Kufungiwa kwa gazeti la mwanahalisi:

Kufungiwa kwa gazeti la mwanahalisi:

Tumelimis sana,nahiyo nikwasababu ya wanahabari kukosa umoja kwani wakiamua sisiku moja tu linafunguliwa? Waandish wa habar wa pigania haki wakiungana mbona mda mdogo na sheria kandamiz mbona itakua mwisho.tatizo wa wanahabar wetu hawajuan.kila mtu anabutua awezavyo haya sasa tz daima nalo dk yoyote watalibani maana imeamua kufuata alipo ishia mwana halisi.tulikupenda lakini kwa uzaifu wa wana habari ccm ilikupenda zaid.me sikuiz hua sisomi magazeti kwani magazeti yalikua matatu tu moja lilisha nunuliwa,lingine lilifungiwa limebaki moja tu sina ham na nch yangu nisha choka
 
Wasajili gazeti lingine tu! Kulifungulia mwanahalisi mpaka utawala uliopo umalize muda wake,Kulifungulia kwa sasa ni sawa na kumsamehe babu Seya na Papii Kocha kitu ambacho hakiwezekani kufanyika kwa utawala huu.
 
Daima Tutakukumbuka!

A1-MWANAHALISI-GAZETI+LA+MWANAHALISI-SAED+KUBENEA-TANZANIA+NEWSPAPERS-MAGAZETI+YA+TANZANIA-HABARI+ZA+TANZANIA-TANZANIA+NEWS-PRESS.JPG
 
[h=2]Ni muda mrefu sasa gazeti la mwanahalisi limefungiwa kwa sababu za kisiasa. Wanaharakati tuungane kushinikiza gazeti hili kipenzi cha watanzania lifunguliwe. Vyama vya siasa makini pia vichangie kuhusu suala la mwanahalisi kufunguliwa kwa kuishinikiza serikali ifuate sheria kwa kuifungulia kesi gazeti hilo na si kuliweka kizuizini kama mhaini. Naomba mchango wenu.[/h]
 
Angalia kesi ya Lema ilivyoamuliwa kihuni wangenyamaza magamba wangefurahi sasa ni wakati wa sheria kuchukua mkondo wake ili magamba waache kuvunja katiba ya nchi. Washinikizwe wapeleke kesi mahakamani wakaumbuliwe.
 
Kwa kweli watanzania tuwe makini na huu utawala utatufikisha kubaya, ebu angalia Mtu kama Membe anataka Urais wakati ukatili wake umeanza kuonekana. Tuukatae uvunjaji huu wa katiba, wanasheria mko wapi jamani, suala si kusajili gazeti lingine kwani hawa wavunjaji wa katiba watalifungia tuum suala ni kukataa kwa nguvu zote udikteta huu.
 
Tanzania Daima dhubutu wajaribu waone ni kama kuimwaga pombe ya mlevi. Kubenea tupo pamoja tafuta wanasheria na wanaharakati tuanakuunga mkono.
Tumelimis sana,nahiyo nikwasababu ya wanahabari kukosa umoja kwani wakiamua sisiku moja tu linafunguliwa? Waandish wa habar wa pigania haki wakiungana mbona mda mdogo na sheria kandamiz mbona itakua mwisho.tatizo wa wanahabar wetu hawajuan.kila mtu anabutua awezavyo haya sasa tz daima nalo dk yoyote watalibani maana imeamua kufuata alipo ishia mwana halisi.tulikupenda lakini kwa uzaifu wa wana habari ccm ilikupenda zaid.me sikuiz hua sisomi magazeti kwani magazeti yalikua matatu tu moja lilisha nunuliwa,lingine lilifungiwa limebaki moja tu sina ham na nch yangu nisha choka
 
Tatizo waandishi wengi wa Tanzania hawana umoja na ni waoga.
 
