Kuelekea Mfumo wa Utangazaji wa Digital: Maswali na Majibu Muhimu

Utatambuaje kwamba TV yako ni ya Dijitali? Au labda niweke hivi, Je kuna Umuhimu wa Mtu sasa kukimbilia TV ya Dijitali kuliko Kin'gamuzi

Naomba kwanza Nianze hivi

1. Fact 1 : - Flat Screen nyingi zilizoko Madukani be it Samsung Smart TV, Sony Bravia na Blah blah ni analogue kwa maana ya kwamba hazina Mfumo uliojengwa kwa ndani kuweza kung'amua Mawimbi ya Digitali kwa maana hiyo hata uende leo Mlimani City Ukanunua Samsung Smart TV bado utahitaji Kin'gamuzi ili uweze kuona Matangazo yaliyo katika Mfumo wa Dijitali

Mkuu @Supervisor

Naomba nikijibu kwa Kifupi kwa njia ya Kukupa Ushauri

1. Hata kama una uwezo sasa Nakushauri Usinunue TV ambayo ina uwezo ndani yake wa Kung'amua Mawimbi ya Dijitali. Najua waafrika wengi tuna Kasumba ya Kununua vitu kwa bei yeyote ili mradi na sisi tuonekane TUMO. Katika hili Nakushauri Nunua King'amuzi tumia katika TV yako uliyo nayo na hata kama unataka Flat Screen Nakushauri go for the normal and Cheap LED (Not LCD)

Nakupa Ushauri huu kwa Sababu Bado Teknolojia ya Digitali (DVB-T ambayo tunayoitumia) haija stabilize na watu bado wako Darasani wanaendelea kuiboresha. Tatizo la kukimbilia kununua vitu vya Bei ghali wakati Technolojia bado HAIJABALEHE unaweza ukaja kujilaumu na kujikuta ndani ya Mwaka Mmoja ukatakiwa Kukitupa kitu ulichokinunua kwa Gharama kubwa

Mkuu Nakupa Mfano wa Kenya. Makampuni yalianza kutoa huduma kwa kutumia Teknolojia ya Mwanzo (DVB-T) lakini baada ya Muda mfupi sana wakagundua kwamba DVB-T imepitwa na Wakati wakabadilisha Mitambo na Kuweka teknolojia mpya ya DVB-T2 you know what? Wakenya wengi walikuwa wamenunua Ma TV ya DVB-T kwa gharama lakini sasa hayafanyi kazi tena maana mfumo wa Matangazo umehama kutoka DVB-T kwenda DVB-T2 (Juzi nilikuwa na Rafiki yangu wa Uingereza akaniambia hii inaitwa Transition with Transition).

Mkuu nakushauri subiri Teknolojia Istabilize ndio uweze kununua la Sivyo inaweza kula Kwako Mazima

Ha ha haaa
 
Kwa sasa haijalishi kama TV yako ni flat au ya tumbo, unachotakiwa kuwa nacho ni king'amuzi. Down-side yake ni lazima wote tununue ving'amuzi ili kuona matangazo kuanzia January 2013. Cheapest, ni 39,000 star times. Kama una dish au kama unatumia cable, basi uko safe.
 
Sisi huku kijijini kwetu tunatumia king'amuzi cha MediaCom MFT 930 Plus na dish za futi 6 kuna sababu ya kununua ving'amuzi vingine kama sihitaji chanel za kulipia? Kwani huku wameshafika wakala wa ZUKU na wanatoza king'amuzi na dish dogo Tsh 192,000/= na chanel za bure ni TBC1 na Chanel ten tu.
 
