Kufuatia wabunge wa CHADEMA kwenda Karantini, Spika Ndugai amshukia Mbowe kama mwewe

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,755
15,238
Spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania mh Job Ndugai wakati akihojiwa na kituo cha luninga kuhusu wabunge wa Chadema kukataa kuingia bungeni kwa madai ya kukwepa Corona amemshukia kama mwewe Freeman Mbowe!

Spika Ndugai amesema Freeman Mbowe kwa muda mrefu amekuwa na tabia za udikteta na hataki kubadilika hata baada ya chama chake kuwa kikubwa.! Spika ameenda mbali zaidi kwa kusema bunge lote ni timu moja na lina uongozi wake lakini Mbowe amechukua uamzi wa kuwatoa wabunge wa Chadema pekee bila kumshirikisha wala kujadiliana na mtu yeyote!
Amesema tabia hizi za ubabe na kuweka upinzani kwenye kila kitu ndiyo zinazopelekea wabunge na madiwani wengi wa chadema kuhama chama hicho. Mbowe anatakiwa ajue Corona ni janga na haijulikani litaishi lini hapa duniani .

Kwa upande wa wabunge waliobaki, Ndugai amesema wataendelea kuchapa kazi kama kawaida na kuwapitishia bajeti wananchi huku akisema kama bunge litaacha kupitisha bajeti na kuiacha serikali ianze kutumia hela bila kuidhinishwa na bunge ni Mbowe huyo huyo tena atakuja kulalamika kwamba serikali inatumia hela bila idhini ya bunge.!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wacha ccm wamalize kazi waliyotumwa na wananchi
Yes maana hata corona ikiwafyekea mbali zaidi ya kugonga meza na ndiyooo wanafaida gani tena?wewe rais kurudia kuteua watu wale wale aliowatumbua kutoka kwenye group la zaidi ya watu zaidi ya 200 unapata picha gani? Wengi ni empty heads
 
Mawazo na michango ya upinzani imrgeuzwa kuwa ni takataka kwani huwa hawapendi kuitambua hivyo hata kutokuwepo kwao bungeni naona mh. Spika atafurahia zaidi maana hakutakuwa na uhakiki wa hoja zitakazotolewa hivyo kuwarasishia chama tawala mteremko wa kufikidha hoja zao

DUMU KUBWA
 
Ni kwel Mahiga kufa afu Ndugai kubak ni hasara kwa Taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
ha ha ha! sidhani kama mkuu umewaza vizuri, nakusihi waza tena upya uje na jibu jingine huku ukijikumbusha Mama mchungaji alishangilia na kugonga meza Zana Za Kilimo auwawe unajua kilichomtokea!! Yule dingi Mgogo ni muhimu mno wakati huu ubabe unahitajika katika ujengaji nchi ya watu waliozoea uvivu, wizi, udalali na ufisadi, Mzee Baba akimaliza ngwe yake ya pili nae anaweza kupumzika!! ana faida kubwa ukiwaza vizuri!
 
Etwege,
1. Kwa vile tumeambiwa kuwa Bunge lijalo litakuwa 100% CCM, hii itakuwa nafasi nzuri kutuonyesha litakavyokuwa.

2. Nilitarajia Mheshimiwa Spika angeueleza umma hatua gani wanachukua kuepuka maambukizo maana kwa mfumo wa Bunge ni vigumu kuwa na social distancing.

3. Badala ya kumshambulia KUB, angetusaidia zaidi kama angejibu hoja alizoibua na kutueleza kwa nini hazistahili kutekelezwa. Hii ya kuitana majina haisaidii kitu zaidi ya kupandisha joto linalotokana na ugonjwa wake. Yeye kama Spika alitakiwa kupoza, sio kuchochea moto.

Amandla.....
 
Ndugai ameeleza vizuri sana hatua ambazo bunge limechukua
1. Kwa vile tumeambiwa kuwa Bunge lijalo litakuwa 100% CCM, hii itakuwa nafasi nzuri kutuonyesha litakavyokuwa.
2. Nilitarajia Mheshimiwa Spika angeueleza umma hatua gani wanachukua kuepuka maambukizo maana kwa mfumo wa Bunge ni vigumu kuwa na social distancing.
3. Badala ya kumshambulia KUB, angetusaidia zaidi kama angejibu hoja alizoibua na kutueleza kwa nini hazistahili kutekelezwa. Hii ya kuitana majina haisaidii kitu zaidi ya kupandisha joto linalotokana na ugonjwa wake. Yeye kama Spika alitakiwa kupoza, sio kuchochea moto.

Amandla.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom