Kufanya mapenzi kinyume na maumbile | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufanya mapenzi kinyume na maumbile

Discussion in 'JF Doctor' started by jamii01, Jan 23, 2011.

 1. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Watu wengi wanajikuta ni waathirika wa mchezo wa kudandia ukuta kwa sababu kadhaa. Mosi ni stori za vijiweni, kwamba wanaume wanadanganyika mno na habari za kusikia kwa wengine.

  Wapo wanaoingia huko kwa sababu ya kulazimishwa na wapenzi au waume zao. Kuna wanawake wanaoamua kujitoa mhanga kwa ajili ya kutibu shida za maisha. Pia lipo kundi linaloamini kwamba kwa kuwaruhusu wanaume wao kuwadandia ukuta, watawafanya wawapende zaidi.

  Yapo maneno ya kuwa tendo likitekelezwa taratibu, pia matumizi ya mafuta yanaweza kuleta usalama. Mtandao wa womenanswers.org

  Unalizungumzia hilo lakini unachambua kwa upana kwamba mlango husika unaunga kwenye uti wa mgongo, hivyo ni lazima ulindwe kwa sababu ukiharibiwa husababisha ulemavu wa maisha.

  Unaeleza kuwa mlango huo haupo kwa ajili ya kupitisha kitu kutoka nje, hivyo ukitumiwa ndivyo sivyo ni rahisi kuchanika, kumsababishia maumivu makali mhusika pamoja na kuvuja damu.

  Yapo pia maneno kwamba ni rahisi mwanaume kufika mwisho anapopita mlango huo kwa sababu ni mdogo na unabana. Hayo yanaibua upofu wa kuona ukweli kuwa mwisho wa tendo ni sawa na kumsababishia ulemavu mtendwa.

  "Mimi ni mke wa mtu, naomba unihifadhi jina. Mume wangu alidhani sifa kuniingilia kinyume na maumbile lakini nilipata usumbufu mkubwa wakati wa kuzaa. Niliambulia matusi kutoka kwa manesi kwani nilishindwa kumsukuma mtoto, hii yote ni kwa sababu ya mchezo huo".

  Nikifafanua SMS ya Mama X ni kuwa athari nyingine ya mapenzi ya kudandia ukuta ni wakati wa kuzaa. Kitaalamu mwanamke anayefungua mlango wa nyuma, inapofika wakati kumsukuma mtoto nao hufunguka na kukaa wazi, hivyo kumsababishia usumbufu mzazi na kuchoka haraka.

  Kwa hali hiyo, mtoto hushindwa kutoka kwa urahisi kwenye njia yake kwa sababu mzazi hushindwa kumsukuma inavyotakiwa. Hilo linapotokea, wakunga huwa wakali dhidi ya wazazi na matokeo yake kwa wale wasio na staha ni kuwatolea lugha chafu.

  Kuna simulizi kutoka Zanzibar kuwa mabinti wadogo huingia katika mchezo wa kuruhusu wageni kwa mlango wa nyuma ili kulinda bikira zao, kwamba heshima yao kwenye ndoa ni kukutwa ukiwa mwali. Wajuzi wa mambo wanasema ‘katabia' hako Zenji kamekolea kweli kweli.

  Yapo mafundisho ya kidini, ipo mifano ya Sodoma na Gomora ndani ya vitabu vya dini. Hii ina maana kuwa yeyote ambaye anajihusisha na mchezo huo, hafanyi kile kinachompendeza Mungu wake.

  ATHARI YA KUDANDIA UKUTA KIAFYA
  Pointi kuu ni kwamba watu wanaokimbilia mlango huo wako kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa kwa sababu kitaalamu, njia hiyo ni rahisi kupitisha Virusi Vya Ukimwi (VVU).

