Kufunga ndoa kwa Mkuu wa Wilaya

Kufunga ndoa kwa Mkuu wa Wilaya

Mie ni Muislamu mume Mkirsto mtoto wetu ni Mkirsto pia na watakaokuja wala sijali. Tunaishi kwa amani na upendo mwaka wa tano huu.

Mwanzo ndugu ndio walitaka kutuyumbisha maana sie tulishaamua kua na ndoa ya bomani.Tukasimama imara wakaona tupo serious wametuacha maisha yanaenda poa kabisa.

Mbiu yetu ambayo aliianzisha mume wangu wakati tunaanza mahusiano ni "Dini tunayoshare mimi na yeye ni upendo" ilinishawishi ndio tunaiishi. Tunaamini ukiwapenda unaowazunguka utawatendea mazuri na ukijipenda hutajitendea mabaya. Tunaabudu dini zetu kwa uhuru kabisa iwe nyumbani ama kwenda sehemu za ibada.

Kwahio na wewe pima kama upendo kati yenu ni mkubwa mnaweza kuishi katika mazingira yeyote yale.
Kwa sasa mtaishi kwa upendo kabisa ila itakapofika wakati wakuzihitaji hizi dini za kilimwengu ndo upendo utakapotoweka.
 
Changamoto kweli kweli inapotokea Mume na Mke wana imani tofauti wakibarikiwa kupata Watoto huwa Watoto wakishakuwa na uwezo wa kujitambua wanachagua wenyewe imani yao wanayoipenda kama ni ya Baba au Mama.
 
Mkuu kamwe usijenge kwenye kiwanja chenye mgogoro
 
Hiyo ndoa lazima itaishia kwenye changamoto nzito
 
Wadau kuna mrembo flani hivi ni muislamu ila tumeelewana sana na tunatamani tuishi kama mume na mke, mm ni mkristo. Tatizo la huyo manzi hataki kubadili dini na ameshauri kama tukikibalina kuishi pamoja basi tukafunge ndoa kwa mkuu wa wilaya. Nawaza sana kuikabidhi ndoa yangu kwa mkuu wa wilaya badala ya kumkabidhi Mungu. Nilitamani sana tufunge ndoa kanisani halafu baada ya ndoa kila mmoja aendelee na dini yake ila manzi kagoma.

La pili nilitaka uzoefu wenu kuhusu kuishi na mwenza wako akiwa ni dini tofauti, nawaza pia watoto wanaweza kumfwata mama yao kwenye dini yake wakati mm natamani wanifwate kwenye ukristo.

Naombeni ushauri wadau
Mimi nimeoa msabato, mimi ni mkatoliki. Ndoa tulifungia kanisani kwetu (katoliki), wakatoliki tuna utaratibu wanaita "ndoa mseto", kama mmoja wa wanandoa ni wakatoliki, mwingine sio, ndoa inafungwa ila kila mtu anaendelea na dini yake.
10 years down the line. If I were to go back in time, I would still choose her. Our two kids, wote wamekua wakatoliki. Dini tofauti haijakua kikwazo kwenye ndoa yetu au kutusababishia mikwaruzo/migongano.
Watoto wetu tuliwalelea katika misingi ya kumjua na kumuamini Yesu Kristu (tuna utaratibu wa kuomba kifamilia, kusoma biblia pamoja kifamilia, na pia watoto walivyokua wadogo, walikua wanaenda kanisani na mama yao kwa sababu mimi kazi yangu ilikua ya kusafiri sana, i was never at home-ila end of the day wote wameishia kuwa wakatoliki).
Sijui kama unaelewa mtifuano uliopo (kidini/kiimani) kati ya wakatoliki na wasabato. Kuna watabiri walitabiri kuwa hatutadumu, wanaendelea kusubiri hadi sasa, wanahesabu tu miaka, na wengine wametangulia mbele ya haki kabla ya kushuhudia walichotabiri.
Pia mkuu, kwani Mungu hayupo kwa mkuu wa wilaya? Mungu yupo kanisani tu? Si biblia inasema kuwa mamlaka yote yanatoka kwa Mungu? Na cheti mtakachopewa kwa mkuu wa wilaya ni kile kile ambacho aliefungia kanisani/msikitini anapewa pia. Kumkabidhi Mungu ndoa yako hauhitaji kuapa kanisani. It's you, and your God, in your heart.
Inawezekana ikiwa kinachowaongoza ni UPENDO.
Majighu2015
 
Mimi baada ya kuishi na mwanamke kwa miaka 8 na kupata watoto wawili akataka tufunge ndoa ,ila nibadili dini niwe mkristo mi nimegoma ,ingawa watoto anawapeleka kanisani siku moja moja hiyo sio inshu Sana kwangu,tumefunga ndoa ya bomani,ila sijiskii kama nimeoa au nina Mke,tunaishi mbalimbali kwa muda mrefu ,siku moja nipo nae anadiss eti ndoa gani ile haina hata shamramshara Ili watu wamjue kama yeye ni Mke wa fulani,nikamwambia wewe mwanamke umegoma kubadili dini na Mimi siwezi kubadili dini na kama unaona ndoa haina maana na wewe ndo uliitaka utajijua mwenyewe sitaki kelele, ni hivi haya Maisha bora mtu uishi mwenyewe tu ukiwa na hamu tafuta malaya gonga kalale na si kumfuga mwanamke ndani ni mateso tu
Sasa kwani kufunga ndoa kwa DC kunazuia shamra shamra? Mbona kuna wakulungwa wengi tu wanafunga ndoa kwa DC, baada ya hapo wanaangusha shamra shamra la kufa mtu, sherehe la kukata na shoka, fedha tu iwepo. Sigara Kali
 
Mimi nimeoa msabato, mimi ni mkatoliki. Ndoa tulifungia kanisani kwetu (katoliki), wakatoliki tuna utaratibu wanaita "ndoa mseto", kama mmoja wa wanandoa ni wakatoliki, mwingine sio, ndoa inafungwa ila kila mtu anaendelea na dini yake.
10 years down the line. If I were to go back in time, I would still choose her. Our two kids, wote wamekua wakatoliki. Dini tofauti haijakua kikwazo kwenye ndoa yetu au kutusababishia mikwaruzo/migongano.
Watoto wetu tuliwalelea katika misingi ya kumjua na kumuamini Yesu Kristu (tuna utaratibu wa kuomba kifamilia, kusoma biblia pamoja kifamilia, na pia watoto walivyokua wadogo, walikua wanaenda kanisani na mama yao kwa sababu mimi kazi yangu ilikua ya kusafiri sana, i was never at home-ila end of the day wote wameishia kuwa wakatoliki).
Sijui kama unaelewa mtifuano uliopo (kidini/kiimani) kati ya wakatoliki na wasabato. Kuna watabiri walitabiri kuwa hatutadumu, wanaendelea kusubiri hadi sasa, wanahesabu tu miaka, na wengine wametangulia mbele ya haki kabla ya kushuhudia walichotabiri.
Pia mkuu, kwani Mungu hayupo kwa mkuu wa wilaya? Mungu yupo kanisani tu? Si biblia inasema kuwa mamlaka yote yanatoka kwa Mungu? Na cheti mtakachopewa kwa mkuu wa wilaya ni kile kile ambacho aliefungia kanisani/msikitini anapewa pia. Kumkabidhi Mungu ndoa yako hauhitaji kuapa kanisani. It's you, and your God, in your heart.
Inawezekana ikiwa kinachowaongoza ni UPENDO.
Majighu2015
Upendo ndio kila kitu. Mbona kuna watu wengi wamefunga ndoa za bomani na wanaishi vizuri tu miaka nenda. Wengine tulifunga za kidini na tulikuwa dini moja lakini tuliishia kuachana. Kamwe usiache mtu mnayependana kwa sababu ya dini. Halafu aliyewaaminisha kuwa dini yako ni ya kweli kuliko mwingine ni nani? Wote tuko kwenye dini hizi by default. Kuna mtu alitokewa na Mungu au malaika akaambiwa unachokiamini ndio cha kweli? Wengi tumeaminishwa toka tukiwa wadogo.
 
Mkuu,binadamu tuna vituko sana. Kuna mambo ukiyafikiria unabaki kushangaa sana.
Mimi kuna ndugu zangu walikua wananisema hatari, umepotea unakwenda kuoa msabato? Sijui nini na nini, yaani wakageuka miungu watu na kutoa hukumu. Sasa cha ajabu ukiangalia wao wanaosema hayo; walevi, wazinzi, waongo. Unabaki kunyamaza tu. Yaani mtu anajiona yeye ndo bora sana kwa sababu ya dini yake, na mwingine anamuona takataka na mdhambi kisa tu yuko dini tofauti na yeye. Navula
 
Mimi nimeoa msabato, mimi ni mkatoliki. Ndoa tulifungia kanisani kwetu (katoliki), wakatoliki tuna utaratibu wanaita "ndoa mseto", kama mmoja wa wanandoa ni wakatoliki, mwingine sio, ndoa inafungwa ila kila mtu anaendelea na dini yake.
10 years down the line. If I were to go back in time, I would still choose her. Our two kids, wote wamekua wakatoliki. Dini tofauti haijakua kikwazo kwenye ndoa yetu au kutusababishia mikwaruzo/migongano.
Watoto wetu tuliwalelea katika misingi ya kumjua na kumuamini Yesu Kristu (tuna utaratibu wa kuomba kifamilia, kusoma biblia pamoja kifamilia, na pia watoto walivyokua wadogo, walikua wanaenda kanisani na mama yao kwa sababu mimi kazi yangu ilikua ya kusafiri sana, i was never at home-ila end of the day wote wameishia kuwa wakatoliki).
Sijui kama unaelewa mtifuano uliopo (kidini/kiimani) kati ya wakatoliki na wasabato. Kuna watabiri walitabiri kuwa hatutadumu, wanaendelea kusubiri hadi sasa, wanahesabu tu miaka, na wengine wametangulia mbele ya haki kabla ya kushuhudia walichotabiri.
Pia mkuu, kwani Mungu hayupo kwa mkuu wa wilaya? Mungu yupo kanisani tu? Si biblia inasema kuwa mamlaka yote yanatoka kwa Mungu? Na cheti mtakachopewa kwa mkuu wa wilaya ni kile kile ambacho aliefungia kanisani/msikitini anapewa pia. Kumkabidhi Mungu ndoa yako hauhitaji kuapa kanisani. It's you, and your God, in your heart.
Inawezekana ikiwa kinachowaongoza ni UPENDO.
Majighu2015
Nice advise
 
Mnaelewana sana harafu hataki badili dini na wewe hutaki pia. Tafsiri yake ni kwamba hamuelewani kabisa.
Wadau kuna mrembo flani hivi ni muislamu ila tumeelewana sana na tunatamani tuishi kama mume na mke, mm ni mkristo. Tatizo la huyo manzi hataki kubadili dini na ameshauri kama tukikibalina kuishi pamoja basi tukafunge ndoa kwa mkuu wa wilaya.

Nawaza sana kuikabidhi ndoa yangu kwa mkuu wa wilaya badala ya kumkabidhi Mungu. Nilitamani sana tufunge ndoa kanisani halafu baada ya ndoa kila mmoja aendelee na dini yake ila manzi kagoma.

La pili nilitaka uzoefu wenu kuhusu kuishi na mwenza wako akiwa ni dini tofauti, nawaza pia watoto wanaweza kumfwata mama yao kwenye dini yake wakati mimi natamani wanifwate kwenye ukristo.

Naombeni ushauri wadau
 
Ugumu ukoje chief
Alafu wewe inaonekana unakaubishi fulani yaani unaona unachotaka kufanya ni sawa(unaomba ushauri tyari ukiwa na maamuzi)yaani wewe hilo suala unalichukulia kirahisi wakati wote mna itikadi kali za kidini,nikutakie kila lenye kheri
 
Kama alikukazia kwenye dini basi jiandae kuletewa kiburi cha ajabu hapo ndani.

