Kufunga kampeni: UKAWA-Jangwani, CCM- Mwanza CCM Kirumba

Kufunga kampeni: UKAWA-Jangwani, CCM- Mwanza CCM Kirumba

Hiyo ni karibu mikoa mitano ila Dar pekee ina kura mil. 3.

Unapokosea ni kuweka target kwa Lowassa tu.
Watu wanapiga pasi ndefu.
Kanda ya ziwa ina majimbo mengi sana ya ubunge
 
UKIWA hamjajiuliza kwanini LUWASA apenda enda Dar kila wakati....muona daktari ili pima afya ngogoro...
 
UKIWA hamjajiuliza kwanini LUWASA apenda enda Dar kila wakati....muona daktari ili pima afya ngogoro...
Kwanza jiulize mbona Kikwete kila siku yupo Marekani?
Wewe unasahau kabisa kuwa Ikulu iko Dar. Lowassa ni lazima kila Mara awepo Dar.
 
Kikwete anagombea cheo gani katika uchaguzi huu?
 
Huenda unaandika hii post uko Dar,ila nikuambir tu kanda ya Ziwa Mgombea pekee atakayeongoza ni Magufuli..."uluulema lekaga nkoi tugwisaga halubuga"


Wewe kuandika kilugha hakubadili uhalisia kuwa Lowasa anachukua 65% ya kura za kanda ya ziwa.
 
Ndio sasa ujue huwezi kumtumia Gwajima kama strategist wako. Hizo milioni 3 za Dar ni za kugawana. Ila za Arusha, Moshi na Manyara ni za uhakika. Kuonesha yupo pamoja nao angefungia kampeni Sheikh Amri Abeid.

Lowassa kwenye uwanja huo au?
 
Chadema wawahi kabisa coverage ya television kabka hawa jamaa hawajalipia zote kwa siku tatu mfululizo.

Hata ukawa wakilipia magamba watahonga na kuwatisha media kuongeza hela nyingi ili wapinzani wakose publicity. Hivyo wapinzani mjiandae kisaikolojia
 
Nawapongeza sana viongozi wa UKAWA,wametumia intelijensia ya hali ya juu katika kupanga sehemu ya kufungia kampeni.
Endapo wangefungia Arusha lingekuwa kosa kubwa sana maana ile dhana ya ukabila ingepata mashiko.
Wale wenzetu sijui kwahili watajitetea vipi....
Sisi UKAWA tuna ukabila,wao wanaofungia kampeni Mwanza wanajitoa vipi katika ukabila?
#KataaUkabila
#TanzaniaNiYetuSote
#ChaguaUKAWA

Mwaka huu lazima rais atoke kanda ya ziwa, take it from me. Hilo la ukabila lipo na sisi wasukuma na vikabila vidogovidogo ni 35% ya wapiga kura wote, 25% wanamkubali mgombea tz nzima, 15% ni wapenda ccm ( iko ndani ya damu na wananufaika nayo). Jumla 85%. Ukawa mtambulia 15%.
 
Umenena vyema mkuu

Watu watamchagua. Magufuli kwakuwa ana Sifa zaidi ya wengine na ana maanisha anachosema au kuahidi. Hadithi za mabadiliko bila kuonyesha njia ya kuyafikia hazina mpango.
 
Back
Top Bottom