Kufungiwa kwa gazeti la mwanahalisi:

Kufungiwa kwa gazeti la mwanahalisi:

Daima Tutakukumbuka!

A1-MWANAHALISI-GAZETI+LA+MWANAHALISI-SAED+KUBENEA-TANZANIA+NEWSPAPERS-MAGAZETI+YA+TANZANIA-HABARI+ZA+TANZANIA-TANZANIA+NEWS-PRESS.JPG
 
Katika mambo yanayoniumiza sana katika nchi yetu hii ni kuendelea kufungiwa kwa MWANAHALISI. Kufungiwa inaweza isiwe tatizo, bali sababu za kulifungia. Baada ya siku 172 bado Serikali hii dhalimu haijatoa sababu haswa za kufungiwa gazeti hilo.

Wadau, Wanahabari na Jamii nzima tuungane kupigia kelele uonevu huu unaofanywa na Serikali inayojinasibu inaheshimu demokrasia, uhuru na haki za watu katika kutoa maoni na fikra zao. Tukiendelea kupiga kelele na kupaza sauti zetu, hawa watawala dhalimu watashtuka na watatahayari na bila shaka wataona aibu kwa mambo yao ya aibu wanayotufanyia Watanzania.

Nawasihi wadau wote wa kwenye Radio, Magazeti na TV (Dotto Bullendu wa Star TV ameanza hiyo kampeni kwenye kipindi chake cha Tuongee Asubuhi kila jumamosi) muanzishe Mada na vipindi mbalimbali kila siku kwa lengo la kuilazimisha Sirikali ilifungulie gazeti hili.
 
Mmeshafulia kaeni kimya watu tufanye mambo mengine .... tulikuwa tusinywe maji kila siku hikii mara kileee mara hikiii
Sheinz type...
Mtuache tupumueeeee
 
shure nimemis sana makala za ndimara na tangu gazeti linaanza sijawahi kukosa nakala hata moja .kwanin hiv jaman,dk nchimb think twice on this matter.tutainua saut na mungu atatusaidia
 
Miongoni mwa mambo ambayo yanamfanya mwananchi wa kawaida mwenye uelewa wa mambo kuwa na mashaka na serikali yake juu ya usalama wake ni hatua za kulifungua mwanahalisi. Binafsi mpaka sasa naamini ukimya wa serikali juu ya sakata la kutekwa na kuteswa kwa uliomboka ukiunganisha nukta na jinsi Mulindi anavyo omba Ulimboka aletwe ili amtambue, na jinsi mwanahalisi lilivyo andika mawasiliano ya ndani ya wale vigogo wa Ikulu! Hakika unaona giza nene lenye ukungu mzito.

Mzee Ndimara ameuliza vitu vya msingi sana kuamsha fikra mpya! Ona hapa "Watawala walishindwa, labda kwa kiwewe tu, kuelewa kuwa taarifa za ndani na za kina zingeonyesha muhusika mmoja na siyo serikali yote wala ikulu yote. Hawakuona kwamba taarifa za kina zingesafisha hata Usalama wa Taifa na Polisi – ambao ndio walikuwa wanatungwa kidole".

Je kwa maandiko hayo hapo juu ya Mzee Ndimara tuanze kuamini kuwa tumempangisha mtesaji pale magogoni?! Je, kuna watu walio tayari kutesa wengine ili kuuficha ukweli?!

Kama jibu sio, kwa nini walifungie Mwanahalisi sasa na hawataki kulifungulia? Kama lili kuwa linaandika uchochezi kama wanavyo sema. Je, ni kweli habari ya kutekwa na kuteswa ulimboka ilikuwa uongo na hivyo mwanahalisi lilituchochea kwa kuandika uwongo?! Kama ndio, ukweli ni upi sasa mbona hawatuelezi?!


Lakini swali la dogo tu,uko wapi umoja wa waandishi wa habari
kuongea juu ya kufungiwa mwanaHalisi?

Uko wapi mdomo wa jukwaa la wahariri, au wamefungwa plasta?
 
Umoja wa kitaifa katika kupigania mambo ya maendeleo umedorora sana.Watanzania wengi bado ni wajinga na hatujakomboka kifikra.Ni ngumu sana kuweza kukusanyika na kutetea jambo kama hilo.Kuna kamsemo maarufu kamtaani kanasema"TATIZO SHULE".Labda wanazuoni mliobobea kwenye sheria mjipange kwenda kuwatetea mahakamani kama inawezekana ila nguvu ya umma mmmh baadae sana.

Hakika wewe umetoa tafsiri haswaaa ya signature yangu.
Mitanzania ndivyo tulivyo
 
Mmeshafulia kaeni kimya watu tufanye mambo mengine .... tulikuwa tusinywe maji kila siku hikii mara kileee mara hikiii
Sheinz type...
Mtuache tupumueeeee

mmmh,nawe unaishi.
 
Hili gazeti lilisha wahi kufungiwa vipi tutumieni shinikizo kama lile la mwanzo nilazima watalifungulia hii selikal sio sikivu kabisa nilazima tuishinikize nimelimis sana gazeti la MwanaHalisi mwenyezi umefika muda wa kutia mkono wako amiii
 
Tunamwomba Dr Slaa rais wetu wa moyoni tufungulie gazeti letu Mwanahalisi na Shonza hata kama anasema ukweli
 
LEO ni siku 172 tangu serikali ilifungie gazeti la MwanaHALISI “kwa muda usiojulikana.” Siku hizo ni sawa na miezi mitano na siku 22 au miezi sita kasoro siku nane. Ni nusu mwaka.
Kwa muda usiojulikana maana yake ni mpaka serikali itakapotaka yenyewe. Itakapojisikia. Itakapofurahi. Itakapopigiwa magoti na wamiliki wa gazeti. Itakapoombwa na marafiki wa gazeti. Itakaposhinikizwa vya kutosha na wapigania uhuru wa habari.
Kwa muda usiojulikana yaweza kuwa pale viongozi wa serikali waliolifungia gazeti watakapotembelewa na akili na uelewa kuwa hawapaswi/hawakupaswa kuingilia uhuru wa kupata, kutafuta na kukusanya habari; au pale serikali itakapoamuliwa na mahakama; au wenye gazeti watakapoamua kulichapisha kwa mapenzi ya wananchi bila kujali serikali inasema nini. Hilo nalo linawezekana.
Nusu mwaka. Serikali inayojidai kutenda na kulinda haki za raia wake imeamua kuwa wafanyakazi wa gazeti la MwanaHALISI wawe ombaomba mitaani; au wasambaratike kwa kuhama kampuni au wafe kwa njaa – potelea mbali! Kama hii ndiyo haki, basi ni haki ya mashetani.
Imekuwa safari ndefu – nusu mwaka – lakini iliyojaa karaha na kinyaa. Hapa kuna serikali inayojigamba kutawala kwa “misingi ya demokrasia” lakini ni serikali hiyohiyo inayotaka kutawala gizani – kishirikina na inayonyakua uhuru wa wananchi wake wa kutoa, kupata na kusambaza taarifa na habari.
Hapa kuna watawala wanaojigamba kuwa wakweli na wawazi lakini wanaficha hata kilichowazi kwa kila mmoja.
Wanafungia gazeti kwa nia ya kuua jicho la nyongeza la jamii; kuziba sikio la nyongeza la jamii na kusiliba mdomo wa nyongeza ya jamii. Wanataka jamii mfu – isiyoona uoza, isiyosikia mipango ya “uhaini” dhidi ya jamii na isiyotoa kilio cha wengi.
Kufungiwa kwa MwanaHALISI kulisononesha nyoyo; kukazika shauku, kukanyakua maarifa, kukapora uhuru na kukaondoa mategemeo. Watawala wanajua lakini hawajali.
Hili ni gazeti lililofungiwa wakati habari kuu katika vyombo vyote vya habari nchini ilikuwa “Utekaji na utesaji wa Dk. Steven Ulimboka.” Kufungiwa kwa gazeti, katika mazingira haya, tena kwa muda usiojulikana, kulionekana kwa wasomaji wake, wafuatiliaji na wachunguzi kuwa njia ya kuzima mifereji ya ukweli iliyokuwa ikielekea kumwaga ushahidi mwanana katika macho na masikio ya wasomaji wake.
Funga! Ili lisiandike habari nyeti juu ya unyama aliofanyiwa kiongozi wa madaktari katika kudai vitendeakazi na mazingira bora ya kazi. Funga! Lisifumue taarifa za nyongeza na mkondo wa mawasiliano. Funga! Ili lisiendelee kuumbua wahusika – kuanzia waliobuni “mradi” hadi waliotekeleza. Funga! Ili dunia nje ya Tanzania isije kujua unyama unaohusishwa na serikali.
Leo, kama ilivyokuwa siku ya kwanza ya siku 172 za kifungo cha MwanaHALISI, ninaendelea kukubaliana na wasomaji, wafuatiliaji na wachunguzi juu ya sababu za kufungiwa kwa gazeti: Kuingiza taifa gizani ili lisiweze kuona masuala muhimu ambayo gazeti hili limekuwa likiibua.
Kinachosikitisha ni kwamba watawala, kwa upofu wao, katika suala la Ulimboka, hawakuona kuwa gazeti lilikuwa linatoa taarifa za ndani na za kweli ambazo zingesaidia serikali kujiondoa katika tope la “kutaka kumuua Ulimboka”.
Watawala walishindwa, labda kwa kiwewe tu, kuelewa kuwa taarifa za ndani na za kina zingeonyesha muhusika mmoja na siyo serikali yote wala ikulu yote. Hawakuona kwamba taarifa za kina zingesafisha hata Usalama wa Taifa na Polisi – ambao ndio walikuwa wanatungwa kidole.
Kwa vipi? Ikulu siyo pango la wauaji. Ni makao makuu ya mtawala wa nchi. Haitarajiwi kuwa makazi ya watekaji, watesaji au wauaji.
Kwa hiyo, kama ikulu kuna mtuhumiwa mmoja, watawala wana haki na sababu ya kuachia wanaojua kazi kuwasaidia kufichua nani anachafua heshima na uhalali wa ikulu.
Vivyo hivyo kwa usalama wa taifa. Hawanabudi kukaa kitako na hata kuomba msaada wa nyongeza kutoka kwa wanaojua kazi yao, ili kufichua wanaotaka “kuharibu sifa” yao. Kwani, kazi ya usalama wa taifa siyo kuteka, kutesa na kuua. Anayefanya hayo sharti awekwe wazi ili chombo hicho kibaki kikiaminiwa. Vivyo hivyo kwa jeshi la polisi.
Mvumo wa taarifa za gazeti ambao ungetunga wahusika mmoja mmoja kama shanga katika “sakata la Ulimboka” ungenusuru ikulu, usalama wa taifa na polisi. Hapo ndipo ukweli na uwazi ambavyo vinaimbwa, vingesaidia serikali kuondokana na uchafu unaoweza kuiondolea imani ya wananchi na uhalali wake.
Tumekuwa tukiiambia serikali, tena mara nyingi tangu 1985 – kwamba iwapo chombo cha habari kitakosea, basi kipelekwe mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. Watawala hawataki hilo, bali wanataka kuonyesha kuwa wako juu ya sheria za nchi. Wanatumia ubabe.
Amini usiamini. Hata madikteta wanahitaji taarifa na habari sahihi na za kina; hata zile zinazoonyesha wanavyonyukana ndani kwa ndani. Wameachana na ubazazi wa kufikiri kuwa kama gazeti halikuandika au limezuiwa kuandika, basi jambo husika halitafahamika na hivyo watatulia. Hawafanyi hivyo leo. Wanakataa kuishi kwa umbeya au vitaarifa vya kuwapongeza, kuwasifu na kuwapakata, wakati halihalisi ni tofauti.
Serikali ambayo haina taarifa juu yake na haijui wananchi wanasema au wanajua nini juu yake na wao wenyewe; haiwezi kuchukua hatua. Sasa serikali inayoua vyombo vya habari hadi itakapopakatwa, kubembelezwa na kupigwa busu, siyo serikali ya wananchi.
Hata kama watawala wake watadai kuwa walichaguliwa na wananchi, sharti tukubaliane kuwa ilikuwa kiinimacho. Huwezi kuchaguliwa kutawala halafu ukapora waliokuchagua uhuru wao wa kufikiri na uhuru wa kauli.
Ni siku 172 leo tangu serikali izuie wasomaji kuona kipenzi chao MwanaHALISI. Vyombo vingine vya habari havijaguswa, haina maana kwamba serikali ina ushoga wa kudumu na vyombo hivyo. Vikitaka haki vitazimwa. Vikitaka uhuru vitaning’inizwa. Vikitaka ukweli vitafungiwa “kwa muda usiojulikana”.
Kisichoeleweka vema na haraka kwa wengi ni kwamba kuifungia MwanaHALISI au gazeti kama hilo au lolote lile lililokwishajitambulisha kuwa mdomo wa umma, ni kuweka kifungoni mamilioni ya watu na kuwaondolea kichocheo cha kufikiri.
Wangapi watakubali kubaki kifungoni bila kuhukumiwa na mahakama bali kwa utashi dhaifu na “hukumu” ya waliobeba mamlaka ya kisiasa? Binafsi, sikubali!


makala hii ya ndimara Tegambwage.Wadau tutafute njia ya kulikowa GAZETI HILI
 
..............................................................
 
"Hapa kuna watawala wanaojigamba kuwa wakweli na wawazi lakini wanaficha hata kilichowazi kwa kila mmoja"
Source:Tanzania Daima 18/1/2013
 
"Wangapi watakubali kubaki kifungoni bila kuhukumiwa na mahakama bali kwa utashi dhaifu na “hukumu” ya waliobeba mamlaka ya kisiasa? Binafsi, sikubali!"
Source:Tanzania Daima 18/1/2013
 
thread iko hewani haieleweki ni bora ungeweka habari yote hapa.
 
Mmeshafulia kaeni kimya watu tufanye mambo mengine .... tulikuwa tusinywe maji kila siku hikii mara kileee mara hikiii
Sheinz type...
Mtuache tupumueeeee

Nyie magamba nawachukia sana mnafuraiya ujinga
 
Kwa vile Mungu huwa Hashindwi kitu , basi bila ya shaka yoyote Mwanahalisi litashinda njama za Watawala , na litarudi mitaani .
 
Tulianzisheni, tulianzisheni, tulianzisheni...
 
Back
Top Bottom