Wanawake huwa anakutest na mambo serious akuone msimamo wako, ukitikisika tu basi imekula kwako.....

Sasa wewe umesikia wapi mwanaume unabadili dini au mwanamke anakukazia kubadili dini yake kuja ya kwako....?!

Ipo hivi, ni wazi kwamba huyo mwanamke yeye anatazama yeye anachotaka.... Mwanamke huwa anakabidhi maisha yake kwa mwanaume wake MUNGU anawaongoza wote.....

Mwanamke hanaga dini yeye anaweza olewa na kubadili dini kufuata maelekezo ya mwanaume wake....

Tafuta manzi mwingine haraka sana.... Huyu pukutisha sasa hivi....

Hata ungekuwa ni mwanaume wa kiislamu, mpagani, buda, mhindu, au hata rastafariani.... usikubali kubadili dini kufuata imani ya mwanamke, huo ni udhaifu mkubwa sana.

Hapo mwanamke kakupima. Haws mabinti wa sasa wanaviburi sana..... Kwenda shule kumewatoa sana katika mitazamo ya imani na uimara katika maisha ya ki MUNGU ......
Mkuu sijawaza kabisa swala na mm kubadili dini.
 
Kama ni wewe ni Mkatoliki nenda walau ukafunge ya mseto kanisani, hiyo ya Bomani kiimani utaendelea kuwa mzinifu na mzinishaji. Yaani hapo kama imeshindikana kabisa kumshawishi akufuate. Kama ni dhehebu lingine sifahamu utaratibu
Kwa taarifa yako ukishatoa mahari na pande zote mbili za wazazi zikakubaliana hapo tayari ni ndoa na hazini..hayo ya kanisani na msikitini ni mipango yenu tu kiimani..ila maandiko yanautamua muunganiko huo.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnatishana tu.!! Mi mzee wangu kafunga hiyo ndoa ya Bomani tangia enzi hizo mpaka leo anazeeka na Mkewe na wana watoto vizuri
Tatizo watu wako brain washed na hizi dini..ila kimsingi suala la ndoa..linapata kibali pale wazazi wa pande mbili wakiridhia huo muunganiko..hapo tayari mi mke na mume..hata huko makanisani sijui kwenye masinagogi..wengi wanafuata cheti tu ambacho kinatoka bomani..mana kama uzinzi hata hao wanaowafungisha ndoa ni wazinzi wakutupa..

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli mkuu.. Ndoa ya kwa DC naona ni mtihani kwangu kiimani, naona kabisa namkabidhi DC ndoa yangu badala ya kumkabidhi Mungu
Ndoa ni baraka za wazazi..usiwe brainwashed wewe na imani za kuletwa...lipa mahari anzeni kuishi kama mnapendana kweli..likijaga hili suala naonaga dini zimeleta utengano zaidi katika jamii zetu..

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu tunasahau kwamba ndoa ni makubaliano ya watu wawili, mkishakubaliana na kuwa na msimamo wengine hawana nafasi. Kinachotakiwa ni chagua sahihi. Unaweza kuolewa au kuoa wa dini moja na wala msidumu. Haya mambo ya hayana fomula. Nimejifunza mambo mengi sana kwenye haya maisha, watu wanashadadia ohh usioe au kuolewa na huyu hakufai, lakini mnapokuwa na matatizo kwenye ndoa yenu hakuna anayejali kila mtu yuko bize na familia yake. Mwishowe unabaki majuto ni mjukuu. Do what is right for you, hakuna atakayekuwa pamoja na wewe ukiwa na matatizo, watabaki kuwa washauri tu na maumivu utayapata nyie. Halafu kwa taarifa yenu ndoa zote ni za serikali ndio maana mnapewa vyeti vinavofanana haijalishi mmefungia wapi.
Hapa umemaliza kila kitu..tatizo binadamu wabishi na wako brainwashed sana..hawata kuelewa hawa misukule.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom