Kufeli Mitihani siyo kufeli maisha

King Jody

JF-Expert Member
Oct 8, 2022
914
1,704
Nikiwa katika matembezi mara nikasikia mlio wa honi ya gari kugeuka nakutana na jamaa niliyesoma naye darasa moja, [Class mate] Aliposhusha kioo cha gari na kunisabahi, Nikabaki nashangaa, Jamaa kwa muonekano wa haraka haraka yupo vizuri kiuchumi, Mavazi ya gharama na Micheni ya dhahabu.

Nikakumbuka huyu jamaa darasani alikuwa mmoja wa vilaza, yaani kupata zero ilikuwa kawaida sana.

Je, wewe umewahi kukutana na hali kama hiyo?

Kweli kufaulu mitihani siyo kufaulu maisha, na kufeli mitihani siyo kufeli maisha.

Kwa kifupi maisha hayana formula, Anything is possible by the way.
 
Mkuu haya maisha kwa jinsi yalivyo bila kujifariji hutoboi.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Nipo hapa kwa gari nimecheka daah kweli mkuu...
Yaani umejibu positive sana hata sikutegemea daaah....

Yaan King Jody respect sana 🀝🀝🀝🀝🀝🀝🀝🀝🀝🀝🀝🀝
 
mkuu tazama wasomi katika nafasi mbalimbali
Angalia wasio na elimu walivyo katika hali ya mateso zaidi!!

Ukiachana mafanikio,elimu inasidia sana kutanua mawazo na mapana ya mtu kuwazua changamoto mbalimbali zinazomzunguka.

Pima tu maisha ya mtu ambae ameishia hata kidato nne na mtu ambaye hakwenda shule kabisa.
 
mkuu tazama wasomi katika nafasi mbalimbali
Angalia wasio na elimu walivyo katika hali ya mateso zaidi!!

Ukiachana mafanikio,elimu inasidia sana kutanua mawazo na mapana ya mtu kuwazua changamoto mbalimbali zinazomzunguka.

Pima tu maisha ya mtu ambae ameishia hata kidato nne na mtu ambaye hakwenda shule kabisa.
Ndo maana nikasema maisha hayana formula
 
Tuliofeli darasani tunajifariji kwa kushindana na waliosoma. Tukubalini tu waliosoma wametuzidi kitu, hata kama wanapitia msoto au hawana maisha mazuri.

Waliosoma wanaifaidi dunia kuliko sisi tusiosoma, hata kama tumewazidi kipato. Waliosoma wanaifaidi dunia kwa mapana.
 
Mbona kuna wengine walikuwa ni bright darasani wakafeli mtihani na kurudi mtaani ku straggle maisha na ramani haisomi kisha kujutia kufeli mtihani? Wanaona wangefaulu wasingejikuta katika hali ngumu kiuchumi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom