Kuelekea 2015: Kiongozi UVCCM awataka vijana wavute bangi wawe kama wendawazimu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuelekea 2015: Kiongozi UVCCM awataka vijana wavute bangi wawe kama wendawazimu...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mohamedi Mtoi, Oct 10, 2012.

 1. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #1
  Oct 10, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  KAMANDA wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Christopher Gachuma, amewataka vijana wa chama hicho, kuwa kama ‘wendawazimu' ifikapo mwaka 2015.

  Akifafanua kauli hiyo, Gachuma ambaye pia ni Mjumbe wa NEC alisema, vijana wanapaswa kufikia hali hiyo katika kuhakikisha hadhi ya chama hicho, inarudi katika mwaka huo wa uchaguzi.

  Gachuma alitoa kauli hiyo jana katika ukumbi wa CCM wilayani hapa, wakati alipokuwa akitoa nasaha zake kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa viongozi wa umoja huo Mkoa wa Mara.

  "Katika kuhakikisha hadhi ya CCM inarudi katika uchaguzi wa mwaka 2015, vijana hamna budi kuwa kama wendawazimu, yaani huwa natamani ingewezekana mvute hata bangi," alisema.

  Katika mkutano huo, Gachuma alitoa Sh milioni 6 katika kufanikisha uchaguzi huo, ikiwa ni shinikizo la wajumbe kutaka kulipwa posho baada ya kelele nyingi za "poshooo" kutawala ukumbini.

  Pamoja na mambo mengine, Gachuma aliwataka makatibu wa CCM wa wilaya na mkoa, kuandaa makambi ya vijana, kwa ajili ya kile alichokiita kujenga ukakamavu na ujasiri katika kupambana na upinzani.

  Katika uchaguzi huo, Ditto Manko (28) alichaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa UVCCM Mkoa wa Mara, baada ya kupata ushindi wa kura 274 kati ya kura 528 zilizopigwa.

  Wengine waliogombea nafasi hiyo na kura zao katika mabano ni Gabriel Munassa (245) na Mariam Magesa (7).

  Nafasi ya Baraza Kuu Taifa ilikuwa ikigombewa na wagombea watatu na kura walizopata katika mabano ni David Wembe, aliyeshinda kwa kura 253.

  Wengine ni Fyeka Sumera (209) na Edward Misanga aliyejitoa baada ya uchaguzi katika nafasi hiyo kurudiwa kwa mara ya pili.

  Katika nafasi ya mkutano mkuu CCM Taifa, Kennedy Nsenga alishinda nafasi hiyo kwa jumla ya kura 230, Yohana Munema (48) na Gabriel Munassa aliyeamua kujitoa.

  Anna marwa alichaguliwa kuwakilisha nafasi ya uwakilishi wa vijana kwenda Umoja wa Wanawake (UWT) mkoa kwa ushindi wa kura 271 dhidi ya mpinzani wake, Naima Minga aliyepata kura 155.

  Naye, Amon Mtega kutoka Songea anaripoti kwamba, mgombea aliyekuwa anawania nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Injinia Zephania Chaula kupitia Wilaya ya Ludewa, amekata rufaa ya kupinga matokeo ya uchaguzi.

  Mgombea huyo amefikia uwamuzi huo kwa kile kilichodai kutotendewa haki kutokana na kukiukwa kanuni za uchaguzi zilizowekwa na chama hicho.

  Akizungumza na Mtanzania jana, Chaula alisema kuwa, amefikia uamuzi huo wa kukata rufaa kupinga matokeo kwa kudai hayakuwa sahihi.

  "Wajumbe walipowasili kwa ajili ya uchaguzi waliambiwa ukumbi hautoshi, jambo ambalo tulilazimika kwenda kufanyia uchaguzi nje ya ukumbi, jambo ambalo lilikuwa kinyume na taratibu.

  "Kitendo cha kufanyia uchaguzi nje ya eneo husika, kiliwafanya wajumbe kubaki wakishangaa na huku baadhi ya viongozi ambao waliwania nafasi hiyo majina yao hayakurudi.

  "Walikuwa wakipiga kampeni za waziwazi kwa kumtaka mgombea wao Elizabeth Haule, aweze kushinda. Hii ni kinyume cha taratibu za uchaguzi.

