Kufeli kwa wanafunzi Law School tatizo ni wanafunzi wengi ni vilaza wamezoea kutoa hongo na kununua mitihani

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,074
Najua mtabisha lakini Ukweli utabaki Ukweli.Utaratibu wa kufundisha Kutunga Mitihani kufanya Mitihani kusahihisha Mitihani na kisha Zoezi hilo Huchunguzwa na kuhakikiwa na Bodi kama kuna Dosari na Upendeleo uliofanywa Bodi ikijiridhisha MATOKEO HUTANGAZWA. Utaratibu huo ni Tofauti kabisa na Vyuo vingine.

Vyuoni Mwalimu mmoja ana uwezo wa KUKUFAULISHA. Naipongeza BODI Uongozi na Watendaji wa LAW SCHOOL kwa kusimamia Weledi.

TATIZO la Wanafunzi kufeli linachangiwa na
1. Lugha ya KIINGEREZA ni Tatizo kubwa sana kwa Wanafunzi
2. Vyuo walikotoka hawakuandaliwa ipasavyo
3. Rushwa ya Fedha na Ngono kwa Wanafunzi wengi ili WAFAULU.
4. Kununua Mitihani
LAW SCHOOL hakuna UJINGA HUO pale ni KUSOMA TU

Naipongeza BODI Uongozi na Watendaji ni Bora kupata Wanafunzi Wachache Waliofanya Vizuri kuliko Wengi waliofeli kwa Ajili tu ya kutaka kuwa na IDADI KUBWA ya Waliofaulu

LAW SCHOOL IPO kwa Ajili ya KUWAANDAA WANASHERIA WALIOELIMIKA KISHERIA TANZANIA sio Kichaka cha Wanasheria MAKANJANJA.

Sasa hivi Wanafunzi wengi wa Vyuo vingi ukiangalia VYETI vyao Wana UFAULU wa KUTISHA Lakini HAWAELEWI KITU wengi wana DEGREE za MAGUMASHI.

LAW SCHOOL imekataa UHUNI huo
 
Najua mtabisha lakini Ukweli utabaki Ukweli.Utaratibu wa kufundisha Kutunga Mitihani kufanya Mitihani kusahihisha Mitihani na kisha Zoezi hilo Huchunguzwa na kuhakikiwa na Bodi kama kuna Dosari na Upendeleo uliofanywa Bodi ikijiridhisha MATOKEO HUTANGAZWA.Utaratibu huo ni Tofauti kabisa na Vyuo vingine .Vyuoni Mwalimu mmoja ana uwezo wa KUKUFAULISHA .Naipongeza BODI Uongozi na Watendaji wa LAW SCHOOL kwa kusimamia Weledi.
TATIZO la Wanafunzi kufeli linachangiwa na
1.Lugha ya KIINGEREZA ni Tatizo kubwa sana kwa Wanafunzi
2.Vyuo walikotoka hawakuandaliwa ipasavyo
3.Rushwa ya Fedha na Ngono kwa Wanafunzi wengi ili WAFAULU.
4.Kununua Mitihani
LAW SCHOOL hakuna UJINGA HUO pale ni KUSOMA TU
Naipongeza BODI Uongozi na Watendaji ni Bora kupata Wanafunzi Wachache Waliofanya Vizuri kuliko Wengi waliofeli kwa Ajili tu ya kutaka kuwa na IDADI KUBWA ya Waliofaulu
LAW SCHOOL IPO kwa Ajili ya KUWAANDAA WANASHERIA WALIOELIMIKA KISHERIA TANZANIA sio Kichaka cha Wanasheria MAKANJANJA.
Sasa hivi Wanafunzi wengi wa Vyuo vingi ukuangalia VYETI vyao WanaUFAULU wa KUTISHA Lakini HAWAELEWI KITU wengi wana DEGREE za MAGUMASHI
LAW SCHOOL imekataa UHUNI huo
Binafsi naomba nisema yafuatayo kuhusu shule ya sheria Tanzania:

Mosi, kutokana na uhitaji wa elimu ya kusoma kwa vitendo (Post-Graduate Diploma in Legal Practice) haikutakiwa kuwe na shule moja nchi nzima tena ambayo iko kwenye mji kama Dar es salaam. Walau hizi shule zingekuwepo kikanda ili kuwaepusha na kadhia wale wanafunzi wanaotoka mikoa ya mbali kuja kurudia mitihani Dar es Salaam. Mtoto anasafiri kutoka Tarime, hana hata mkopo halafu anakuja Dar es salaam kufanya mtihani akiwa na 50/50 kwamba hilo somo analorirudia atafuaulu au lah.

Pili, mbinu ya kumpima mwanafunzi (Mode of Assessment) siyo rafiki kabisa na haizingatia utaalamu wa kisaikolojia kwamba wanafunzi wana uelewa tofauti. Mtoto anasoma mwaka mzima halafu anapewa mitihani 24 ndani ya mwaka ambayo kama akifeli hata mmoja basi anaweza kupoteza zaidi hata ya miaka 2 anarudia tu kozi hiyo hiyo. Kikawaida tulitegemea kwenye elimu ya vitendo wanafunzi wapimwe kupitia kazi nyingine muhimu ambazo lazima ziwe na alama, kama PRESENTATIONS, GROUP ASSIGNMENTS, CLINICS + WORKSHOPS and INTERNSHIP WITH MARKS.

Sasa wanaitwa DIPLOMA IN LEGAL PRACTICE huku wakichukua ada ya zaidi ya milioni moja, ilhali vipimo vyote vinatolewa kupitia mitihani. Hii siyo sahihi, kwasababu hata mahakamani kwenyewe wanasheria huwa hatuviziani ila tunapewa muda wa kujiandaa. Sasa mtoto anakaa INTERNSHIP miezi zaidi ya sita huku akija kukaguliwa kihunihuni tu mara moja, bila kupewa alama yoyote ile ya muhimu. Kwanini hawa wanafunzi wasipangiwe hata miezi miwili-miwili kufanya kazi la lazima zenye alamu mahakama za mwanza, mabaraza ya ardhi, mabalaza ya usuluhishi, dawati la jinsia ???

Jingine, ambalo nimeliona ni jambo la kipumbavu kufanywa na watu wanaojiita wasomi ni kitendo cha kutoa matokeo ya mitihani yote ya mwaka mzima ndani ya siku moja, baada ya mwaka mzima na miezi mitatu kupita. Kwanini matokeo ya ICA (Individual Continous Assessment), WPE (WRITTEN PRACTICAL EXAMINATION) na FINALS NON-CORE hayatolewi mapema, ili mwanafunzi ajue mbivu na mbichi na aweze kujipanga vizuri kwenye mitihani ya mwisho ??? Pia wawekewe utaratibu maalamu kabisa wa kuyarudia haya masomo wakati hata wako shule, hasa wiki moja baada ya kumaliza WPE ???

Lingine muhimu ni kwamba LST, kuna mitihani ya WPE (Written Practical Examination) ambayo kwingineko duniani mwanafunzi huifanya kwa kufanya tafiti pamoja na majadiliano na wanafunzi wenzake, kisha baadae huenda kufanya huo mtihani. Ilhali sasa pale LST, wanafunzi wanafungiwa masaa manne (4) wakisoma mavitabu, bila kuruhusiwa kuzungumza halafu wanapewa saa moja kupumzika, ili warudi kufanya mtihani huohuo kwa masaa matatu. (It's just emotional debilitating)

Tatu, hili la kulazimisha kila anayesoma sheria awe wakili nadhani ni jambo la kishenzi ambalo lilifanywa kwa mihemko bila kufikiriwa. Miaka yote huko nyuma watu tuliajiriwa kama STATE ATTORNEYS bila hata kuwa wanasheria. Tulitakiwa tu tufanye INTERNSHIP miezi tisa kwa ATTORNEY GENERAL halafu tunaenda kufanya BAR-EXAMINATION kule Arusha. Kinachoshangaza ni kwamba wengi ambao hawakupita Law School wako vizuri kuliko hata hawa watoto wenu wa Mawasiliano nyuma kule.

Kubwa zaidi, wanasheria tuko kwenye nyanja kuu mbili ambazo ni LEGAL PRACTITIONER (ADVOCATES) na JURIST (LEGAL SCHOLARS/LEGAL RESEARCHERS). Hawa ni watu wawili tofauti na wanafanya kazi tofauti kabisa, sasa ukitaka kuwalazimisha wawe kitu kimoja utakuwa unapuyanga mno. Leo hii ushauri wa sheria wa JURIST unaweza kuwa una uzito kuliko hata ORDINARY LEGAL PRACTITIONER, kutokana na tafiti na ufahamu. Sasa kwenye nchi fulani ya kusadikika, wenyewe kwasababu hawana SPECIALIZATION basi wanalazimisha kila mtu awe wakili, kwamba hata JURIST haweza kutoa ushauri kama hana muhuri. Just Lackadaissical and Nonsensical....

Nne, mtaala wa shule ya sheria ni wa kizamani sana na hauwezi kumfanya mwanafunzi awe vizuri kwenye soko la kimataifa. Kuna baadhi ya masomo tulitegemea yafundishwe pale LST, lakini hayapo kwenye mtaala. Mfano, INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, INVESTMENT LAW, BASICS OF INTERNATIONAL ECONOMICS LAW/ INTERNATIONAL TRADE AND FINANCE LAW. Nchi haina wataalamu wa haya masomo, sisi tunakomaa kufundisha PROPABATE & ADMINISTRATION OF ESTATES, COMMERCIAL LAW, LEGAL ETHICS, HUMAN RIGHTS and ACCOUNTS FOR LAWYERS masomo ambayo vyuo vingi vinayafundisha na vinaweza kuyafundisha vizuri.

Kesi kubwa kama zila za makinikia, DOWANS, ESCROW n.k zinahitaji mwanasheria walau awe anajua masomo ya INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, ambapo anatakiwa aifahamu mikataba mikubwa BIT (Bilateral Investment Treaties), pamoja na taasisi muhumu kama ICSID, PIC, ICC. Lakini sisi tunakomaa kuwafelisha watoto masomo kama ACCOUNTS. Sijui hii nchi haina watu wenye akili kabisa. Mambo ya ajabu yanafanyika na hakuna hata anayestuka.

Tano, mradi wa LST tangu mwaka 2006 marehemu Prof. Mukoyogo aliupinga kweli kwasababu aliona hauna maana zaidi ya kuwatengenezea ulaji baadhi ya wataalamu wa pale University of Dar es Salaam. Hivi kweli, tuna uhakika kwamba haya masomo ya LST hayawezi kufundishwa vizuri kwenye vyuo ambavyo wanafunzi wanasoma wakiwa wanatafuta Shahada ya kwanza kweli ???

Jambo jingine ni kwamba wataalamu wengi wa pale LST wameamua kufanya biashara ya vitabu. Wanatunga mitihani ambayo majibu yake utayapata kama tu umenunua vitabu vyao. Hili nilishawahi kuambiwa nikathibitisha mwenyewe kwenye baadhi ya vitabu. Hii ni tabia ya kishezi ambayo inaumiza na kukwamisha wengine huku wengine wakipata ukwasi mkubwa. Mwanafunzi anataoa pesa nyingi za Ada lakini hivyo vitabu havipo maktaba, utavipata mpaka umfuate mwandishi mwenyewe na umlipe 50,000. Kwanini msiweke vitabu vingi kule maktaba wanafunzi wakavisoma ???

Sita, hivi inawezekanaje mwanafunzi ambaye amefauli vizuri shahada yake afeli vibaya kwa kiwango cha DISCONTINUE pale LST ??? Ina maana huyu mwanafunzi hafahamu kitu chochote kabisa ??? Lakini, kubwa zaidi ni hili la wanafunzi 600 kuanza pamoja, lakini wanaofaulu ni watu 30, huku nusu ingine ikiwa inafanya SUPPLEMENTARY au DISCONTINUED. Sijui kwanini hili haliwastui Majaji na Wizara. Watu hufeli, lakini siyo kwa kiwango hicho ambacho kinafanyika pale Law School.

Pia, pale pana rushwa sana ya ngono, kukomoana na kubadilishiana matokeo. Kuna jamaa niliwahi kuwa naye mahakamani aliwahi niambia kwamba kuna rafiki zake wanafundisha pale walimuahidi kwamba watamfaulisha, na kweli alifauri vizuri hadi tukashangaa. Alikuwa na maswali hata kabla mitihani haijaanza. Nikasema HIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII...

Credit: Malcom Lumumba
 
Nimeona mada za kuchambua taarifa ya kufeli kwa wanafunzi Law School of Tanzania.

Binafsi na mimi nimepitia Law School, na haya ndiyo ninayoyafahamu kuhusiana na hiki chuo.

1. Law School kiuhalisia, siyo sehemu ya mafunzo kwa vitendo kama mnavyosikia redioni.

2. Somo la field lipo, ila marks zake hazihusiki kwenye kubaini ufaulu. Yaani alama za somo la field hazina maana kwenye GPA calculation maana hazitambuliki.

3. Wanafunzi wa Law School hufundishwa kwa nadharia darasani, na kuingia semina kama ilivyo vyuo vikuu.

4. Mwalimu mmoja hutoa mhadhara kwa wanafunzi wote 600+ na akimaliza anaingia mwingine hadi siku inaisha.

5. Mada zinazofundishwa Law School ni zilezile mwanafunzi alifundishwa vyuoni ngazi ya degree na hakuna tofauti.

6. Muda wa mitihani haupo fair. Kwenye mtihani mmoja, kunakuwa na maswali ya kuandaa hati za mashtaka na madai nyingi mno kiasi kwamba muda wa kuandaa hati hizo hautoshi. Kwa wasijua, hati za kisheria uandaaji wake unahitaji kurejea vifungu vya sheria mbalimbali ambazo unakuwa unazo mezani(Acts).

7. Wahadhiri wa Law School huamini kwamba wanafunzi wao watafeli na mtu akifaulu wanashangaa sana. Yaani wapo kama miungu watu. Pale Law School hata secretary anamdharau mwanafunzi na anataka umuinamie kumsujudu.

8. Mahakimu, na waajiriwa wengine wenye uzoefu kwenye sheria wakienda kujiendeleza Law School nao hufeli pia.

9. Kuna wakati mahakimu walishauriwa wasijiendeleze Law School maana ni fedhea hakimu mzoefu unafeli Law School. Badala yake waliaambiwa watapewa utambulisho maalum kwamba wamefuzu vigezo vya sheria kwa vitendo.

10. Suplementary yaani mitihani ya kurudia haina kikomo Law School. Unaweza hata ukakaa na sup. hata miaka 40.

11. Law School ukikata rufaa ya matokeo haipatiwi majibu na unaweza ukaanza apya kusoma na kumaliza bila kupata majibu ya rufaa.

12. Law School unasoma masomo yote uliyofundishwa kwenye shahada ya sheria kwa miaka minne, lakini ukifika Law School unafundishwa kwa miezi 6 na unapewa mitihani. Halafu miezi mingine 6 unaenda field.
 
Sasa kama Lawyers ndio wana lalamika hivi JF, blogs, Fb , Instagram, nk je sisi tusio Wanasheria? Hawa Lawyers wa Tz wame lala. HESLB ili kuwa ina watoza penati za hovyo kinyume na mikataba ya 1995 to 2015, hakuna aliye fungua shauri kupinga, wali lipa wote; Mwigulu ali leta tozo nyingi zinazo kiuka utu, na kunyonya raia na watumishi wapo kimya! JPM alikuwa ana kiuka Katiba hadharani, wako kimya! DED na DCs wana simamia Chaguzi akati ni CCM agents wapo kimya; Sasa hivi wame feli badala wajaribu ku challenge LEGALITY kupitia TLS, Mahakama za Tz au Mahakama ya East Africa, ila nao wako fb, JF, fb, blogs wana lalamika utadhani wawekezaji wa QNET, Kalynda E-Commerce. Sisi tuwasaidie nini? Hii ina onesha bado mmelala tofauti na Wenzenu wa Kenya. Ina bidi mfanyiwe hivyo ili muamke usingizini.
 
Nimekusoma naona umejigeuza msemaji wa hao walimu wa Law School, sijui kama wamekupa hiyo ruhusa, au umejitwalia kwa nguvu toka kwao.

Naona unataka kutumbia mwalimu hapo Law School akitaka rushwa ya ngono, au akimpa mwanafunzi maksi kwa sababu ya kujuana, lazima kwanza aje kukwambia wewe.
 
Hii nchi siasa zinaiharibu mno.

Tunapenda sana kufurahishana.

Na kwakua wanasiasa wanapenda sifa.

Basi wataiharibu hiyo shule.
 
Nimekusoma naona umejigeuza msemaji wa hao walimu wa Law School, sijui kama wamekupa hiyo ruhusa, au umejitwalia kwa nguvu toka kwao.

Naona unataka kutumbia mwalimu hapo Law School akitaka rushwa ya ngono, au akimpa mwanafunzi maksi kwa sababu ya kujuana, lazima kwanza aje kukwambia wewe.
Rushwa ya Ngono ni O.0000001 ya Rushwa Tz. Na ile ni watu wazima. Ww wa kiume, rushwa ya ngono ya binti ina kuhusu nn? Faulu wewe kama wewe.
Pia Ripoti ya TAKUKURU ya hali ya Rushwa nchini iliyo online.
1. Polisi
2. Sekta ya Afya
3. Mahakama. Hapa tena Mahakimu na Lawyers mko tena top 3. Rushwa ni jadi yenu.