Utatambuaje kwamba TV yako ni ya Dijitali? Au labda niweke hivi, Je kuna Umuhimu wa Mtu sasa kukimbilia TV ya Dijitali kuliko Kin'gamuzi

Naomba kwanza Nianze hivi

1. Fact 1 : - Flat Screen nyingi zilizoko Madukani be it Samsung Smart TV, Sony Bravia na Blah blah ni analogue kwa maana ya kwamba hazina Mfumo uliojengwa kwa ndani kuweza kung'amua Mawimbi ya Digitali kwa maana hiyo hata uende leo Mlimani City Ukanunua Samsung Smart TV bado utahitaji Kin'gamuzi ili uweze kuona Matangazo yaliyo katika Mfumo wa Dijitali

Mkuu @Supervisor

Naomba nikijibu kwa Kifupi kwa njia ya Kukupa Ushauri

1. Hata kama una uwezo sasa Nakushauri Usinunue TV ambayo ina uwezo ndani yake wa Kung'amua Mawimbi ya Dijitali. Najua waafrika wengi tuna Kasumba ya Kununua vitu kwa bei yeyote ili mradi na sisi tuonekane TUMO. Katika hili Nakushauri Nunua King'amuzi tumia katika TV yako uliyo nayo na hata kama unataka Flat Screen Nakushauri go for the normal and Cheap LED (Not LCD)

Nakupa Ushauri huu kwa Sababu Bado Teknolojia ya Digitali (DVB-T ambayo tunayoitumia) haija stabilize na watu bado wako Darasani wanaendelea kuiboresha. Tatizo la kukimbilia kununua vitu vya Bei ghali wakati Technolojia bado HAIJABALEHE unaweza ukaja kujilaumu na kujikuta ndani ya Mwaka Mmoja ukatakiwa Kukitupa kitu ulichokinunua kwa Gharama kubwa

Mkuu Nakupa Mfano wa Kenya. Makampuni yalianza kutoa huduma kwa kutumia Teknolojia ya Mwanzo (DVB-T) lakini baada ya Muda mfupi sana wakagundua kwamba DVB-T imepitwa na Wakati wakabadilisha Mitambo na Kuweka teknolojia mpya ya DVB-T2 you know what? Wakenya wengi walikuwa wamenunua Ma TV ya DVB-T kwa gharama lakini sasa hayafanyi kazi tena maana mfumo wa Matangazo umehama kutoka DVB-T kwenda DVB-T2 (Juzi nilikuwa na Rafiki yangu wa Uingereza akaniambia hii inaitwa Transition with Transition).

Mkuu nakushauri subiri Teknolojia Istabilize ndio uweze kununua la Sivyo inaweza kula Kwako Mazima

Ha ha haaa
Polo nashukuru kwa maelezo yako ambayo yamenipa mwanga, Ila naomba unisaidie kunifahamisha kidogo mimi niko nje ya TZ na nina king'amuzi cha media Com nafikiri ni MPG2 na dish la ft6 ninapata channel za FTA za ITV, Capital, EATV, TBC1, Startv,Chanel 10, TVM1&2, na TIM na hizi ni kupitia satelite ya intelsat 906 64e na C Pas 7/10 64e. Sasa je itakapofika hiyo tarehe 31 Desemba, 2012 saa sita usiku nitakuwa mmoja wa mwathirika kuwa sitona tena hizo channel za bongo au mie nitakuwa nime-survive kwa kuwa niko kwenye satelite.

Na kama nitakuwa ni mwathirika nini nifanye au decoder/king'amuzi gani niwe nacho niendelee kufaidi hizo channel nilizokuwa naziona na ungo je nitapaswa kubadilisha?

