Nyamemba
JF-Expert Member
- Nov 3, 2011
- 845
- 446
TAMBUA MIPANGO KABAMBE KATIKA KUELEKEA UCHAGUZI WA OCTOBER 2020
GACHUMA APANGA SAFU YA VIONGOZI MARA
Ndugu wana ccm wenzangu naomba kuleta kwenu taarifa ya masikitiko iliyotufikia kutoka Mkoa wetu pendwa wa Mara kwa namna ambavyo tunapangiwa safu ya uongozi katika ngazi za ubunge kutoka kwa matakwa MNEC Gachuma ambaye amepoteza hadhi ya Mkoa kwa baadhi ya majimbo pamoja na kupanga wapendwa wake katika Ubunge wa viti maalumu Mkoa wa Mara.
Harakati tayari zimepamba moto ambapo katika kikao kilichokaa katika eneo la Bukenye nyumbani kwa Mzee Gachuma tarehe 31/05/2020 huku hoja kuu ikiwa ni kupanga safu ya wabunge wa majimbo na viti maalumu ambapo waliafikiana kama ifuatavyo...
Jimbo la Tarime Mjini apitishwe Ndugu Michael Kembaki au kijana wa Kangoye..
Jimbo la Tarime vijijini apitishwe Mwita Mwikwabe Waitara.
Jimbo la Rorya Mr. Sanya
Jimbo la Butiama Magori Zeba
Jimbo la Bunda vijijini Boni Getere.
Jimbo la Serengeti Mr. Patrick Chandi.
Musoma Mjini Vedastus Mathayo.
Mwibara Kangi A Lugola
Baada ya makubaliano hayo kikao kiliweka mkakati kuwa ni lazima Gachuma aandaliwe kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara 2022 ili kumwondoa Mwenyekiti aliyepo kwa sasa kwa sababu tu hakubaliani na Mzee Gachuma katika mipango ya kuitawala Mara.
Pia katika kikao hicho walikubaliana wote kwa pamoja kuwa ni lazima viti maalumu vichukuliwe na Rhobi Kabaka ambaye ni mtoto wa Mama Kabaka kwa gharama yoyote ile pia kikao hicho kiliwapendekeza wabunge wengine wa Viti Maalumu kuwa ni Amina Makilagi pamoja Mossy Magere.
Katika kukamilisha Mkakati huo waliazimia na kukubaliana kuwa Mama Kabaka ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya NEC na Mjumbe wa NEC apewe jukumu la kuhakikisha kuwa hayo majina yote yaliyopendekezwa na Kikao hicho cha faragha yanarudi na kwamba kwa gharama yoyote ile yasikatwe huko juu. Mama Kabaka ahakikishe wahusika wote wanapewa chao ili wakamilishe Mkakati huu kwa manufaa yao.
Mkakati mwingine katika kikao hicho ilikuwa ni kuwadhibiti kwa gharama yoyote ile watia nia wengine ambao siyo wa kundi hilo na ambao wanaonekana tishio katika Majimbo hayo.
Azimio lingine katika kikao hicho ilikuwa ni jukumu la Mama Kabaka kuhakikisha kuwa anawadhibiti Viongozi wa Makao Makuu ya Chama kwa gharama yoyote ile.
Aidha Mzee Gachuma aliwajulisha wajumbe wa kikao hicho kuwa yeye yupo karibu sana na Mzee Mangula na Katibu wa CCM Taifa Dr. Bashiru Ali na Bwana Humphrey Polepole na kwamba anawamudu ila alionesha hofu yake kwa Makamu Mwenyekiti wa zanzibar na Mwenyekiti wa Taifa.
Hivyo alitoa ombi lake kwa Mama Kabaka afikishe hoja hiyo kwa viongozi hao wa juu jukumu ambalo Mama Kabaka alikubali na akasema hilo lipo ndani ya uwezo wake na kuwa atalimudu kwa asilimia mia moja.
Baada ya makubaliano kikao hicho kilihiarishwa na wajumbe kuondoka kutoka Bukenye ambapo ndiyo ngome kuu ya mipango yote kwa sasa.
Hoja yangu hapa ni kuwa ni kweli kwamba mipango hii ya kuchaguliwa viongozi sisi wananchi wa Mkoa wa Mara bado ni endelevu na inafanywa na Mzee Gachuma? Tuendelee kuvumilia kweli mpaka lini?
Hii kambi ya Gachuma ambaye pia ni zao la kupoteza majimbo mengi Mkoa wa Mara kwenda Upinzani bado ataendelea kuvuruga mkoa wetu ili wengine tunaangalia? Tuseme imetosha na SASA GACHUMA NA KABAKA BASI
Ni kweli kuwa swara la kura za maoni kwa sasa mkoa wa mara ni viini macho tu na pia ni danganya toto na kuwa uchaguzi sasa ni dhahili uliisha isha kitambo?
Nani wa kuikomboa ccm mkoa wa mara?
Tunamasikitiko makuu juu ya mipango hii dhalimu ndani ya chama chetu ccm mkoa wa Mara.
*HILI NI SIKIO LA MWANACCM ASIYE NA KAMBI KUTOKA MKOA WA MARA.*