Kuelekea Uchaguzi Mkuu: Sekta ya Elimu haijapata fursa ya kujadili changamoto zao au imetengwa?

sopinta

Member
May 28, 2020
46
93
Wadau wa Sekta ya Elimu mnakwama wapi? Tokea Serikali ya awamu ya tano imeingia madarakani Novemba 15 , 2015 , kumekuwepo na mikutano mbalimbali juu ya kujadiliana changamoto mbalimbali katika sekta husika nakumbuka mapaema tu baada ya serikali iliyopo sasa kuanza kazi , kuliitishwa mkutano mkubwa wa wafanyabiashara mbalimbali juu ya kujadiliana changamoto zinazojitokeza katika sekta nzima ya biashara kama vile utitiri wa kodi , utaratibu wa utoaji mizigo bandarini , changamoto ktk utoaji na uingizaji mizigo bandarini , yote haya yalijadiliwa kwa kina na kukapatikana suluhisho mbalimbali .

Katika awamu hii hii , kuliitishwa mkutano mkubwa juu ya kujadiliana ktk changamoto za sekta ya madini , wafanyabiashara mbalimbali ktk sekta hii walitoa changamoto zao mbalimbali kuanzia wachimbaji wadogo , blockers wa madini, dealers wa madini , wamiliki wa leseni za madini kuanzia leseni ndogo mpaka kubwa na katika kikao hiki ndio kuliibuka kwa kuonekana kwa sheria mbovu za madini , kanuni kubadilishwa pamoja na kujengwa ukuta wa Mererani.
Swali la kujiuliza wadau sekta ya elimu mmekwama wapi au ndio hamna tija ktk taifa?

Serikali imeweza kuwaita Ikulu mabalozi mbalimbali na kuwaeleza juu ya mustakabali wa taifa kuhamia Dodoma , pamoja na mambo mengine mabalozi hawa walipata fursa ya kupewa hati ya viwanja. Je sekta ya Elimu imekwama wapi na changamoto zao?

Viongozi wa kiroho (Dini) hawa ndio wamepata fursa nyingi sana ya kuitwa Ikulu na kujadili changamoto zao katika swala zima la kidini , viongozi hawa wa dini wameenda Ikulu na kujadili changamoto mbalimbali juu ya maswala ya kiroho ndani ya taifa. Nahisi hata wadau wa sekta ya elimu wanahitaji fursa kama za viongozi wa kiroho kutoa yao ya moyoni , Mkulu wakumbuke hawa kabla ya filimbi haijapigwa.

Katika sekta ya michezo , hawa nao walipata zaidi ya mara mbili kwenda ikulu kujadiliana na mkulu na kupewa motisha kubwa ya pesa na aseti ya viwanja hii iliwatia moyo wachezaji katika kuinua soka la Tanzania , nafikiri hata hawa wadau wa sekta ya Elimu wanahitaji kujadili changamoto zao , serikali wakumbukeni wadau wa sekta hii.

Sekta ya kilimo nao wamepata fursa zao na kusema juu ya kilimo cha korosho , ufuta , mahindi changamoto katika bei , masoko , kodi vyote hivyo vilijadiliwa katika mkutano maalum ulioitishwa na mamlaka husika , wadau wa sekta ya elimu vipi nyie hamna changamoto zenu ndani ya miaka hii mitano?

Tukumbuke tu sekta ya elimu ndio chimbuko la kila kitu , hata viongozi wa juu kabisa wanatoka sekta ya elimu , hivyo na wao wanachangamoto zao , sekta ya elimu ni kubwa sana kama tunavyoiona .

Hata katika familia zetu Baba anaponunua kila kitu ndani kwa ajili ya familia na kutoa hela ya ziada , hii haimaanishi kuwa familia hiyo haina changamoto , pamoja na kununua chakula na kutimiza mahitaji mengine , bado familia inahitaji majadiliano kwa ajili ya kuweka sawa kinachojitokeza.

Nimalizie kwa kusema wadau wa Sekta ya elimu nao wanayao ya kujadiliana kama sekta nyingine.
 
Walishaongea na makonda,ndio maana wakaanza kupnda bure magari huko Dar es salaam. Nahisi walituwakilisha sisi wamikoani!
 
Back
Top Bottom