Kufungiwa MwanaHalisi: Serikali yapewa Siku saba kulifungulia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufungiwa MwanaHalisi: Serikali yapewa Siku saba kulifungulia

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by only83, Aug 21, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  KWA mara nyingine tena, tumewaiteni hapa kuwaomba mtufikishie ujumbe wetu huu kwa watawala. Ujumbe wenyewe unahusu kufungiwa kwa gazeti la kila wiki la MwanaHALISI na kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda aliyeitoa bungeni, Alhamisi tarehe 16 Agosti 2012. Kama mnakumbuka vema, wakati akijibu swali bungeni siku hiyo, Waziri Mkuu Pinda alisema, "Serikali imechukua wajibu wake kufungia gazeti hilo, na kwamba kama wahusika hawakuridhika ni wajibu wao kwenda kukata rufaa kwa mamlaka za juu."

  Awali ya yote, tuseme wazi, kuwa hatukuridhika na majibu ya waziri mkuu kuhusu kufungiwa kwa MwanaHALISI. Majibu ya Waziri mkuu Pinda yamelenga kughairisha tatizo, siyo kutatua. Kwanza, Waziri Mkuu anatetea uamuzi huo uliofanywa na sheria katili ya magazeti. Sheria inayonyang'anya uhuru wa kufikiri, uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa kuwasiliana. Pili, Mheshimiwa Pinda anatumia sheria hiyo kutaka kuliangamiza gazeti hili ambalo limesifiwa kwenye ripoti mbalimbali za ndani na nje ya nchi ikiwamo ile iliyotolewa majuzi na Baraza la Habari Tanzania (MCT) inayochambua Mwenendo wa vyombo vya Habari nchini kwa mwaka 2011 inayosema katika ukurasa wa tisa:

  "Pamoja na kusakamwa na serikali, MwanaHALISI limesimamia uandishi wake wa kuikosoa serikali."

  Serikali limeituhumu gazeti hili kwa kuchapisha habari ambazo inasema "zinakiuka" vifungu 32(1) (a), (c) – (d); 32(1)(c) na 36(1) vya Sheria ya Magazeti Na. 3 ya 1976. Habari hiyo inahusu kutekwa, kuteswa kinyama na hatimaye kutupwa katika msitu wa Mabwepande kwa kiongozi wa madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka. Hii ndiyo habari ambayo serikali inaita "uchochezi." Yaani badala ya serikali inayojigamba ina mkono mrefu wa kumfikia yeyote kuutumia mkono huo kutafuta watuhumiwa waliotajwa na gazeti kuwa walifanikisha kutekwa kwa Dk. Ulimboka, imeamua kutumia mabavu kufungia MwanaHALISI huku wakiacha maisha ya Dk. Ulimboka na wanaharakati wengine njia panda.

  Serikali imechukua hatua hiyo, huku wakijua kuwa Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 kama ilivyorekebishwa na Sheria ya Mabadiliko ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2005), ilipanua haki ya kutoa, kutafuta, kupokea, na kusambaza habari. Mabadiliko hayo yaliondoa kivizo cha "kwa mujibu wa sheria" Kila mtu- anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake; anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi; anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake.

  Aidha, mabadiliko hayo yanatoa haki kwa kila raia ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio muhimu mbalimbali kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii. Hivyo basi haki na uhuru wa kujieleza, kupokea na kutoa habari haina vipingamizi ambavyo serikali inadai kuwamo katika Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976.

  Vilevile, kuwekwa kwa Vipengele vya Haki za Msingi na Wajibu wa Mwanadamu (Bill of Rights) katika Katiba ya nchi yetu kulibadilisha sheria zote ambazo zinakiuka haki za binadamu. Vifungu vyote ulivyovitaja hapo juu viliguswa moja kwa moja na Vipengele vya Haki za Msingi na Wajibu wa Mwanadamu. Ibara ya 14 ya Katiba inalinda haki ya kuishi na inaitaka jamii kutoa hifadhi ya maisha kwa kila mtu. Kana kwamba hiyo haitoshi, Ibara ya 26(1) na (2) zinataka kila mtu na serikali kutii Katiba ya nchi na vilevile kuchukua hatua za kuheshimiwa haki na sheria za nchi.

