Kufunga ndoa kwa Mkuu wa Wilaya

Kufunga ndoa kwa Mkuu wa Wilaya

Majighu2015

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
2,941
Reaction score
3,963
Wadau kuna mrembo flani hivi ni muislamu ila tumeelewana sana na tunatamani tuishi kama mume na mke, mm ni mkristo. Tatizo la huyo manzi hataki kubadili dini na ameshauri kama tukikibalina kuishi pamoja basi tukafunge ndoa kwa mkuu wa wilaya.

Nawaza sana kuikabidhi ndoa yangu kwa mkuu wa wilaya badala ya kumkabidhi Mungu. Nilitamani sana tufunge ndoa kanisani halafu baada ya ndoa kila mmoja aendelee na dini yake ila manzi kagoma.

La pili nilitaka uzoefu wenu kuhusu kuishi na mwenza wako akiwa ni dini tofauti, nawaza pia watoto wanaweza kumfwata mama yao kwenye dini yake wakati mimi natamani wanifwate kwenye ukristo.

Naombeni ushauri wadau
 
Mmmh!

Hiyo ndoa lazima itaishia kwenye changamoto nzito. Kufanikiwa hapo ni fifty fifty sana.

Ndoa sio taasisi ya kulazimishana, kutegana au kuvutana. Ndoa ni taasisi ya kupendana na kupatana.

Kama mnapendana lakini mkashindwa kupatana kwenye suala nyeti kama hilo (imani), basi huko mbele ya safari hamuwezi kutoboa.
 
Kama ni wewe ni Mkatoliki nenda walau ukafunge ya mseto kanisani, hiyo ya Bomani kiimani utaendelea kuwa mzinifu na mzinishaji. Yaani hapo kama imeshindikana kabisa kumshawishi akufuate. Kama ni dhehebu lingine sifahamu utaratibu
 
Mm sio mkatoliki, na hata ningekua mkatoliki huyu mwenzangu hataki ndoa ya kikristo
 
Niliwahi pata msichana wa islamic ukweli tulikuwa tunapendana sana aligoma kubadiri kabisa ila alikuwa na upendo na maadiri sana ilibidi tuachani na kuachana kwetu nilimuomba ahame mkoa ilikuwangumu nikaamua badiri namba ya simu,

Hapa jirani kuna jamaa ameoa mkristo yaani lifestyle yao akizaa mtoto wa kike mama atampeleka kanisani ila akizaa wa kiume baba atampeleka msikitini, na jamaa anampenda mke wake asikwambie mtu, na mwanamke anamheshimu mme wake balaa,
 
unaelewa kwanini umeumbwa Mwanaume.??

kwenye kila kitu hapa duniani Mwanaume ni kiongozi, ndiyo maana YESU KRISTO alikumbwa Mwanaume, Mtume MOHAMAD aliumbwa Mwanaume, Mungu hakuwa mjinga kufanya hivi..

Namaanisha kama huyo Mwanamke anakupenda kweli, na anatambua wewe ni Mwanaume, ilipaswa umpe kauli mona tu kuwa abadili dini muishi pamoja na akubali..

usifunge ndo ya kwa DC hiyo ni mahsusi kwaajili ya security ya mwanamke haswa mkitengana itamsaidia kwa nyie kugawana mali ulizochuma..

maana ya ndoa ni Mungu kuwatambua ninyi ni mwili mmoja, na hamfanyi dhambi ya uzinzi bali ni mke na mume halali..
 
Yote unayotuuliza, wakupatana naye ni huyo unayetegemea kuishi naye. Kama haiwezekani, ujue hilo sio bandiko kwenu, fanya yanayowezekana na kwa kukubaliana na maelewano. Umefukiria wewe kuwa muisilamu?
 
Niliwahi pata msichana wa islamic ukweli tulikuwa tunapendana sana aligoma kubadiri kabisa ila alikuwa na upendo na maadiri sana ilibidi tuachani na kuachana kwetu nilimuomba ahame mkoa ilikuwangumu nikaamua badiri namba ya simu,

Hapa jirani kuna jamaa ameoa mkristo yaani lifestyle yao akizaa mtoto wa kike mama atampeleka kanisani ila akizaa wa kiume baba atampeleka msikitini, na jamaa anampenda mke wake asikwambie mtu, na mwanamke anamheshimu mme wake balaa,
Good experience, ndoa yao waliifungia wapi?
 
Back
Top Bottom