Kufanya kazi na dissapora ni balaa

MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,861
6,230
Heshima kwenu wadau,

Yaani afadhali imefika ijumaa maana nipo hoi, hapa kibaruani kampuni ina utaratibu wa kuajiri sana jamaa walioamua kurudi nyumbani baada ya kufanya sana kazi huko dunia ya kwanza, as company ina amini hawa jamaa wachapakazi na hawana longo longo as maisha ya ulaya na america yamewafundisha kuwajibika.

Dah basi kwenye department yangu juzi kati tukapata senior manager dissapora aliyepigika sana texas huko amekuja na strategies zake balaa, targets kibao yaani full presha,

Jamani kama upo jamvini huko jua hii tabia hatuitaki sisi ni watanzania and no hurry in tanzania si tumeshazoea kufanya kazi huku tunasindikiza na castle light baridiii... Msituletee maisha yenu ya kubeba maboksi kwenye nchi yetu ya longo longo kama vipi mbaki huko huko ughaibuni... Si tushazoea leo naumwa, kesho msiba wa jirani, kesho kutwa naozesha so ninaandaa send of kitu wekend imefika,

Nchi yetu tumeshaizoea mafao yenyewe hadi ufike miaka 55 wakati life expectancy miaka 40,

Yaani nashindwa hata kupata chance ya kufukuzia dili zangu, alaaniwe huyu dissapora
 
We utakuwa unafanyia kazi vodacom maana mi diaspora kibao huko.
Vumilia tu mkuu,usichezee kazi chezea mshahara.
 
Pole aisee ndo advantage tuliyopata mwenyewe nimerudi hivi karibuni na nimeona culture ya bongo makazini ni finyu sana so nimejaribu kurekebisha eti wananimaindi na nimesikia wengine wanataka kuniendea kwa waganga.. Sio hivyo ukiwa kazini inabidi kuchapa kazi kua serious na kazi na mchezo kazini usiwepo.. Sawa kuna wakati wa kucheka na utani bt performance iwepo pia. Mtu kazi inaanza saa mbili anaingia ofsini saa tatu na nusu.. No no nooo!!!
 
Heshima kwenu wadau,

Yaani afadhali imefika ijumaa maana nipo hoi, hapa kibaruani kampuni ina utaratibu wa kuajiri sana jamaa walioamua kurudi nyumbani baada ya kufanya sana kazi huko dunia ya kwanza, as company ina amini hawa jamaa wachapakazi na hawana longo longo as maisha ya ulaya na america yamewafundisha kuwajibika.

Dah basi kwenye department yangu juzi kati tukapata senior manager dissapora aliyepigika sana texas huko amekuja na strategies zake balaa, targets kibao yaani full presha,

Jamani kama upo jamvini huko jua hii tabia hatuitaki sisi ni watanzania and no hurry in tanzania si tumeshazoea kufanya kazi huku tunasindikiza na castle light baridiii... Msituletee maisha yenu ya kubeba maboksi kwenye nchi yetu ya longo longo kama vipi mbaki huko huko ughaibuni... Si tushazoea leo naumwa, kesho msiba wa jirani, kesho kutwa naozesha so ninaandaa send of kitu wekend imefika,

Nchi yetu tumeshaizoea mafao yenyewe hadi ufike miaka 55 wakati life expectancy miaka 40,

Yaani nashindwa hata kupata chance ya kufukuzia dili zangu, alaaniwe huyu dissapora
hapo kwenye red pameniacha hoi, mecheka mpaka watu wananishangaaa lol,
 
Back
Top Bottom