  Waziri mkuu anayajua haya vizuri. Anafahamu kuwa sheria iliyotumiwa kufungia gazeti, ni sheria katili na imepitwa na wakati. Kuitumia sheria hii kunaendeleza dhana ya kuwa serikali hii inatumia udhaifu wa Katiba na baadhi ya sheria kukandamiza Haki za Binadamu na Uhuru wa Habari! Mambo haya hayakubaliki.

  Kutokana na hali hiyo, sisi watetezi wa haki za binadamu na asasi nyingine za kiraia:
  1. Tunarejea wito wetu wa kuitaka serikali kulifungulia mara moja na bila masharti, gazeti hili ambalo limekuwa kipenzi cha wananchi. Tunaitaka serikali ndani ya siku saba (7) kutekeleza hilo kwa kuangalia maslahi mapana ya jamii badala ya kuangalia maslahi ya baadhi ya viongozi wenye maslahi fulani katika kutimiza malengo yao binafsi.


  Serikali itekeleze takwa hili haraka iwezekanavyo, na kwamba asasi za kijamii hazikubaliani na kauli ya Waziri Mkuu ya kutaka wahusika waende kwenye vyombo vya juu kwa sababu tatu zifuatazo:

  Kwanza, sheria ya magazeti hairuhusu ukataji wa rufaa kwa waziri wa Habari ambaye ndiye aliyetuhuhumu na kuhukuhumu gazeti bila kutoa nafasi kwa wahusika kusikilizwa. Pili, Waziri Mkuu Pinda pamoja na sheria hiyo kutomtaja, hakueleza kuwa yuko tayari kupokea malalamiko ya MwanaHALISI. Hivyo kutoelekeza kwake tunakuchukulia kama njia ya kukwepa wajibu wake.

  Tatu, hatukubaliani na kauli ya Waziri Mkuu na wengine wanaotika MwanaHALISI waende mahakamani kutafuta haki yao kwa kuwa serikali yenyewe haikutumia njia ya mahakama kufungia gazeti. Serikali inataka kuitumia mahakama ili kuchelewesha MwanaHALISI kupata haki yake. Nyote mnajua jinsi mahakama zetu zinavyokabiliwa na gonjwa kubwa la ucheleweshaji wa kesi.

  2. Serikali, baadala ya kushughulika na watetezi wa haki na wanahabari wanaofichua uovu, ishughulike na wahalifu waliomteka, kumtesa na hatimaye kumtelekeza Dr Ulimboka. Ushahidi uliobainishwa na gazeti hili haukuacha shaka yeyote juu ya waliohusika na sakata hili, na kama serikali au watendaji wake waliotajwa (na waliohusishwa) wana mashaka wangetumia ushahidi na taarifa zile kutafuta haki zao: kwanini wasiende mahakamani au wajitokeze na ushahidi wa kukanusha yaliyobainishwa?

  3. Serikali iachane kabisa na ukandamizaji huu wa haki na uhuru wa habari. Matendo aliyofanyiwa Ulimboka, habari zilizobainishwa na MwanaHalisi juu ya sakata hili na kufungiwa kwa gazeti hili kunaonesha mtiririko wa matukio ya serikali kuminya uhuru na haki.


  Ikumbukwe pia kuwa, Kesi Na. 34/2009 iliyofunguliwa tangu 2008 kupinga sheria ya magazeti ya mwaka 1976 iliyotumika kuwafungia MwanaHALISI haijasikilizwa mpaka sasa. Hii inaenda sambamba na serikali kufumbia macho mahitaji ya sheria ya uhuru wa habari na kudharau mapendekezo ya muswada wa habari tangu 2007 bila kupeleka Bungeni.

  Kwa hoja hizo, sisi watetezi wa haki za binadamu, asasi za kijamii na wadau wa kuu wa habari nchini, tunaendelea kusisitiza kuwa serikali itimize wajibu wake kwa kulifungulia mara moja gazeti hili na kufanyia kazi yaliyobainishwa. Kama ikishindwa kufanya hivyo, tutaitisha maandamano ya kupinga hatua ya serikali kufungia gazeti hili, kuminya uhuru wa habari, haki za binadamu na uteswaji wa wanaharakati na watetezi wa haki na kwamba tukifika hapo tunawaomba waandishi wa habari mtuunge mkono kwa yafuatayo.
  i. Msichapishe habari yoyote inayomhusu Waziri wa Habari, Naibu Waziri, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, na pia Mkurugenzi wa Maelezo. Tunawasihi wahariri wasiwatume waandishi katika Ukumbi wa Habari Maelezo kwa ajili ya kuchukua habari kama ilivyo kawaida na badala yake Watanzania wote wahakikishiwe kupata habari kwa njia nyingine mbadala.

  ii. Tunawasihi wadau wote wanaoweza kutuunga mkono mara tutakapohitaji msaada wao ikiwa ni pamoja na kushiriki kwenye maandamano na kupata mawakili ambao watasaidia katika uendeshaji wa shauri letu mahakamani.

  iii. Tunawasihi wanaharakati wote wasichoke ma wala wasirudi nyuma katika azma hii ya kutetea haki, uhuru na ulinza kwa haki na watetezi wake.
   
 2. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #2
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Nimeikuta hii mahala

  Kamati ndogo iliyoundwa na taasisi nne za kiraia nchini ambayo inaratibu kupigania haki ya kufunguliwa kwa gazeti la MwanaHalisi, leo imeipa serikali siku saba kuliruhusu gazeti hilo kuendelea kuchapishwa.

  Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa kamati hiyo Marcossy Albanie, amesema hawana sababu yakwenda mahakamani juu ya jambo hilo kwasababu hata serikali haikutumia njia hiyo ya mahakamani kwani ilikuwepo badala yake wametumia sheria kandamizi ya vyombo vya habari inayopigiwa kelele na wadau wa habari.

  Kamati hiyo inayoungwa mkono na taasisi tano za kiraia baadhi ya taasisi hizo ni MISA TANZANIA, TANZANIA HUMANRIGHTS DEFENDERS COALITIONS NA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU (LHRC) imeitaka serikalikutekeleza madai yafuatayo:-


  1. Kuitaka serikali kulifungulia gazeti la Mwanahalisi maramoja.
  2. Serikali badala ya kushughulikia Watetezi wa haki na wanahabari wanaofichua uovu ishughulike na wahalifu waluiomteka Dkt. Ulimboka.
  3. Serikali iache kabisa na ukandamizaji huu wa haki na uhuru wa habari.

  WAANDISHI WA HABARI WAOMBWA YAFUATAYO SERIKALI ISIPOTEKELEZA HAYO:


  1. Kutochapisha habari yoyote itakayo wahusu Waziri wa Habari wa Wizara hiyo na Naibu wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo.
  2. Kusimama kidete kuunga mkono harakati hizo hadi zinapata ufumbuzi wake.

  Ikumbukwe kesi Na.34/2009 iliyofunguliwa tangu 2008 kupinga sheria ya magazeti ya 1976 iliyotumika kufungia MwanaHalisi haijasikilizwa mpaka sasa.


  Source: wavuti - wavuti
   
 3. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #3
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Cha kujiuliza, serikali itasalimu amri ama hawa jamaa wanajisumbua?
   
 4. k

  kagame Senior Member

  #4
  Aug 21, 2012
  Joined: Dec 6, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sakata hili lanikumbusha enzi za waziri Ramadhani Omari Mapuri na msimamo wa waandishi wa habari kugoma kuandika habari zinazomhusu.
  Kuna vyombo vya habari vitakavyoendelea kuandika habari za viongozi hao hata kama serikali haitotekeleza agizo la kulifungulia MwanaHALISI, sanction ipi itawekwa kwa vyombo kama hivyo?
   
 5. t

  thatha JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Njaa inawasumbua hawa.
   
 6. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Tunaomba serikali yetu hasa wahusika wa suala hili watafakari kwa makini na wachukue hatua za kulifungulia gazeti tajwa kwa ajili ya mustakabali wa amani ya nchi yetu. Tuko katika kipindi cha mpito, hivyo issue kama hii yaweza kuleta mkanganyiko katika jamii.
   
 7. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #7
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  duh aisee Mapuri hivi bado yuko ubalozi China? nadhani media zetu hazina umoja, vinginevyo hii ingesaidia kuwashinikiza haki itendeke
   
 8. KXY

  KXY JF-Expert Member

  #8
  Aug 21, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Sijaelewa hapa

  Hivyo tu?

