Kufunga ndoa kwa Mkuu wa Wilaya

Kufunga ndoa kwa Mkuu wa Wilaya

Mimi baada ya kuishi na mwanamke kwa miaka 8 na kupata watoto wawili akataka tufunge ndoa ,ila nibadili dini niwe mkristo mi nimegoma ,ingawa watoto anawapeleka kanisani siku moja moja hiyo sio inshu Sana kwangu,tumefunga ndoa ya bomani,ila sijiskii kama nimeoa au nina Mke,tunaishi mbalimbali kwa muda mrefu ,siku moja nipo nae anadiss eti ndoa gani ile haina hata shamramshara Ili watu wamjue kama yeye ni Mke wa fulani,nikamwambia wewe mwanamke umegoma kubadili dini na Mimi siwezi kubadili dini na kama unaona ndoa haina maana na wewe ndo uliitaka utajijua mwenyewe sitaki kelele, ni hivi haya Maisha bora mtu uishi mwenyewe tu ukiwa na hamu tafuta malaya gonga kalale na si kumfuga mwanamke ndani ni mateso tu
Mtalaamu naona hapo ishu ni ww kukaa mbali na familia, mngekua mpo karibu maisha yangesonga
 
Mie ni Muislamu mume Mkirsto mtoto wetu ni Mkirsto pia na watakaokuja wala sijali. Tunaishi kwa amani na upendo mwaka wa tano huu.

Mwanzo ndugu ndio walitaka kutuyumbisha maana sie tulishaamua kua na ndoa ya bomani.Tukasimama imara wakaona tupo serious wametuacha maisha yanaenda poa kabisa.

Mbiu yetu ambayo aliianzisha mume wangu wakati tunaanza mahusiano ni "Dini tunayoshare mimi na yeye ni upendo" ilinishawishi ndio tunaiishi. Tunaamini ukiwapenda unaowazunguka utawatendea mazuri na ukijipenda hutajitendea mabaya. Tunaabudu dini zetu kwa uhuru kabisa iwe nyumbani ama kwenda sehemu za ibada.

Kwahio na wewe pima kama upendo kati yenu ni mkubwa mnaweza kuishi katika mazingira yeyote yale.
Ahsante sana kwa huu ushauri. Nimejifunza jambo hapo, kwenye swala la kuabudu, ww naamini unaswali msikitini. Mtoto haimsumbui kumuona mama anasali sehemu tofauti na mama?
 
Mimi nimeoa msabato, mimi ni mkatoliki. Ndoa tulifungia kanisani kwetu (katoliki), wakatoliki tuna utaratibu wanaita "ndoa mseto", kama mmoja wa wanandoa ni wakatoliki, mwingine sio, ndoa inafungwa ila kila mtu anaendelea na dini yake.
10 years down the line. If I were to go back in time, I would still choose her. Our two kids, wote wamekua wakatoliki. Dini tofauti haijakua kikwazo kwenye ndoa yetu au kutusababishia mikwaruzo/migongano.
Watoto wetu tuliwalelea katika misingi ya kumjua na kumuamini Yesu Kristu (tuna utaratibu wa kuomba kifamilia, kusoma biblia pamoja kifamilia, na pia watoto walivyokua wadogo, walikua wanaenda kanisani na mama yao kwa sababu mimi kazi yangu ilikua ya kusafiri sana, i was never at home-ila end of the day wote wameishia kuwa wakatoliki).
Sijui kama unaelewa mtifuano uliopo (kidini/kiimani) kati ya wakatoliki na wasabato. Kuna watabiri walitabiri kuwa hatutadumu, wanaendelea kusubiri hadi sasa, wanahesabu tu miaka, na wengine wametangulia mbele ya haki kabla ya kushuhudia walichotabiri.
Pia mkuu, kwani Mungu hayupo kwa mkuu wa wilaya? Mungu yupo kanisani tu? Si biblia inasema kuwa mamlaka yote yanatoka kwa Mungu? Na cheti mtakachopewa kwa mkuu wa wilaya ni kile kile ambacho aliefungia kanisani/msikitini anapewa pia. Kumkabidhi Mungu ndoa yako hauhitaji kuapa kanisani. It's you, and your God, in your heart.
Inawezekana ikiwa kinachowaongoza ni UPENDO.
Majighu2015
Thanks kwa story yako ndugu. Unachomaanisha ni kuwa si lazima sana kufunga ndoa dhehebu flani, cha msingi ni imani mliyo nayo baina yenu.
Hapo kwenye cheti cha ndoa, ina mana waliioona msikitini, kanisani au kwa DC wanapewa cheti hicho hicho? Na ukifunga ndoa kwa DC kanisa au msikiti wanaitambua?
 
unaelewa kwanini umeumbwa Mwanaume.??

kwenye kila kitu hapa duniani Mwanaume ni kiongozi, ndiyo maana YESU KRISTO alikumbwa Mwanaume, Mtume MOHAMAD aliumbwa Mwanaume, Mungu hakuwa mjinga kufanya hivi..

