Kufunguliwa!!! - Kwanini wanavijiji wanaikimbia CCM kwa kasi kubwa kuliko watu wa mijini?

Pengine wao ndio wataonyesha watu wa mjini njia ya wapi tunapaswa kwenda. Huwa hawaamui kwa papara ila wakiamua, sijui kama kutakuwa na kurudi nyuma. Naangalia tu kwa bumbuwazi!!!
 
Jibu: Kwa sababu watu wa vijijini wamefunguliwa na sasa wametambua kuwa hawana matumaini tena na CCM kwani haijalishi kama wako CCM au nje ya CCM maisha yao yako vile vile. Watu wa mijini - wasomi, wenye fedha na wenye raslimali zaidi za maisha BADO WENGI wana matumaini na CCM!

ELABORATE a.k.a EXPOUND!!
uko wrong kuhusu watu wa mjini
watu wa mjini hawaitaji kusema wanaikimbia ccm ila matendo yao ndio utajua.

Mfano jimbo la kawe limeanzia osterbay, mikocheni kawe mbezi tegeta na kuendelea. Hawa watu wanakula keki ya taifa vilivyo lakini wamechagua chadema.
Hawa watu hawaji kwenye mikutano ya campaign lakini wanafuatilia siasa kwa ukaribu sana. Watu wa mjini wameshakimbia lakini hawasemi
 
Tatizo hao wananchi wa vijijini wengi hawajasoma, hivyo chadema wanatumia ujinga wa wananchi kuwapotosha kuhusu serikali iliyopo madarakani, ndiyo maana wengi wa washabiki wa Chadema ni weupe kichwani.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
Kuna madiwani wangapi wa CDM Kawe?
 
Tatizo hao wananchi wa vijijini wengi hawajasoma, hivyo chadema wanatumia ujinga wa wananchi kuwapotosha kuhusu serikali iliyopo madarakani, ndiyo maana wengi wa washabiki wa Chadema ni weupe kichwani.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".

Na CCM ilipojikita huko vijijini nakupatiwa ushindi kutoka vijijini ni kwa sababu ya huo ujinga wao?
 
Na CCM ilipojikita huko vijijini nakupatiwa ushindi kutoka vijijini ni kwa sababu ya huo ujinga wao?

Wanachagua CCM kwa kuwa ni chama pekee hapa Tanzania chenye lengo la dhati kumkomboa mwananchi toka janga la umaskini.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
Watu wanaonufaika na uwepo wa CCM sio watu wa vijijini.
In fact hawajawahi kunufaika.Wanaonufaika na uwepo wa CCM ni watu wa mijini.
Na hii sio kwa Tanzania tuu. Inatokea kwenye nchi kibao.
Kwa mfano Syria, Damascus kimyaaaaa.
 
Wanachagua CCM kwa kuwa ni chama pekee hapa Tanzania chenye lengo la dhati kumkomboa mwananchi toka janga la umaskini.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
kwa miaka mingapi watakuwa wamemkomboa huyu mwananchi maskini?
 
Wasomi wengi mijini hawana hamu tena na CCM toka moyoni lakini ama kwa ajili ya kuogopa adhabu ya mfumo wanaoufaidi kwa namna moja au nyingine wanaamua kukaa kimya lakini wanaongea sana kwenye mitandao kama hapa JF.

Na pia wanawaunga mkono Wapinzani kwa kuwapa taarifa nyeti. Mwanakijiji elewa kuwa CHADEMA sasa inajengwa na WanaCCM bila kelele yaani kimya kimya!!!
 
Udhaifu wa kufikiri huo.

Ngome ya CCM iko vijijini na si mjini. Usitake kuwalambisha watu tope.

vijiji vya bububu na mwanakwerekwe na paje nako tunakuja kuwashika mpaka mikindani waliko majuha nako tunakuja.
 
Tatizo hao wananchi wa vijijini wengi hawajasoma, hivyo chadema wanatumia ujinga wa wananchi kuwapotosha kuhusu serikali iliyopo madarakani, ndiyo maana wengi wa washabiki wa Chadema ni weupe kichwani.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".

Nape inabidi aangalie tena safu yake ya mawakala hapa JF kwa sababu ni aibu kuandika ***** namna hii kwa GTs.
 
Nape inabidi aangalie tena safu yake ya mawakala hapa JF kwa sababu ni aibu kuandika ***** namna hii kwa GTs.

Ona sasa ulivyo juha, kwa fikira zako finyu unadhani kila aliye upande wa Ccm ametumwa na Nape? wengine tumetumwa na akili zetu wenyewe, unasikia wewe kilaza.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
On the red: that was then! Sasa hivi mambo yamegeuka!

Na aliyoyageuza ni nani? Mageuzi ya dhati ya kuweza kufikisha ujumbe huko vijijini hamuoni yameanzia wapi.

Vipofu, viziwi na mabubu.
 
'Kwanini wanavijiji wanaikimbia CCM kwa kasi kubwa kuliko watu wa mijini?'

Ujio wa media kama TV, redio, magazeti na mitandao ya simu imesaidia sana kuongeza uelewa wa watu na hivyo kuondoa woga uliokuwepo vijijini, wanaona na kusikia kumbe hata rais anaweza kupingwa, kumbe hata Mkapa anaweza kujibiwa kitu ambacho kilikuwa nadra sana kutokea. Hali hiyo ndiyo imewajenga watu wa vijijini kuwa na ujasiri na kuona kumbe wanaweza kujiunga na vyama tofauti na CCM na wasifanywe kitu.

Sababu nyingine inaweza kuwa ni kukinai kwa CCM wanataka kujaribu kitu kipya, watu wamekinai hata sale za kijani ukivaa unaonekana kama wa zamani wakati mwingine unazomewa. Hiyo ni hulka ya binadamu unapoishi na kitu fulani kwa muda mrefu huwa kuna matamanio ya kujaribu kipya kinyemi.

Watu wa vijijini wengi wao wamejiajiri tofauti na wa mijini, wanaona hata wakihama chama hawana cha kupoteza. Hakuna mtu atakayewafukuza kazi tofauti na wa mijini walioajiriwa kwa hiyo hawaoni hasara wala faida yeyote watakapohama CCM.

Shule za kata nazo zina mchango kwenye mapinduzi haya. Karibu kila kata ina sekondari na inazalisha vijana wengi, wengi wao wanabaki hapo hapo kijijini. Hawa ni uzao wa miaka ya 90 uzao wa mageuzi, wanajua matatizo wanayopata yamesababishwa na serikali ya CCM. Hawa ndio wanakuwa kama wasemaji wa center towns huko vijijini, kwa vile wana angalau elimu ya sekondari wanauwezo wa ushawishi kwa wenzao na wazazi wao kuhamia vyama vya upinzani.
 
'

Hii ya mwisho nimeipenda; kwani hata kama wanafeli lakini mbegu za kufikiria na udadisi zinakuwa zimeshapandikizwa!
 
Back
Top Bottom