Tatizo ni sheria mbovu,kandamizi na zilizopitwa na wakati zinazotumika na serikali ya Tanzania kudhibiti uhuru wa vyombo vya habari.Sheria ingetakiwa iwe ya kumshitaki mwandishi ama gazeti mahakamani kama gazeti limeandika habari ya uongo ama ya kashfa ,na mtuhumiwa apewe nafasi ya kutetea juu ya yale yaliyoandikwa na ndipo mahakama itoe hukumu isiyo na shaka kwamba mtuhumiwa kafanya kosa ama la.

Sheria ya Sasa ambayo imeasisiwa tangu 1976 kipindi cha mfumo wa chama kimoja, inampa uhuru Rais ama waziri wa habari kulifungia gazeti lolote kwa muda wowote atakaojisikia ikiwa amejiridhisha mwenyewe kwamba gazeti limefanya uchochezi.

Katiba mpya inabidi iziangalia sheria mfu kama hizi na kuzibadilisha ili kuendana na wakati wa sasa wa democracy ya vyama vingi ,vyombo vya habari n.k

MCT wawasaidie Mwanahalisi lipate kufunguliwa na waendelee na kazi yao kwa kuzingatia weledi wa taaluma ya habari kama ilivyokua kawaida yao.
 
Tatizo waandishi wengi wa Tanzania hawana umoja na ni waoga.
Kweli kama wale waliokuwa kwenye tume ya Nchimbi kuchunguza kuuawa kwa Mwandishi Mwangosi kule Iringa wakasema polisi si wa kulaumiwa wakati wameua. Sasa hivi wanasubiri kuteuliwa ukuu wa Wilaya maana ndio nafasi zao kwa kuitetea serikali!
 
Mkuu uko sawa lakini kwa sasa kuna haja ya kuchukua hatua fulani kuwashinikiza hawa magamba walifungulie gazeti hilo bila masharti yoyote maana lilitoa habari za ukweli kuhusu kutekwa kwa Ulimboka na ndio maana mpaka sasa kesi yao ya usanii inapigwa tarehe tuu maana wanajua wakidhubutu tuu kumruhusu Malundi atambuliwe na Ulimboka wameumbuka sasa wanabuy time tuu ili siku zisogee mbele watafute usanii mwingine Mungu atupishe mbali na maharamia hawa.
Tatizo ni sheria mbovu,kandamizi na zilizopitwa na wakati zinazotumika na serikali ya Tanzania kudhibiti uhuru wa vyombo vya habari.Sheria ingetakiwa iwe ya kumshitaki mwandishi ama gazeti mahakamani kama gazeti limeandika habari ya uongo ama ya kashfa ,na mtuhumiwa apewe nafasi ya kutetea juu ya yale yaliyoandikwa na ndipo mahakama itoe hukumu isiyo na shaka kwamba mtuhumiwa kafanya kosa ama la.

Sheria ya Sasa ambayo imeasisiwa tangu 1976 kipindi cha mfumo wa chama kimoja, inampa uhuru Rais ama waziri wa habari kulifungia gazeti lolote kwa muda wowote atakaojisikia ikiwa amejiridhisha mwenyewe kwamba gazeti limefanya uchochezi.

Katiba mpya inabidi iziangalia sheria mfu kama hizi na kuzibadilisha ili kuendana na wakati wa sasa wa democracy ya vyama vingi ,vyombo vya habari n.k

MCT wawasaidie Mwanahalisi lipate kufunguliwa na waendelee na kazi yao kwa kuzingatia weledi wa taaluma ya habari kama ilivyokua kawaida yao.
 
Hta hivyo hongreni wanaJF kwa jitihada zenu kuhusu mwanahalisi na ukombozi wa Tanzania kwa ujumla Mungu yuu pamoja nasi.
 
Na Ndimara Tegambwage

LEO ni siku 172 tangu serikali ilifungie gazeti la MwanaHALISI “kwa muda usiojulikana.” Siku hizo ni sawa na miezi mitano na siku 22 au miezi sita kasoro siku nane. Ni nusu mwaka.