Namaanisha kama huyo Mwanamke anakupenda kweli, na anatambua wewe ni Mwanaume, ilipaswa umpe kauli mona tu kuwa abadili dini muishi pamoja na akubali..

usifunge ndo ya kwa DC hiyo ni mahsusi kwaajili ya security ya mwanamke haswa mkitengana itamsaidia kwa nyie kugawana mali ulizochuma..

maana ya ndoa ni Mungu kuwatambua ninyi ni mwili mmoja, na hamfanyi dhambi ya uzinzi bali ni mke na mume halali..
Kwani ndoa za kanisani au msikitini hazimpi mwanamke au mwanaume security ya mali?
Pia tukifunga ndoa ya kwa DC Mungu hataitambua ndoa yetu?
 
Thanks kwa story yako ndugu. Unachomaanisha ni kuwa si lazima sana kufunga ndoa dhehebu flani, cha msingi ni imani mliyo nayo baina yenu.
Hapo kwenye cheti cha ndoa, ina mana waliioona msikitini, kanisani au kwa DC wanapewa cheti hicho hicho? Na ukifunga ndoa kwa DC kanisa au msikiti wanaitambua?
Cheti ni kile kile. Kwa sababu cheti kinatolewa na Serikali ya Jamhuri.
Hapo kwenye kutambulika Kanisani ndo changamoto sasa! Kanisani haitambuliki! Ila nikuulize tu saali fikirishi, ndoa ya Adam na Hawa ilifungiwa kanisani? NDOA NI YA WATU WAWILI.
Ila pia mkifungia kanisani, kule kwa mwenzako pia (msikitini) haitambuliki vile vile! (Japokua mkifungia kwa DC, haitatambulika kote kote, msikitini wala kanisani).
Hapo inabidi nyie wenyewe sasa wahusika mkae kwa utaratibu na muangalie pande zote... Mfanye consideration zote, kabla hamjaamua.
Sio kwa kupigizana kelele, ila kwa upendo. Ni uamuzi mgumu ila huwa rahisi kukiwa na UPENDO.Angalieni options ZOTE zilizopo na faida/hasara zake na mtafakari.
 
Ahsante sana kwa huu ushauri. Nimejifunza jambo hapo, kwenye swala la kuabudu, ww naamini unaswali msikitini. Mtoto haimsumbui kumuona mama anasali sehemu tofauti na mama?
Bado mdogo 3 year's old ila kama akijitambua na akawa na maswali tutampa majibu sahihi.
 
Hili ni moja ya jambo Naposhindwa muelewa Mungu anayeelezwa na waislam na wakristo.

Kama wanasema Mungu ndie muumba wa binadamu, na katika uumbaji huo amewapa Uwezo wa hisia za kutamaniana na kupendana bila mipaka. Iweje tena awawekee mipaka ya kutotimiza kile[kuoana] kilichoanzishwa na uumbaji wake mwenyewe[kupendana]? Kama Mungu hata wasio dini moja waoane, nayeye ndiye Muweza wa yote, kwani in the first place asizuie wasipendane? Why creating this inconvinience?

Kama kweli tunaamini mwanadamu ameumbwa na Mungu, basi Dini ni Anti-God.
 
Mkishidwa kuelewana kwa vitu vidogo ustegemee makubwa mbeleni kila la kheri
 
Acheni kutisha watu acheni waamue mapenzi yao hayo masheria yenu ya kijinga yasiwaharibie mapenzi yao
 
Cheti ni kile kile. Kwa sababu cheti kinatolewa na Serikali ya Jamhuri.
Hapo kwenye kutambulika Kanisani ndo changamoto sasa! Kanisani haitambuliki! Ila nikuulize tu saali fikirishi, ndoa ya Adam na Hawa ilifungiwa kanisani? NDOA NI YA WATU WAWILI.
Ila pia mkifungia kanisani, kule kwa mwenzako pia (msikitini) haitambuliki vile vile! (Japokua mkifungia kwa DC, haitatambulika kote kote, msikitini wala kanisani).
Hapo inabidi nyie wenyewe sasa wahusika mkae kwa utaratibu na muangalie pande zote... Mfanye consideration zote, kabla hamjaamua.
Sio kwa kupigizana kelele, ila kwa upendo. Ni uamuzi mgumu ila huwa rahisi kukiwa na UPENDO.Angalieni options ZOTE zilizopo na faida/hasara zake na mtafakari.
Aisee kwa hiyi kama haitambuliki inamaana hatuwezi kushiriki jambo lolote kama sakramenti kwa sababu kanisa wanaona sisi ni waasherati. Hapo shughuli ipo kwa kweli
 
Mmmh!

Hiyo ndoa lazima itaishia kwenye changamoto nzito. Kufanikiwa hapo ni fifty fifty sana.

Ndoa sio taasisi ya kulazimishana, kutegana au kuvutana. Ndoa ni taasisi ya kupendana na kupatana.

Kama mnapendana lakini mkashindwa kupatana kwenye suala nyeti kama hilo (imani), basi huko mbele ya safari hamuwezi kutoboa.

Kivipi imani inazuia hayo uliyotaja hapo juu mkuu?
 
Back
Top Bottom