Natanguliza shukrani.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Rubi

Kwa Mujibu wa Maelezo kutoka kwa TCRA kupitia vipindi vyao vya Redio na Televisheni ni kwamba Mabadiliko haya hayahusu watumiaji wa Madishi. Kwa hiyo kama unatumia dish Mkuu tar 31/12/2012 lala usingizi wako Mnono kabisa wala huhitaji kufanya Mabadiliko yeyote

Ila kwa wele wanaopata Matangazo kwa Kutumia hizi antena za CHADEMA, MWIBA WA SAMAKI tar 01/01/2013 huna King'amuzi basi Utaangalia Chenga kwenye Televisheni yako

N.B Kama hutaki Hasara Usinunue TV ya Dijitali, Nunua Kin'gamuzi tumia kwenye TV yako ya Zamani
 
Last edited by a moderator:
Mfumo wa Urushaji wa Matangazo ya Television katika Mfumo wa Digitali si Mgeni hapa Tanzania. Matangazo ya Televisheni kwa mfumo wa Digtal yanatofautiana tu katika Namna Matangazo yanamfikia Mteja. Katika Mfumo wowote wa Mawasiliana, Taarifa zaweza kwa kutumia njia kuu tatu.

1. Cable ( Coaxial, Fibre Optics Cable, Copper n.)

2. Satelite ( Taarifa zinamfikia Mtumia kwa njia ya Satelite). Mitambo ya Kurushia Matangazo inakuwa imefungwa katika satelite na Mitambo hiyo huitwa kwa Lugha ya Kitaalam Transponder.

3. Terestrial: Katika Mfumo huu wa kurusha Mtanganazo, Taarifa zinarushwa kwa watumiaji kwa Kutumia Mitambo iliyoko hapa hapa Duniani namaanisha Ardhini.

Kulingana na namna Matangazo yanavyorushwa Technolojia Mbalimbali zimeibuliwa

1. DVB-C : Matangazo ya Digital kwa njia ya Cable

2. DVB-S: Matangazo ya Digitali kwa njia ya Satelite

3. DVB-T: Matangazo ya Digitali kwa Njia ya Mianara iliyoko Ardhini ( Ambako nataka Uzi huu Ujikite hapo)

1. Je Matangazo ya Digital ni Mageni hapa Tanzania?

Hapana, Matangazo ya Televisheni kwa Njia ya Digitali yamekuwepo Tanzania kwa Muda Mrefu. Watanzania wamekuwa wakipata Matangazo ya Televisheni kwa mfumo wa Digital kwa Njia ya Cable ( Cable TV) na Satelite.

2. Je ili kuona Matangazo ya Digitali ni Lazima utumie Ving'amuzi wa Star Times au Ting Peke yake?

Hapana. Matangazo ya Digitali yanakuwa katika Standard iitwayo DVB-T au DVB-T2 ( Digital Video Broadcasting over Terrestrial). Kwa Hiyo Mtu yeyote Mwenye King'amuzi chochote ( Si Lazima Agape au Startimes) ambacho ni DVB-T compliance anapaswa kuona zile channel za Bure kama Channel ten, ITV, TBC1, Agape) Ila ili uweze kuona Channel za Kulipia kama TBC2 au Agape 2 ni Lazima upate ving'amuzi husika.

Nakaribisha Mjadala wenye Siha na Maswali ambayo naamini kuna wana JF wataalamu watayajibu mimi nimeanza na hayo mawili ili kila Mmoja afahamu mfumo huu mpya na aweze kufaidika

Niite Polo

HII Ndio JF bwana for great thinkers.
Safi sana Polo somo zuri
Niite polo.Ha ha safi sana!!!
 
mkuu hizi format za mpeg 4 na usb zinatumikaje ktk mfumo huu??kuna watu wanaitwa BTL wamenitumia sms,mkuu saidia bhana
 