4. TRA.
Yaani mna lalamika kama wawekezaji wa QNET akati mnajua Legal Procedures? Why Can't you all challenge the Examination Methodology? Tuna hitaji kuona mkichallenge hata hao Walimu wenu, Serikali, Vyuo, Mahakama, HESLB, Wizara ya Fedha, EUROPEAN UNION, Taasisi mbalimbali, nk.
 
Swala la watu kupewa degree za mchongo za ngono hiyo sikupingi hipo tu

Lakini siungi mkono uhuni kutoka hiyo shule ya sheria .

Kuhusu vyuo kuzalisha vilaza hilo nikweli Sana Sana Udsm na SUA na Udom , bila kusahau Mzumbe

Mfano Mtu Kama GENTAMYCIME Popoma ndo lecture wa SAUTI hapo mnategemea mwanafunzi kuwa competent
 
Kinachofanya mnafeli ni kuwa hamjui kingereza so jifunzeni kingereza hapo anatafutwa mchawi tu ..au muombe siku ya mtihani muingie na dictionary la sivyo mtalalamika Hadi Kesho

Mkubari ukweli kuwa kingereza kinawapa shida.
 
Swala la watu kupewa degree za mchongo za ngono hiyo sikupingi hipo tu

Lakini siungi mkono uhuni kutoka hiyo shule ya sheria .

Kuhusu vyuo kuzalisha vilaza hilo nikweli Sana Sana Udsm na SUA na Udom , bila kusahau Mzumbe

Mfano Mtu Kama GENTAMYCIME Popoma ndo lecture wa SAUTI hapo mnategemea mwanafunzi kuwa competent
mkuu Genta akiiona hii comment yako itajibiwa kwa lugha ngumu.
 
Sasa kama Lawyers ndio wana lalamika hivi JF, blogs, Fb , Instagram, nk je sisi tusio Wanasheria? Hawa Lawyers wa Tz wame lala. HESLB ili kuwa ina watoza penati za hovyo kinyume na mikataba ya 1995 to 2015, hakuna aliye fungua shauri kupinga, wali lipa wote; Mwigulu ali leta tozo nyingi zinazo kiuka utu, na kunyonya raia na watumishi wapo kimya! JPM alikuwa ana kiuka Katiba hadharani, wako kimya! DED na DCs wana simamia Chaguzi akati ni CCM agents wapo kimya; Sasa hivi wame feli badala wajaribu ku challenge LEGALITY kupitia TLS, Mahakama za Tz au Mahakama ya East Africa, ila nao wako fb, JF, fb, blogs wana lalamika utadhani wawekezaji wa QNET, Kalynda E-Commerce. Sisi tuwasaidie nini? Hii ina onesha bado mmelala tofauti na Wenzenu wa Kenya. Ina bidi mfanyiwe hivyo ili muamke usingizini.
Nyie wanasheria someni vzr acheni kulalamika. Law School wako vzr sana. Sisi tuliopia pale tunajua umahiri wa wahadhiri wa pale Law School. tatizo wanafunzi wakitoka vyuoni wanajiona wamemaliza kila kitu. someni tuendelee kupata wanasheria mahiri.
 
Waajiriwa wote huwa hawana mda WA kusoma ...Wengi hununua vyeti....vyuo vyote huo ndo utamaduni
 
Rushwa ya Ngono ni O.0000001 ya Rushwa Tz. Na ile ni watu wazima. Ww wa kiume, rushwa ya ngono ya binti ina kuhusu nn? Faulu wewe kama wewe.
Pia Ripoti ya TAKUKURU ya hali ya Rushwa nchini iliyo online.
1. Polisi
2. Sekta ya Afya
3. Mahakama. Hapa tena Mahakimu na Lawyers mko tena top 3. Rushwa ni jadi yenu.

4. TRA.
Yaani mna lalamika kama wawekezaji wa QNET akati mnajua Legal Procedures? Why Can't you all challenge the Examination Methodology? Tuna hitaji kuona mkichallenge hata hao Walimu wenu, Serikali, Vyuo, Mahakama, HESLB, Wizara ya Fedha, EUROPEAN UNION, Taasisi mbalimbali, nk.
Kwa hiyo nikiwa wa kiume nikaona binti ananyanyaswa kwa kutumia maumbile yake ninyamaze, ili nae, akiona siku nyingine nanyanyaswa kwa namna tofauti anyamaze pia! sijui kwa huu ujinga wenu mnataka tutengeneze taifa la aina gani.