Kwa muda usiojulikana maana yake ni mpaka serikali itakapotaka yenyewe. Itakapojisikia. Itakapofurahi. Itakapopigiwa magoti na wamiliki wa gazeti. Itakapoombwa na marafiki wa gazeti. Itakaposhinikizwa vya kutosha na wapigania uhuru wa habari.

Kwa muda usiojulikana yaweza kuwa pale viongozi wa serikali waliolifungia gazeti watakapotembelewa na akili na uelewa kuwa hawapaswi/hawakupaswa kuingilia uhuru wa kupata, kutafuta na kukusanya habari; au pale serikali itakapoamuliwa na mahakama; au wenye gazeti watakapoamua kulichapisha kwa mapenzi ya wananchi bila kujali serikali inasema nini. Hilo nalo linawezekana.

Nusu mwaka. Serikali inayojidai kutenda na kulinda haki za raia wake imeamua kuwa wafanyakazi wa gazeti la MwanaHALISI wawe ombaomba mitaani; au wasambaratike kwa kuhama kampuni au wafe kwa njaa – potelea mbali! Kama hii ndiyo haki, basi ni haki ya mashetani.

Imekuwa safari ndefu – nusu mwaka – lakini iliyojaa karaha na kinyaa. Hapa kuna serikali inayojigamba kutawala kwa “misingi ya demokrasia” lakini ni serikali hiyohiyo inayotaka kutawala gizani – kishirikina na inayonyakua uhuru wa wananchi wake wa kutoa, kupata na kusambaza taarifa na habari.

Hapa kuna watawala wanaojigamba kuwa wakweli na wawazi lakini wanaficha hata kilichowazi kwa kila mmoja.

Wanafungia gazeti kwa nia ya kuua jicho la nyongeza la jamii; kuziba sikio la nyongeza la jamii na kusiliba mdomo wa nyongeza ya jamii. Wanataka jamii mfu – isiyoona uoza, isiyosikia mipango ya “uhaini” dhidi ya jamii na isiyotoa kilio cha wengi.

Kufungiwa kwa MwanaHALISI kulisononesha nyoyo; kukazika shauku, kukanyakua maarifa, kukapora uhuru na kukaondoa mategemeo. Watawala wanajua lakini hawajali.

Hili ni gazeti lililofungiwa wakati habari kuu katika vyombo vyote vya habari nchini ilikuwa “Utekaji na utesaji wa Dk. Steven Ulimboka.” Kufungiwa kwa gazeti, katika mazingira haya, tena kwa muda usiojulikana, kulionekana kwa wasomaji wake, wafuatiliaji na wachunguzi kuwa njia ya kuzima mifereji ya ukweli iliyokuwa ikielekea kumwaga ushahidi mwanana katika macho na masikio ya wasomaji wake.

Funga! Ili lisiandike habari nyeti juu ya unyama aliofanyiwa kiongozi wa madaktari katika kudai vitendeakazi na mazingira bora ya kazi. Funga! Lisifumue taarifa za nyongeza na mkondo wa mawasiliano. Funga! Ili lisiendelee kuumbua wahusika – kuanzia waliobuni “mradi” hadi waliotekeleza. Funga! Ili dunia nje ya Tanzania isije kujua unyama unaohusishwa na serikali.

Leo, kama ilivyokuwa siku ya kwanza ya siku 172 za kifungo cha MwanaHALISI, ninaendelea kukubaliana na wasomaji, wafuatiliaji na wachunguzi juu ya sababu za kufungiwa kwa gazeti: Kuingiza taifa gizani ili lisiweze kuona masuala muhimu ambayo gazeti hili limekuwa likiibua.

Kinachosikitisha ni kwamba watawala, kwa upofu wao, katika suala la Ulimboka, hawakuona kuwa gazeti lilikuwa linatoa taarifa za ndani na za kweli ambazo zingesaidia serikali kujiondoa katika tope la “kutaka kumuua Ulimboka”.

Watawala walishindwa, labda kwa kiwewe tu, kuelewa kuwa taarifa za ndani na za kina zingeonyesha muhusika mmoja na siyo serikali yote wala ikulu yote. Hawakuona kwamba taarifa za kina zingesafisha hata Usalama wa Taifa na Polisi – ambao ndio walikuwa wanatungwa kidole.

Kwa vipi? Ikulu siyo pango la wauaji. Ni makao makuu ya mtawala wa nchi. Haitarajiwi kuwa makazi ya watekaji, watesaji au wauaji.

Kwa hiyo, kama ikulu kuna mtuhumiwa mmoja, watawala wana haki na sababu ya kuachia wanaojua kazi kuwasaidia kufichua nani anachafua heshima na uhalali wa ikulu.

Vivyo hivyo kwa usalama wa taifa. Hawanabudi kukaa kitako na hata kuomba msaada wa nyongeza kutoka kwa wanaojua kazi yao, ili kufichua wanaotaka “kuharibu sifa” yao. Kwani, kazi ya usalama wa taifa siyo kuteka, kutesa na kuua. Anayefanya hayo sharti awekwe wazi ili chombo hicho kibaki kikiaminiwa. Vivyo hivyo kwa jeshi la polisi.

Mvumo wa taarifa za gazeti ambao ungetunga wahusika mmoja mmoja kama shanga katika “sakata la Ulimboka” ungenusuru ikulu, usalama wa taifa na polisi. Hapo ndipo ukweli na uwazi ambavyo vinaimbwa, vingesaidia serikali kuondokana na uchafu unaoweza kuiondolea imani ya wananchi na uhalali wake.

Tumekuwa tukiiambia serikali, tena mara nyingi tangu 1985 – kwamba iwapo chombo cha habari kitakosea, basi kipelekwe mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. Watawala hawataki hilo, bali wanataka kuonyesha kuwa wako juu ya sheria za nchi. Wanatumia ubabe.

Amini usiamini. Hata madikteta wanahitaji taarifa na habari sahihi na za kina; hata zile zinazoonyesha wanavyonyukana ndani kwa ndani. Wameachana na ubazazi wa kufikiri kuwa kama gazeti halikuandika au limezuiwa kuandika, basi jambo husika halitafahamika na hivyo watatulia. Hawafanyi hivyo leo. Wanakataa kuishi kwa umbeya au vitaarifa vya kuwapongeza, kuwasifu na kuwapakata, wakati halihalisi ni tofauti.

Serikali ambayo haina taarifa juu yake na haijui wananchi wanasema au wanajua nini juu yake na wao wenyewe; haiwezi kuchukua hatua. Sasa serikali inayoua vyombo vya habari hadi itakapopakatwa, kubembelezwa na kupigwa busu, siyo serikali ya wananchi.

Hata kama watawala wake watadai kuwa walichaguliwa na wananchi, sharti tukubaliane kuwa ilikuwa kiinimacho. Huwezi kuchaguliwa kutawala halafu ukapora waliokuchagua uhuru wao wa kufikiri na uhuru wa kauli.

Ni siku 172 leo tangu serikali izuie wasomaji kuona kipenzi chao MwanaHALISI. Vyombo vingine vya habari havijaguswa, haina maana kwamba serikali ina ushoga wa kudumu na vyombo hivyo. Vikitaka haki vitazimwa. Vikitaka uhuru vitaning’inizwa. Vikitaka ukweli vitafungiwa “kwa muda usiojulikana”.

Kisichoeleweka vema na haraka kwa wengi ni kwamba kuifungia MwanaHALISI au gazeti kama hilo au lolote lile lililokwishajitambulisha kuwa mdomo wa umma, ni kuweka kifungoni mamilioni ya watu na kuwaondolea kichocheo cha kufikiri.

Wangapi watakubali kubaki kifungoni bila kuhukumiwa na mahakama bali kwa utashi dhaifu na “hukumu” ya waliobeba mamlaka ya kisiasa? Binafsi, sikubali!
 
