Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Kwenye jamii yetu kuna watu wenye mahitaji maalum ikiwemo walemavu, Watoto mayatima, waliotelekezwa n.k ambapo watu hawa hawawezi kujinusuru wenyewe mpaka wasaidiwe.
Kwa sasa watu hawa huomba omba mtaani wakitegemea kupewa 200 kotoka kwa raia wachache wenye huruma, wengine wakiomba wakikosa huamua kugeuaka kuwa wezi.
Badala ya kuacha hali hii iwe itakavyokuwa, Ni muhimu tuweke Tozo angalau ya Tsh. 20 kwa Kila chupa ya maji ya kunywa, Fedha itakayopatika itumike kujenga safe house ambazo zina kila huduma (bure) kwa ajili ya makundi haya maalum huku wakifundishwa fani mbalimbali, wanaoweza kujitegemea wanaachwa wanaanza kujitegemea, wanaoshindwa wanalelewa hadi mwisho wa Maisha yao.
Watu hawa hawajapenda kuwa walemavu n.k hivyo ni sahihi na ubinadamu kutumia kodi ya raia wazima kusaidia wenye uhitaji maalum. Hili ni jambo muhimu kiuchumi, Kijamii, Kiusalama na ki ubinadamu. Tunganeni kupigania jambo hili kwa kuwa ni muhumu kwa Taifa na ustawi wa mwanadamu.