  Vp habari zinazowahusu mabosi wa hao namba 1 hapo juu?
   
 9. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #9
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Nani huyo mwenye njaa? kwani hapa wanatafuta pesa mkuu? Au u missed the point?
   
 10. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #10
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  You must have a starting point. Ikianza na hao na hatua zisipochukuliwa kutenda haki, basi wanaweza kuongeza wengine kukazia 'hukumu'. tatizo nina shaka na umoja wa media zetu
   
 11. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  cha kujiuliza zaidi,je wanaharakati na wanahabari watasalimu amri na kurudi nyuma?
   
 12. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #12
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mchumia tumbo wewe, we ndo unasumbuliwa na njaa,unaongea u. K tu lamaya mkubwa umelaaniwa we na kizazi chako...agrrrrrrrrrr. Natamani nikuone live chunga sana pimbi.
   
 13. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #13
  Aug 21, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mimi nafikiri wasusie habari zote za serikali tuone kama vyombo vyake vilivyopoteza mvuto kwa jamii km vitafikisha ujumbe kwa wananchi,pia hawa wanaharakati waangalie namna ya kulifikisha suala hili kwenye vyombo vya kimataifa kwa sababu hili suala linahusu namna serikali inavyokiuka haki za binaadamu kwa kutumia dola kunyanyasa raia wake
   
 14. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #14
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  t2015ccm kafumu keshafumuliwa toa maoni yako.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. chelsea fc

  chelsea fc JF-Expert Member

  #15
  Aug 21, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 835
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Daifu,liwalo na liwe ? 2015!vua gamba vaa gwanda,m4c,haponi m2 hapa
   
 16. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #16
  Aug 21, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145

  Umesikia kilichotokea Igunga leo?
   
 17. K

  KIBE JF-Expert Member

  #17
  Aug 21, 2012
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  serikali ndo mdau mkubwa wa habari sa wakisusia watapata wapi habari..hayo magazeti si watakufa njaa
   
 18. B

  Baba Tunde JF-Expert Member

  #18
  Aug 21, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 359
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mojawapo ya njia pia ni kupeleka swala lenyewe kwenye Taasisi ya haki za binadamu (UN) kwani kufungiwa kwa Mwanahalisi kulihusisha kupigwa na kuteswa kwa binadamu (Dr. Ulimboka), Kupeleka swala lenyewe kwenye Jumuiya nyingine za Kimataifa, n.k. Hii itasaidia kutoa pressure kwa sheria Kandamizi. Ikumbukwe pia kuwa Serikali yetu ni ombaomba, kwa hiyo, kwa kupeleka kwenye taasisi hizi, itawafanya wabanwe wakati wa kupitisha bakuli.
   
 19. Antonov 225

  Antonov 225 JF-Expert Member

  #19
  Aug 21, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Maditekta ni watu walioumbwa ki maajbu sana. Katika vitu walivyonyimwa ni upeo wa kujifunza kwa makosa ya wengine. Wote wanakaa miaka mingi bila kijijua,wana aina zile zile za ukandamizaji na kifo chao ni kimoja pia kumbukumbu lao linakufa milele. (angalia idd amin, mengistu,gadafi n.k) hatua yao ya mwisho kwenye kifo chao ni kukandamiza uhuru wa habari na ndio hatua ccm iiyopo sasa, wanaona wanapendwa ili hali hawapendwi, wanaona watadumu milele ili hali wanakufa. Wananunua vyombo vya mahakama,wanatawala bunge , polisi n.k kwa nia ya kushindana na nguvu ya umma, polenimccm na supporters wake. Naomba bila kuchoka tuzidi kupambana na nduli ccm.
   
 20. M

  Mpwechekule JF-Expert Member

  #20
  Aug 21, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wamechelewa kutoa tamko hilo, pia siku zote moyo wangu haukufunguka vizuri juu ya waandishi kwani sijaona kama wamelichukulia kwa uzito unaositahili jambo hilo, nilitegemea vyombo vyote huru vya habari vingegoma kuandika habari zote za selikali, lakini natoa rai kwa vyombo vyote huru viache kuandika habari za chama tawala na selikali yake, MCT TAFADHALI onyesheni hili hamlipendi kwa kutangaza mgomo huo, mungu atasimamia watumishi wake,
   
Loading...