Nakushangaa zaidi unapokiri Lawyers na mahakimu wapo kwenye top three ya rushwa Tz, lakini hutaki tulaani hayo matendo!. na sioni ni kwa vipi kulaani hayo matendo huku mitandaoni kwako kusiwe aina ya challenge.
 
huwa ukiwauliza wanasema niko chuo fulani nachukua sheria...huwa sielewi wanamaanisha nini.

lakini wengine utasikia nasomea udaktari, nasomea uhasibu, nasoma engineering etc
 
Compare this with other professional accreditation eg ACCA, CPA, CSA etc. Watu wengi don't pass their professional exams although they may have good academic results. Tuwe realistic, this is another ball game aimed at setting quality and standards.
 
Kwa hiyo nikiwa wa kiume nikaona binti ananyanyaswa kwa kutumia maumbile yake ninyamaze, ili nae, akiona siku nyingine nanyanyaswa kwa namna tofauti anyamaze pia! sijui kwa huu ujinga wenu mnataka tutengeneze taifa la aina gani.

Nakushangaa zaidi unapokiri Lawyers na mahakimu wapo kwenye top three ya rushwa Tz, lakini hutaki tulaani hayo matendo!. na sioni ni kwa vipi kulaani hayo matendo huku mitandaoni kwako kusiwe aina ya challenge.
Mbona huja enda Mahakamani kufungua kesi kupinga Tozo, au kupinga wizi wa Kura 2020, au kupinga wizi wa data bundles mitandao ya simu, au Retention fee, penalties na interest za HESLB.

Rushwa ya ngono haija kuathiri ww, na ni makubaliano yao...wale ni watu wazima, wivu wako tu eti Lecturer ana faidi uache kusoma vzr kisa kiherehere. Hicho kili kupeleka chuo? Unajua huyo demu ame gongwa na wangapi kitaa? Ww soma. Uanaharakati, peleka huko NGOs.

Rushwa Mahakamani/Lawyers mko no. 3 Tanzania. Una semaje kuhusu hili? Mbona hulalamiki kuwa mna kula sana Rushwa?
 
Najua mtabisha lakini Ukweli utabaki Ukweli.Utaratibu wa kufundisha Kutunga Mitihani kufanya Mitihani kusahihisha Mitihani na kisha Zoezi hilo Huchunguzwa na kuhakikiwa na Bodi kama kuna Dosari na Upendeleo uliofanywa Bodi ikijiridhisha MATOKEO HUTANGAZWA. Utaratibu huo ni Tofauti kabisa na Vyuo vingine.

Vyuoni Mwalimu mmoja ana uwezo wa KUKUFAULISHA. Naipongeza BODI Uongozi na Watendaji wa LAW SCHOOL kwa kusimamia Weledi.

TATIZO la Wanafunzi kufeli linachangiwa na
1. Lugha ya KIINGEREZA ni Tatizo kubwa sana kwa Wanafunzi
2. Vyuo walikotoka hawakuandaliwa ipasavyo
3. Rushwa ya Fedha na Ngono kwa Wanafunzi wengi ili WAFAULU.
4. Kununua Mitihani
LAW SCHOOL hakuna UJINGA HUO pale ni KUSOMA TU

Naipongeza BODI Uongozi na Watendaji ni Bora kupata Wanafunzi Wachache Waliofanya Vizuri kuliko Wengi waliofeli kwa Ajili tu ya kutaka kuwa na IDADI KUBWA ya Waliofaulu

LAW SCHOOL IPO kwa Ajili ya KUWAANDAA WANASHERIA WALIOELIMIKA KISHERIA TANZANIA sio Kichaka cha Wanasheria MAKANJANJA.

Sasa hivi Wanafunzi wengi wa Vyuo vingi ukiangalia VYETI vyao Wana UFAULU wa KUTISHA Lakini HAWAELEWI KITU wengi wana DEGREE za MAGUMASHI.

LAW SCHOOL imekataa UHUNI huo

Kwamba Law School ndiko hawapokei rushwa za ngono na pesa tofauti na vyuo vingine vyote? Kwa weledi upi huo wa LST?

Ama haya si ni kuvitukana vyuo vingine vyote? Hii si ndiyo ile ya mtuhumiwa anapo taka kumgeuzia kibao hakimu?

Hivi aliyeanza kutuhumiwa hapa ni nani? Jibuni hoja ndugu:

Law School kufumbia macho tuhuma zinazowakabili haikubaliki

Au hadi mkute makufuli chuoni yameongezeka?
 
Back
Top Bottom