Mkuu kama nakumbuka vizuri,carrier wave signals huwa hazibadilishwi,kazi yake ni ku-carry tu inteligemce signals/information to detination ambapo ndio zinakuwa demodulated,kwa masafa mafupi unaweza ukarusha inteligence signals bila kutumia carrier signals,
modem ni muungano wa herufi za mwanzo toka katika maneno MOdulator na DEModulator. Modulation ni kitendo cha kubadili carieer signal kutokana na sifa fulani ya message signal(i.e frequency, amplitude,phase e.t.c). Na demodulation ni kitendo cha kurudisha message signal kama ilivokuwa hapo awali. Hivyo basi hii inamanisha kwamba modem ina uwezo wa kufanya modulation na demodulation. katika radio communication signal ni lazima iwe modulated katika transimetter na demodulated katika receiver. modulation imegawanyika katika nyanja kuu mbili i.e Digital modulation na Analog modulation. katika digital modulation kuna schemes kama vile FM, AM na PM. wakati katika digital modulation kuna schemes kama PSK, QPSK, MSK, FSK, ASK, GMSK e.t.c. Kwa hiyo basi ili hiyo unayoita analog tv iweze kamata digita transmitted signal ni lazima iwe na demodulator yenye uwezo wa kubadili digitaly modulated signal kwenda katika normal message signal. Ukipima hapo utatambua kwamba modem digital ndo inahitajika na si decoder kama ulivyodai wewe. hope nimeeleweka na unakaribishwa kwa swali lolote lihusulo radio waves propagation.
 
Mkuu kama nakumbuka vizuri,carrier wave signals huwa hazibadilishwi,kazi yake ni ku-carry tu inteligemce signals/information to detination ambapo ndio zinakuwa demodulated,kwa masafa mafupi unaweza ukarusha inteligence signals bila kutumia carrier signals,

Spot on, carrier frequency ni fixed hisipo kuwa modulating signal ndio ina-ride juu na chini ya carrier frequecy, kitu kingine huwezi kurusha baseband masafa mafupi through the air bila ya kutumia carrier frequency labda ukitumia waya, lakini hata na hiyo inategemea kama base band ni ya analogia au ya digitali; kama ni ya digitali itakuwa ngumu kuituma masafa mafupi kwa kuwa data za digitali zina a DC componet, odd na even Harmonics kuanzia moja mpaka infinity!!!! Ndio maana wanatumia MODEM kufanikisha kutuma mawimbi ya digitali kupitia kwenye copper waya. labda niongezee kwamba MODEM zinatumika vile vile kwenye wireless communication kwa ajili ya kufanikisha zoezi zima la kusafirisha mawimbi ambayo ndani yake kuna data za kidigitali, nimejitahidi sana kuzungumza in a lay language - samahani.
 
mkuu hizi format za mpeg 4 na usb zinatumikaje ktk mfumo huu??kuna watu wanaitwa BTL wamenitumia sms,mkuu saidia bhana

Mkuu pono

MPEG 2 au MPEG 4 ni njia tu za Ku Compress information ili ziweze kupita kwa wingi katika Chanel finyu. MPEG 4 ni Improvement ya MPEG 2. Mkuu Kama unataka kununua king'amuzi nunua cha

1. DVB-T2 MPGE 4

Cause Ukiwa na MPEG 4 Unaweza kuona Matangazo yaliyofinyangwa ki MPEG2 and not vice verse. Mkuu Sisitiza DVB-T2 MPEG 4
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kama nakumbuka vizuri,carrier wave signals huwa hazibadilishwi,kazi yake ni ku-carry tu inteligemce signals/information to detination ambapo ndio zinakuwa demodulated,kwa masafa mafupi unaweza ukarusha inteligence signals bila kutumia carrier signals,

Mkuu ngoja nijaribu kukuelezea kinamna nyingine. I can see kuna kitu hapa unachanganya. Let say unaambiwa Radio One inarusha matangazo katika frequncy ya 89.5MHz, hii ina maana ya kwamba hiyo frequency ya 89.5 MHz ni frequency ya carrier na ile sauti ya mtangazaji aliyeko studio ndio inaitwa message signal ambayo ina ujumbe unaotakiwa kuasafirishwa kwenda mahala pengine. Kwa kawaida sauti ya mwanadamu huwa inarange toka 60Hz mpaka 7000Hz.

Hivyo basi kwa kusafirisha mawimbi ya data utahitaji kisafirishio(carrier) na kisafirishwa(message) ili ujumbe wako ufikie hatma yake pasipo mushkeri. Ndipo hapo katika usafirishaji utahitaji carrier iwe inabadilishwabadilishwa tokana na sifa fulani ya message signal.