Miongoni mwa mambo ambayo yanamfanya mwananchi wa kawaida mwenye uelewa wa mambo kuwa na mashaka na serikali yake juu ya usalama wake ni hatua za kulifungua mwanahalisi. Binafsi mpaka sasa naamini ukimya wa serikali juu ya sakata la kutekwa na kuteswa kwa uliomboka ukiunganisha nukta na jinsi Mulindi anavyo omba Ulimboka aletwe ili amtambue, na jinsi mwanahalisi lilivyo andika mawasiliano ya ndani ya wale vigogo wa Ikulu! Hakika unaona giza nene lenye ukungu mzito.

Mzee Ndimara ameuliza vitu vya msingi sana kuamsha fikra mpya! Ona hapa "Watawala walishindwa, labda kwa kiwewe tu, kuelewa kuwa taarifa za ndani na za kina zingeonyesha muhusika mmoja na siyo serikali yote wala ikulu yote. Hawakuona kwamba taarifa za kina zingesafisha hata Usalama wa Taifa na Polisi – ambao ndio walikuwa wanatungwa kidole".

Je kwa maandiko hayo hapo juu ya Mzee Ndimara tuanze kuamini kuwa tumempangisha mtesaji pale magogoni?! Je, kuna watu walio tayari kutesa wengine ili kuuficha ukweli?!

Kama jibu sio, kwa nini walifungie Mwanahalisi sasa na hawataki kulifungulia? Kama lili kuwa linaandika uchochezi kama wanavyo sema. Je, ni kweli habari ya kutekwa na kuteswa ulimboka ilikuwa uongo na hivyo mwanahalisi lilituchochea kwa kuandika uwongo?! Kama ndio, ukweli ni upi sasa mbona hawatuelezi?!
 
A piece worthy reading aisee. Asubuhi asubuhi tu unaamuka unakutana na chai ya nguvu kiasi hiki, chakula cha ubongo. Kinachofikirisha. Kwa nini ubongo usiwe na afya. Kwa nini usipanue wigo wako wa kufikiria na kuyachukulia masuala katika mawanda mapana na makubwa zaidi. Kwa manufaa ya wengi wasioweza kupata nafasi kama hizi.

Asante ndi. Unastahili kiti cha meza kuu kwenye taaluma yetu ambayo kuna kila dalili tumeanza kurudi kwa kasi miaka ile ya 1995-2005. Wenye kujua wanajua.
 
Mzee Ndimara Tegambwage kweli umebobea. Hatuwezi kukaa kimya kwa kipindi chote hiki tukikosa kupata habari za kiuchunguzi za Mwanahalisi. LAzima tuchukue hatua. Hata ikibidi kwa maandamano ya nchi nzima ili watawala na jumuiya za kimataifa wajue kwamba tumechoshwa na sheria hizi kandamizi.

Tukikaa kimya, tutalisahau Mwanahalisi.
 
itakua ni usaliti mkubwa kwa wana JF wote na wapigania haki nchi hii tusipolipigania gazeti la mwanahalisi likarud mitaani hasa na issue za investigative news!!!! hili ni kati ya magazeti machache lililokua likitoa habari zenye uchunguzi hadi kufungiwa ni kutokana na ukweli kwamba hakuna kilichokua kikiandikwa kisicho na ushahidi ndio mana serikali ilishindwa kulipeleka mahakamani badala yake ikatumia mabavu ya kulifunga kinyume kabisa na misingi ya demokrasia inayosimamia!!!!
 
Mwanahalisi ni gazeti lililokuwa likisaidia usalama wa Taifa kufanya kazi kwa ufanisi. Namshangaa sana huyu mtu aliyelifungia. Ni mtanzania kweli?
 
Umoja wa kitaifa katika kupigania mambo ya maendeleo umedorora sana.Watanzania wengi bado ni wajinga na hatujakomboka kifikra.Ni ngumu sana kuweza kukusanyika na kutetea jambo kama hilo.Kuna kamsemo maarufu kamtaani kanasema"TATIZO SHULE".Labda wanazuoni mliobobea kwenye sheria mjipange kwenda kuwatetea mahakamani kama inawezekana ila nguvu ya umma mmmh baadae sana.
 
Back
Top Bottom