Kufunguliwa!!! - Kwanini wanavijiji wanaikimbia CCM kwa kasi kubwa kuliko watu wa mijini?

nchi yoyote duniani utakuta ule mji mkuu au miji mikubwa serikali ina influence sana kwa sababu wenye hela wote wako mijini na ndio wanao lobby serikali, huko vijijini wananchi hawana say kabisa na wakati wa uchaguzi watu wanaenda kutoa rushwa unakuta wanavijiji wanapewa shs 10000 kila mmoja wanakupa kura yao...huko mijini unazani unaweza kuwarubuni watu na shs 10000??
 
Kusema ukweli ukiishi kama raia mwema Tanzania ni shida sana ku-excel...Biashara zote zimeungamanishwa na either serikali, chama, ama viongozi nje ya hapo unaambulia kulipa kodi kibao na vihunzi vingi hata kama una mawazo mazuri tena yakuisaidia nchi. kwakua sikuwa na family kubwa wala responsibility kwa extended family niliamua kufanya action research kupitia maisha yangu mwenyewe....I struggled kwakweli na hata hivyo kuna sehemu nyingine bila kujua association yangu na jina fulani kubwa ilirahisisha baadhi ya mambo. Nimefikia conclusion kuwa kwakweli kuwa mzalendo Tanzania ina hitaji neema ya Mungu mwenyewe!

Hatimaye nimeamua sasa katika hatua zangu za mwisho kuelekea utuuzima kutoka ujanani kuwa mwanaharakati na kutumia uzoefu, ujuzi wangu na nguvu zangu zote za kimwili na kiroho kusaidia rural community. Nauhakika kwa nguvu ya roho mtakatifu hata kama si mimi nitakaye ona haya mafanikio wale wa generation ya nyuma yangu watakuwa na chakujivunia kwa nchi yao! Nimeanza na kuangusha mafisadi katika ulimwengu wa kiroho na kuanzia mwaka jana nimeanza na capacity building kabla ya kuingia katika action zenyewe za kiuzalishaji...Over to you Hollyghost yeye aliyeanzisha haya atayakamilisha!
 
Udhaifu wa kufikiri huo.

Ngome ya CCM iko vijijini na si mjini. Usitake kuwalambisha watu tope.

Umeelewa kweli mleta mada anachokiongelea au unakurupuka tu kujibu? Yes ngome yenu ilikuwa vijijini,unaongelea vipi wana CCM wa kijiji cha Lugata (Sengerema Vijijini) kukihama Chama chenu na kujiunga na CDM,au ndio msemo wenu wa "ni upepo tu utatulia". 2015 utamuelewa Mleta mada anamaanisha nini kwa sasa wewe endelea kuota!
 
Nadhani miniji watu wanabase kwenye specialization, wanawaachia ma politician wapractice politics, lakini kwa suala la kupiga kura ambalo halina specialization wengi wanavote kwa upinzani, ila hawana kadi, on the contrary vijijini kila mtu ni politician kwa huku kwetu TZ, sasa wanasiasa wa vijijini wameamka!
 
I have been so impressed and refreshed that CDM has penetrated the very stronghold of CCM country-over. I keenly desired to see this pace is kept intact till CDM assumes total power in the near future and then effect the sought-after changes and leadership.

Caution
As it stands the only enemy I fear is CDM themselves. In moments like these tare seeds of isms such as divisiveness and arrogance could crept in, so I pray we retain our vigillance and prevent it from happening. CCM might be working hard on it for it's probably their main hope right now.
 
Watu wa mijini tayari walishaikimbia ccm siku nyingi (kimya kmya) walikuwa wamebaki ndugu zetu wa vijijini kwani kwa muda mrefu walikuwa wakitishwa kwa picha za Rambo, ila kadli muda ulivyozidi kwenda na kukua kwa tecknologia ya mawasiliano (ufahamu), wanavijiji wakaanza kungundua ukweli na kukimbia chama cha ccm.
 
Jibu: Kwa sababu watu wa vijijini wamefunguliwa na sasa wametambua kuwa hawana matumaini tena na CCM kwani haijalishi kama wako CCM au nje ya CCM maisha yao yako vile vile. Watu wa mijini - wasomi, wenye fedha na wenye raslimali zaidi za maisha BADO WENGI wana matumaini na CCM!ELABORATE a.k.a EXPOUND!!
Mkubwa, nakuhakikishia hata mjini watu wameichoka CCM. Tofauti ni kuwa wa mjini wengi wanaishi kwa mgongo wa CCM. Unakumbuka maneno ya Sumaye 'Ukitaka ufanikiwe katika biashara zako jiunge na CCM'.

Pili, huko vijijini mawasiliano yameongezeka, watu wanasafiri, wanasikiliza redio na wana vijisimu achilia mbali vijana wao wanaorudi kuwatembelea. Ule uzushi kuwa bila CCM ni vita tu umebainika kuwa uongo.

Tatu, wanavijiji sasa wanaelewa kuwa kama kuna mtu anaweza kupata mshahara wa milioni 5 halafu akaweza kununua hekalu la bilioni moja kuna jambo hapo. Wanajiuliza inakuwaje nyumba ya mtu mmoja inathamani sawa na mali za kijiji chote ukiondoa ardhi tu!

Nne, wamechoka kusikia hadithi za tutawaletea maendeleo. Wamesikia hadithi hizo wengine wakiwa wanacheza cha ndimu na nage sasa ni akina babu na bibi. Wanachoshangaa aliyewahi kuwaambia anawaletea maendeleo amestaafu sasa mtoto wake naye amekuja kuendeleza ngano na simulizi zile zile.

Kinachowasukuma ni kuwa, wakati wa mbadala umefika. Kufanya jambo moja kila siku na kwa namna ile ile bila kuwa na matokeo tofauti ni ujinga. Wameamka na wanatimua! Sijui kama wanajua wanakwenda wapi lakini nina uhakika kuwa wanatimka kwasababu sisi watazamaji tunajifuta vumbi la mbio zao. Wanakwenda! wanatimka
 
Nadhani miniji watu wanabase kwenye specialization, wanawaachia ma politician wapractice politics, lakini kwa suala la kupiga kura ambalo halina specialization wengi wanavote kwa upinzani, ila hawana kadi, on the contrary vijijini kila mtu ni politician kwa huku kwetu TZ, sasa wanasiasa wa vijijini wameamka!

thanks... umebeba essence ya jina hili la "Mimi Mwanakijiji"..... tumedharauliwa sana oo hatujui, tufundishwe uraia, sijui hatuelewi sana kinachoendelea kumbwe 'we are the force for change!"
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kukosa matumaini ndo jibu la msingi hapo. Maisha yao yamekuwa magumu na hawana mahali pa kukimbilia. Kwa hiyo wanaona hata huyo ccm waliyekuwa wanamtumainia hana lolote la maana la kuwasaidia, kwa hiyo ni afadhali kuachana naye tu.
 
I have been so impressed and refreshed that CDM has penetrated the very stronghold of CCM country-over. I keenly desired to see this pace is kept intact till CDM assumes total power in the near future and then effect the sought-after changes and leadership.

Caution
As it stands the only enemy I fear is CDM themselves. In moments like these tare seeds of isms such as divisiveness and arrogance could crept in, so I pray we retain our vigillance and prevent it from happening. CCM might be working hard on it for it's probably their main hope right now.

Dont be so skeptical tumeanza na Mungu yeye ndiye atakamilisha kazi aliyoianza....CDM kinatumika kama chombo tu cha Mungu kuifanya kazi yake mpaka watakapoweza kumtoa Mungu katika kiti chake cha enzi ndipo watakapoweza kuzima hii move!
 
Udhaifu wa kufikiri huo.

Ngome ya CCM iko vijijini na si mjini. Usitake kuwalambisha watu tope.
Hapo zamani ilikuwa hivyo! lakini sasa mambo yamebadirika sana. Shule zetu tukufu za sekondari za kata kwa muda mfupi tu zimewazalisha wanavijiji wanao ichukia CCM kama nyoka mwenye sumu kali. Pole kwa kutoujua ukweli huu. Wenzio tupo huku kijijini tunasumbuka nao. Sakata la korosho Tandahimba ni mfano mzuri sana wa wananchi vijijini kuichukia CCM!
 
CCM ilitawala kwa vitisho wakati wa uchaguzi vijijini hutishiwa kuwa wakichagua upinzani watanyimwa huduma muhimu na kwa kuwa elimu ya demokrasia ilikuwa finyu sana vijijini kuliko mjini, watu wengi waliichagua CCM kuogopa vitisho. Lakini kwa sasa watu wameelimika, TV kila mahali, maendeleo ya simu yamesababisha uelewa mkubwa kwa watu wa vijijini na hivyo kuwa na mwammko mkubwa wa kutaka mabadiliko. CCM wamesahau usemi usemao,"You can fool people for some time but not all the time"
 
Back
Top Bottom