Natumai hapo umenipata.
 
Mkuu Hapo kwenye Blue Rekebisha

Human Audible range is 20Hz - 20KHz. Below 20Hz haya Masafa yanaitwa Infrasound
 
Hiyo ipo sahihi mkuu, hapo nazungumzia frequency ya sauti ambayo mwanadamu anaongea. Huwa ni 60 hz mpaka 160 Hz kwa mwanaume na 150 Hz mpaka around mia mbili na kitu hv (sikumbuki vizuri) kwa mwanamke. Sema hiyo 7000Hz ni ambayo mwanadamu anaweza kujitune kuongea/kuimba nayo.

Hiyo 20 Hz mpaka 20 KHz nathani ni audible range i.e sauti ambayo mwanadamu wa kawaida anaweza sikia.
 
Mkuu Hapo kwenye Blue Rekebisha

Human Audible range is 20Hz - 20KHz. Below 20Hz haya Masafa yanaitwa Infrasound

Mkuu saidia hili pia:
Naomba ufafanuzi kwamba,ni utaratibu gani unatumika TV Station ya nyumbani kurusha live matangazo ya TV nyingine,kwa mfano,ITV inapojiunga na BBC World au CAPITAL TV inapojiunga na CNN?

Pili,kuna tv nyingi tu tu zinapatikana live kwenye internet,na tunaziona bure(kwa internet bundle ya hapa nyumbani), je wenye tv hizo wananufaika vipi? Kwa mfano,ni muda mrefu sasa natumia internet kuangalia live football games kupitia ESPN,SKY Sport,ITV(UK) nk. gharama ninayoingia ni kununua internet bundle tu.

Je,vipi hakuna uwezekano wa hawa akina ZUKU kutuonesha hizi internet channels kupitia ving'amuzi vyao? Maana wakifanya hivyo,DSTV watakuwa wamepata mshindani na obviously watashusha gharama zao.

Kwa leo mi nina hayo tu!
 
Mkuu ngoja nijaribu kukuelezea kinamna nyingine. I can see kuna kitu hapa unachanganya. Let say unaambiwa Radio One inarusha matangazo katika frequncy ya 89.5MHz, hii ina maana ya kwamba hiyo frequency ya 89.5 MHz ni frequency ya carrier na ile sauti ya mtangazaji aliyeko studio ndio inaitwa message signal ambayo ina ujumbe unaotakiwa kuasafirishwa kwenda mahala pengine. Kwa kawaida sauti ya mwanadamu huwa inarange toka 60Hz mpaka 7000Hz.

Hivyo basi kwa kusafirisha mawimbi ya data utahitaji kisafirishio(carrier) na kisafirishwa(message) ili ujumbe wako ufikie hatma yake pasipo mushkeri. Ndipo hapo katika usafirishaji utahitaji carrier iwe inabadilishwabadilishwa tokana na sifa fulani ya message signal.

Natumai hapo umenipata.
Mkuu nikuulize kitu kimoja.Frequency ya carrier ina 'vary' from one place to another?Kama ndio kwa nini,kama hapana ni kwa vipi radio station moja inapatikana kwenye frequency tofauti kwenye mikoa au maeneo tofauti.
 
By Kaka'

Jibu ni ndio. Ya kwamba frequency ya carieer inavary kutokana na maeneo tofauti. Na radio station let say clouds, kama inataka sikika katika mikoa tofautitofauti ni lazima iweke repeater katika mikoa hiyo. Na kuna criteria ambazo huwa considered katika uchaguzi wa career frequency.
Nimekujibu swali na dukuduku lako.?
 
turud kwny TV sasa

nna mediacom mpeg2 na dish futi6 nina C band na KU
nikinunua MPEG4 nitapata badiliko gani kwenye tv yangu?
 
Back
Top Bottom