  Inaeleweka kwamba, mwanamke hawezi kupata ujauzito kwenye njia hiyo, lakini nyongeza ya kitaalamu ni kuwa mlango wa nyuma kwa kawaida huwa una wadudu wenye maradhi (bacteria) ambao humshambulia mwanaume anayepita huko.

  Hii ina maana kuwa tendo hilo hata kama litafanywa kwa kondomu, bado athari yake ni kubwa, bakteria ni wengi eneo hilo kwa ajili ya kulinda mlango husika. Hii ina maana kuwa hata kama nyote wawili mmepimwa na mmegundulika mpo salama lakini wadudu wa maradhi siku zote wapo kwenye njia hiyo.

  Mapenzi ya kudandia ukuta, pia hutoa athari kwa mwanaume katika mfumo wa mkojo. Hii ni kwamba kuna urahisi wa kuingiliwa na chembechembe hatari na tatizo likiwa kubwa kumsabishia mhusika kwenda haja ndogo kwa kutumia mipira.

  Ushauri ni kwamba mlango huo haupo kwa ajili ya mapenzi, hivyo kwa mwanamke ni mateso kuliko raha, pia kuchanika kwa urahisi kwa sababu njia hiyo haitanuki kama ilivyo kwa barabara ya kawaida (mlango wa kawaida).

  Utafiti uliofanywa na mtandao wa womenask.com unaweka wazi ripoti yake kwamba mtu aliyezoea mchezo wa kupitisha mgeni kwa mlango wa nyuma, baadaye huathirika mno na hulazimika kuvaa nepi. Hii ni kwa sababu misuli yake hulegea, hivyo kushindwa kudhibiti haja.

  Mtandao huo unashauri pia kwamba ikiwa mwanaume atapita mlango wa nyuma, hatakiwi kurudi mbele kwa sababu kwa kufanya hivyo,

  Anaweza kumuambukiza mwenzake wadudu wa maradhi ambao wameelezwa hapo juu kwamba wanapatikana kwenye mlango wa nyuma.
  :A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2:
   
 2. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,738
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Huu mtandao haujafafanua vizuri kuhusu "kinyume na maumbile"
  Je wanamaanisha tigo tu ndio kinyume cha maumbile? kwenda chumvini je? kulamba koni je?

  Pagumu hapo....
   
 3. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hii tabia ni laana
   
 4. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2015
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,326
  Likes Received: 2,325
  Trophy Points: 280
  Wabongo imekuwa topic maswala ya kinyume na maumbile.Sasa najiuliza nini sababu jamani maana hata humu mmu kumetawala topic hizo? Wabongo nini kimetukuta? Au wengi walikuwa wanafanya ila imekuwa siri yao na baada ya kuona inchi mbali mbali zikilegalize hili jambo nao wamejitokeza
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Jul 9, 2015
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Hiyo obsession na hayo mambo ni dirisha la taswira ya jinsi gani hayo mambo yalivyoenea katika jamii.
   
 6. kabanga

  kabanga JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2015
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 29,803
  Likes Received: 3,702
  Trophy Points: 280
  inashangaza sana.....
   
 7. Konda wa bodaboda

  Konda wa bodaboda JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2015
  Joined: Jul 18, 2014
  Messages: 8,080
  Likes Received: 3,211
  Trophy Points: 280
  Ushauri wa kiimani unakataa, na wa kisayansi pia unakataa, hii ni dalili ya maangamizi yanayomnyemelea mwanadamu siku za karibuni.
  Hii ni zaidi ya laana.
   
 8. L

  Larusai Mux JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2015
  Joined: Oct 24, 2012
  Messages: 978
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Mbona munaijadili haya maovu kuliko mema?,,
   
 9. Gide MK

  Gide MK JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2015
  Joined: Oct 21, 2013
  Messages: 4,718
  Likes Received: 3,384
  Trophy Points: 280
  Ukijidai wewe kidume cha mbegu kufuatilia vya watu lazima utatuliwe marinda maana hakuna namna nyingine
   
Loading...