!
MMM

Iko wazi, wanaofaidika na mfumo mbovu tulionao ni wafanyakazi wa serikali (kati na juu), wafanyabiashara (tena wengi wanakwepa kodi), wezi... na maswahiba

na hao wako vocal mno kwasababu lazima wajilinde

Kuna siku nilikutana na dada mmoja ndugu yangu, nikamuuliza "hivi wewe pamoja na busara zote ulizopewa unateteaje hali ya sasa"? akaniambia ikitengemaa atakula wapi???

and that was it........... she is a lawyer, educated, coming from a very religious family, but has chosen to enjoy other people's plasma
 
hapa nape anapoteza pesa, pumba tupu.

Naona huyu ribosome amehonga ili apewe kazi hii ya counter commentin hapa.. Au inawezekana akawa mtoto wa kigogo.. Maana badala ya kumsaidia Nape ndo anazidi kuwaharibia.. Tufani haizuiliki .. Subiri waone maafa ya tufani..
 
Jibu: Kwa sababu watu wa vijijini wamefunguliwa na sasa wametambua kuwa hawana matumaini tena na CCM kwani haijalishi kama wako CCM au nje ya CCM maisha yao yako vile vile. Watu wa mijini - wasomi, wenye fedha na wenye raslimali zaidi za maisha BADO WENGI wana matumaini na CCM!

ELABORATE a.k.a EXPOUND!!

Mwanakijiji hapa tatizo kwa hao wasomi,wenye fedha na rasimali zaidi ya maisha ,wamegawanyika katika sehemu mbili:Kwanza katika kipindi cha awamu tatu za mwisho za utawala wetu CCM tayari ilisha geuka ngao ya maovu yote hivyo ili wasomi na matajiri wafanye mambo yao sawasawa kupatata nafasi ya kusoma nje yawe ya kifisadi a au kujipatatia nafasi nzuri lazima uiunge mkono CCM utakake usitake kwenda kinyume na hapo utaundiwa mizengwe kibao hii ndio maana katika kipindi hiki wafanyabiaashara na mafisadi walikimbilia na kuiteka CCM kama kinga kwa maovu yao.Sehemu ya pili ya wasomi na matajiri ambao sio mafisadi wamekua na woga kutokana na vitisho vya moja kwa moja au kificho kutoka tawala na hivyo kukiunga mkono kwa shingo upande au kua nuetral katika mabo yao.Lakini sasa mambo yanabadilika nafikiri wakati huu ni wakati muafaka kubadilika na kushiriki katikamabadiliko.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Jibu: Kwa sababu watu wa vijijini wamefunguliwa na sasa wametambua kuwa hawana matumaini tena na CCM kwani haijalishi kama wako CCM au nje ya CCM maisha yao yako vile vile. Watu wa mijini - wasomi, wenye fedha na wenye raslimali zaidi za maisha BADO WENGI wana matumaini na CCM!

ELABORATE a.k.a EXPOUND!!

Wenye kazi na kipato kikubwa wanaogopa system ikibadilika watashindwa kuendeleza maisha yao haya ya kimjini mjini-tapeli tapeli kwani kwa uhakika tukigawana keki ya taifa kutokana na uzalisha mdogo sote tutatakiwa tufunge mikanda kinyume na ilivyo sasa ambapo wanaofunga mikanda ni wale wafanya kazi wa kada ya chini na rural majority. Serikali ya CCM nayo inajua hili kuwa wale elites hawabanwi sana ili wasije wakaigeuka serikali ambayo wengi wa viongozi wake wakuu wanaishi maisha ya kiparadiso kutokana na ufisadi....

Huu uamsho tuwashukuru wanascience wa mawasiliano waliowezesha rural community kupitia simu kupata information kwa haraka na kwa transaction ndogo sana....Kama watu hawatakubali kuweka mfumo wa kila mtu ale kwa jasho lake basi wanaoishi kitapeli ndiyo watakaosababisha taifa liingie katika sintofahamu very soon...

Mimi nikiwa na kura yangu ya VETO nasema hivi hakuna fisadi atakayekatiza kwenda Jumba letu takatifu tena nimesimama na miguu yangu yote miwili na mikono yangu yote ikishikilia rungu la kuangusha wote wenye harufu ya ufisadi....Ni garika na Tanzania njema lazima izaliwe mtu apende ama asipende! kazi imekwisha bado matukio tu!
 
Kwa nchi nyingine huwa mabadiliko yanaanzia mjini na hasa mji mkuu,ila kwa Tz sioni dalili.Yataanzia miji midogo na keenea vijijini.
 
nchi yoyote duniani utakua ule mji mkuu wa miji mikubwa serikali ina influence sana kwa sababu wenye hela wote wako mijini na ndio wanao lobby serikali, huko vijijini wananchi hawana say kabisa na wakati wa uchaguzi watu wanaenda kutoa rushwa unakuta wanavijiji wanapewa shs 10000 kila mmoja wanakupa kura yao...huko mijini unazani unaweza kuwarubuni watu na shs 10000??
 
Back
Top Bottom