Kuendelea kumtaja Hayati Magufuli kwa mabaya ni upuuzi wa ajabu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Anaandika, Robert Heriel

Sikuwa mshabiki wa Magufuli Kutokana na namna alivyokuwa anaongoza, sisemi Kuwa Magufuli hakuwa na mambo Mema aliyoyafanya, yapo mengi mazuri Sana hasa ya miundombinu, lakini pia yapo Mabaya ambayo aidha aliyafanya au kuyafumbia macho, ambayo ndio yalinifanya nimuone kama kiongozi asiyefaa.

Ninashangazwa na kile kinachoendelea hasa Kwa upande wa Upinzani kuendelea kumtaja taja MTU ambaye tayari anasiku nyingi ameshafariki.

Wabaya Waliohai wapo wengi, Kwa nini mhangaike na Watu waliokwisha Kufa wasio na chochote cha kuchangia katika Ulimwengu wa Waliohai? Wema Waliohai pia wapo wengi.

Hatuwezi kuongoza nchi Kwa kuangalia Wafu, na hatutataka nchi yetu iongozwe na watu wenye mawazo na Matendo ya Wafu.

Tunahitaji viongozi ambao wanaongoza nchi Kwa kuangalia Maisha ya kizazi kijacho kitaishije,
Nchi inaongozwa Kwa mahitaji yajayo sio mahitaji yaliyopita. Nchi inaongozwa Kwa maslahi ya Watu wa kesho sio Kwa maslahi ya Watu wa Jana na juzi waliokwisha Kufa.

Wanaoishi Wasiwe watumwa wa Wafu, Watu waliokwisha Kufa. Hivyo ndivyo taifa hili linapaswa kujengwa na kuongozwa. Kwa sababu tunaenda Mbele na sio Nyuma.

Sijui Fulani alikuwa Nani akasema nini, hiyo haina maana yoyote Kwa wakati au kizazi kijacho, kitakachoangaliwa ni manufaa ya kizazi kijacho.

Hata Mungu tunayemuabudu ni MUNGU aliyehai na Mungu wa Waliohai sio Mungu wa Wafu.

Wanasiasa mnaomtaja taja Magufuli Kwa ubaya mnayohaja ya kujitafakari, kama mnaagenda zenu za Siri Sawa lakini eleweni kuwa haitasaidia Jambo LOLOTE lile.

Acha nipumzike SASA.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Makanya, Same, Kilimanjaro.
 
KUENDELEA KUMTAJA MAGUFULI KWA MABAYA NI UPUUZI WA AJABU.

Anaandika, Robert Heriel

Sikuwa mshabiki wa Magufuli Kutokana na namna alivyokuwa anaongoza, sisemi Kuwa Magufuli hakuwa na mambo Mema aliyoyafanya, yapo mengi mazuri Sana hasa ya miundombinu, lakini pia yapo Mabaya ambayo aidha aliyafanya au kuyafumbia macho, ambayo ndio yalinifanya nimuone kama kiongozi asiyefaa.

Ninashangazwa na kile kinachoendelea hasa Kwa upande wa Upinzani kuendelea kumtaja taja MTU ambaye tayari anasiku nyingi ameshafariki,

Wabaya Waliohai wapo wengi, Kwa nini mhangaike na Watu waliokwisha Kufa wasio na chochote cha kuchangia katika Ulimwengu wa Waliohai?
Wema Waliohai pia wapo wengi,

Hatuwezi kuongoza nchi Kwa kuangalia Wafu, na hatutataka nchi yetu iongozwe na watu wenye mawazo na Matendo ya Wafu.
Tunahitaji viongozi ambao wanaongoza nchi Kwa kuangalia Maisha ya kizazi kijacho kitaishije,
Nchi inaongozwa Kwa mahitaji yajayo sio mahitaji yaliyopita,
Nchi inaongozwa Kwa maslahi ya Watu wa kesho sio Kwa maslahi ya Watu wa Jana na juzi waliokwisha Kufa.

Wanaoishi Wasiwe watumwa wa Wafu, Watu waliokwisha Kufa. Hivyo ndivyo taifa hili linapaswa kujengwa na kuongozwa.
Kwa sababu tunaenda Mbele na sio Nyuma.

Sijui Fulani alikuwa Nani akasema nini, hiyo haina maana yoyote Kwa wakati au kizazi kijacho, kitakachoangaliwa ni manufaa ya kizazi kijacho.

Hata Mungu tunayemuabudu ni MUNGU aliyehai na Mungu wa Waliohai sio Mungu wa Wafu.

Wanasiasa mnaomtaja taja Magufuli Kwa ubaya mnayohaja ya kujitafakari, kama mnaagenda zenu za Siri Sawa lakini eleweni kuwa haitasaidia Jambo LOLOTE lile.

Acha nipumzike SASA.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Makanya, Same, Kilimanjaro
 
KUENDELEA KUMTAJA MAGUFULI KWA MABAYA NI UPUUZI WA AJABU.

Anaandika, Robert Heriel

Sikuwa mshabiki wa Magufuli Kutokana na namna alivyokuwa anaongoza, sisemi Kuwa Magufuli hakuwa na mambo Mema aliyoyafanya, yapo mengi mazuri Sana hasa ya miundombinu, lakini pia yapo Mabaya ambayo aidha aliyafanya au kuyafumbia macho, ambayo ndio yalinifanya nimuone kama kiongozi asiyefaa.

Wabaya wapo wengi kwani ni marais. Unaongeleaje kwa wale wanaozungumzia hayo usemayo mazuri yake, hao wanazungumzia ya mtu aliye hai?
 
Wewe endelea na makala za kuelimisha vijana na mahusiano upo vizuri, huku tuache wenyewe huna upako huo.

Magufuli tutaendelea kumsema Kwa maovu aliyowatendea Watanzania tangu kuumbwa Kwa ulimwengu huu, udikteta na utawala wa mkono wa chuma tulikuwa tunausikia tu Kwa wenzetu na kusoma kwenye historia, lakini yule Mrundi wa Chato akaja kutuonesha dhahiri.

Hadithi kama hii usithubutu kwenda kuiogea kwenye familia ya Ben Saanane utakimbizwa na mashoka.

Hebu tuache, huyu tunaye liwe fundisho Kwa waovu wote kwamba ukiishi Kwa Ubaya utasemwa daima Kwa Mabaya yako na mema yako tutayasahau.

Imagine Profesa mzima Kabudi leo anatuambia eti yeye na Magufuli walitudanganya kuhusu pesa za Makinikia halafu unataka tukae kimya?
 
Wabaya wapo wengi kwani ni marais. Unaongeleaje kwa wale wanaozungumzia hayo usemayo mazuri yake, hao wanazungumzia ya mtu aliye hai?

Kwani hakuna Marais wabaya Waliohai?
Kama lengo ni kutafutana ubaya, hatuwezi kosa ubaya WA yeyote.
Lakini kutafuta ubaya wa Wafu ni dalili ya ucheshi wa mwendawazimu.
Hakunaga Hukumu ya Wafu, wanaohukumiwa ni Waliohai.

Hata hivyo kuna Ile hasira ya wahanga ambayo MTU akifa humsema kutuliza hasira na chuki zao. Lakini kumchukia Na kuwa na hasira ya Marehemu Kwa zaidi ya miaka ni Jambo la kipuuzi hasa ukijua amekufa na hatorudi
 
Kama shetani anatajwa na dini zote kwanini Magufuli asitajwe kwa aliyo yatenda.? Mwinyi alisema maisha ya mwanadamu ni hadithi tu. Magufuli kosa lake alijiona Mungu mtu na ni yeye pekee ndiye mwadilifu na wengine wote ni wezi tu.

Shetani ndio Uovu wenyewe,lakini binadamu hata awe muovu kiaje hakosi jema moja.

Tofautisha Shetani na binadamu.
 
Kwani hakuna Marais wabaya Waliohai?
Kama lengo ni kutafutana ubaya, hatuwezi kosa ubaya WA yeyote.
Lakini kutafuta ubaya wa Wafu ni dalili ya ucheshi wa mwendawazimu.
Hakunaga Hukumu ya Wafu, wanaohukumiwa ni Waliohai.

Hata hivyo kuna Ile hasira ya wahanga ambayo MTU akifa humsema kutuliza hasira na chuki zao. Lakini kumchukia Na kuwa na hasira ya Marehemu Kwa zaidi ya miaka ni Jambo la kipuuzi hasa ukijua amekufa na hatorudi
Ukitaka kumsifia unaruhusiwa, na kama unamtetea mtetee kimpango wako. Hao marais wabaya walioko hai waongelee ww. Sisi tuko na dhalimu Magufuli fullstop.
 
Back
Top Bottom