Kufunga ndoa kwa Mkuu wa Wilaya

Kufunga ndoa kwa Mkuu wa Wilaya

Sasa kwa Imani yake, si itakua anahesabika kuwa anazini tu?

Ndoa ni yako mzee baba hebu we ifanyie maamuzi, ukiona unaweza kuishi nae haya, ila usimind ukiitwa kafiri.
Dah!! Hapo napo kunahusika, upande wa ndugu zake itakua kasheshe
 
Acha ujinga wewe kijana
Oa wa dini yako
Asiye sikia la mkuu.....
Malizia mwenyewe
Mimi nishasema
Moto ukiwaka humo ndani sisi hatupo
 
  • Thanks
Reactions: THT
Wadau kuna mrembo flani hivi ni muislamu ila tumeelewana sana na tunatamani tuishi kama mume na mke, mm ni mkristo. Tatizo la huyo manzi hataki kubadili dini na ameshauri kama tukikibalina kuishi pamoja basi tukafunge ndoa kwa mkuu wa wilaya. Nawaza sana kuikabidhi ndoa yangu kwa mkuu wa wilaya badala ya kumkabidhi Mungu. Nilitamani sana tufunge ndoa kanisani halafu baada ya ndoa kila mmoja aendelee na dini yake ila manzi kagoma.
La pili nilitaka uzoefu wenu kuhusu kuishi na mwenza wako akiwa ni dini tofauti, nawaza pia watoto wanaweza kumfwata mama yao kwenye dini yake wakati mm natamani wanifwate kwenye ukristo. Naombeni ushauri wadau
Hakuna ndoa hapo, utapata shida sana badae. Kama hataki siyo tu kubadilisha dini lakini hata kuingia kanisani kufunga ndoa then aendelee na imani yake basi hafai kuwa ubavu. Kaa mbali na bom hilo.
 
unaelewa kwanini umeumbwa Mwanaume.??

kwenye kila kitu hapa duniani Mwanaume ni kiongozi, ndiyo maana YESU KRISTO alikumbwa Mwanaume, Mtume MOHAMAD aliumbwa Mwanaume, Mungu hakuwa mjinga kufanya hivi..

Namaanisha kama huyo Mwanamke anakupenda kweli, na anatambua wewe ni Mwanaume, ilipaswa umpe kauli mona tu kuwa abadili dini muishi pamoja na akubali..

usifunge ndo ya kwa DC hiyo ni mahsusi kwaajili ya security ya mwanamke haswa mkitengana itamsaidia kwa nyie kugawana mali ulizochuma..

maana ya ndoa ni Mungu kuwatambua ninyi ni mwili mmoja, na hamfanyi dhambi ya uzinzi bali ni mke na mume halali..
Ni kweli mkuu.. Ndoa ya kwa DC naona ni mtihani kwangu kiimani, naona kabisa namkabidhi DC ndoa yangu badala ya kumkabidhi Mungu
 
Mimi muislam mke wangu Mkristo wa mashahidi, tumefunga ndoa ya bomani maisha matamu mwaka wa tatu huu, Nampa Uhuru hata Akifanyia ibada Home Poa Tu,
Naheshimu Anachokiamini, kikubwa Haiathiri Amani Ndani Ya Nyumba

Huwa sitakagi kujipa vipengele visivyo na maana eti dini watu mnatengana
 
Watu tunasahau kwamba ndoa ni makubaliano ya watu wawili, mkishakubaliana na kuwa na msimamo wengine hawana nafasi. Kinachotakiwa ni chagua sahihi. Unaweza kuolewa au kuoa wa dini moja na wala msidumu. Haya mambo ya hayana fomula. Nimejifunza mambo mengi sana kwenye haya maisha, watu wanashadadia ohh usioe au kuolewa na huyu hakufai, lakini mnapokuwa na matatizo kwenye ndoa yenu hakuna anayejali kila mtu yuko bize na familia yake. Mwishowe unabaki majuto ni mjukuu. Do what is right for you, hakuna atakayekuwa pamoja na wewe ukiwa na matatizo, watabaki kuwa washauri tu na maumivu utayapata nyie. Halafu kwa taarifa yenu ndoa zote ni za serikali ndio maana mnapewa vyeti vinavofanana haijalishi mmefungia wapi.
 
Wadau kuna mrembo flani hivi ni muislamu ila tumeelewana sana na tunatamani tuishi kama mume na mke, mm ni mkristo. Tatizo la huyo manzi hataki kubadili dini na ameshauri kama tukikibalina kuishi pamoja basi tukafunge ndoa kwa mkuu wa wilaya. Nawaza sana kuikabidhi ndoa yangu kwa mkuu wa wilaya badala ya kumkabidhi Mungu. Nilitamani sana tufunge ndoa kanisani halafu baada ya ndoa kila mmoja aendelee na dini yake ila manzi kagoma.
La pili nilitaka uzoefu wenu kuhusu kuishi na mwenza wako akiwa ni dini tofauti, nawaza pia watoto wanaweza kumfwata mama yao kwenye dini yake wakati mm natamani wanifwate kwenye ukristo. Naombeni ushauri wadau
Acha kuforce kingi mkuu, utawasumbua watoto wako.Ndoa yako inakuwa haina radha. tafuta mwanamke atakaye kuwa dina moja na wewe.Ili siku ya jumapili muwemnaondoka kama familia ya baba,mama na watoto mnaongozana kuelekea kanisani.Kuna raha yake bro.
 
Back
Top Bottom