  "Tumeanza uchaguzi kwa mizengwe mikubwa nikapata kura 521na mpinzani wangu 522, huku wa mwisho alipata kura 22 jambo lililowafanya wajumbe kubaki wanalalamika kwa mizengwe na kufanya uchaguzi urudiwe tena," alisema.

  Kwa mujibu wa Chaula, wajumbe walipoanza mchakato wa kurudia kupiga kura, ndipo kigogo mmoja alianza kupiga kampeni za waziwazi kwa kutaka mgombea wake ashinde nafasi hiyo.

  Akinukuu maneno aliyosema kigogo huyo, Chaula alisema. "Ndugu wajumbe leo mshindi lazima apatikane na nimewaandalia zawadi wajumbe wote, ninatambua matatizo ya kila kata, hivyo nitawapa majenereta, barabara nk," alisema.

  Kauli hiyo iliwafanya baadhi ya wajumbe kuanza kupiga kelele kuwa, kinachofanyika siyo sahihi na kutaka kila mgombea asimame kwa miguu yake mwenyewe, ili kutoa fursa kwa wajumbe kuchagua mgombea wanayemtaka.

  Hata hivyo uchaguzi ulifanyika na baadhi ya wajumbe walitoka kwa kukata tamaa na kuchukizwa kwa mizengwe iliyokuwa ikifanyika katika eneo hilo la uchaguzi, uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Ludewa mjini.

  Alisema tayari ameshawasilisha rufaa yake katika ofisi za CCM Mkoa wa Njombe na katika malalamiko hayo ameweka vielelezo vyote vya ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi, zikiwemo CD za tukio zima.

  Baadhi ya wajumbe katika uchaguzi huo waliozungumza na Mtanzania, walikiri kuwapo kwa ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi.

  "Uchaguzi wa mjumbe wa NEC, umefanyika gizani na kwenye uwanja ambao hata usalama wa kutambua kuwa, hawa ni wajumbe sahihi au si sahihi ni vigumu," alisema mjumbe mmoja.


  Chanzo: Mtanzania
   
 2. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,782
  Likes Received: 36,777
  Trophy Points: 280
  Kwa iyo inabidi wavute bange nyingi ili wajivue ufahamu.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 3. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  ok,seen
   
 4. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #4
  Oct 10, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Wakisha vuta bangi nyingi na kujivua ufahamu wakishutka kutoka kwenye hang over zao za kibangibangi wanakuta watu wako uwanja wa taifa wanakula keki ya M4C
   
 5. mangikule

  mangikule JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 3,171
  Likes Received: 1,256
  Trophy Points: 280
  Tunajua wanavuta hadi leo!! kwani siri? Kiama cha haya majambazi ni 2015 I swear tutakamata hata polisi tufungie ndani wenyewe!!
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,052
  Trophy Points: 280
  Yaani mi naona akili za maiti zina akili kuloko akili za washabiki na wafuasi wa CCM
   
 7. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Hivi ndiyo huyu Gachuma mwenye elimu ya darasa la saba, mwenye kutumia. wakalimani aendapo nje...Si ajabu kutoa ushauri wa namna hii, na kwa hali hii sishangai pia CCM kutaka "wasomi" washike hatamu ndani ya chama.
   
 8. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Sishangai,nahisi wameamua kuonyesha rangi zao halisi!
   
 9. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Tayari ni wendawazimu! au anataka wawe zaidi ya uwendawazimu yaani wawe na mtindio wa ubongo??
  Hilki chama kinaombwe la uongozi! 2015 mwisho wao tunawalaza kifo cha mende! miguu juu!!
   
 10. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Sito shangaa kwani mtu kama lusinde na burn karudi ni ushahidi tosha wa uvutaji bangi:
  sisiemu oyeeeeeeeeeeeeeeeeeee
  bangioooooyeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 11. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Weed! Ha ha ha ha ha teh teh teh teh teh, mwisho wataambizana wale vinyesi
   
 12. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Ha ha haaaa, siku hizi hatumii wakalimani ng'eng'e inapanda vizuri tu tena fluent...

  Ila ukimcheki vizuri anaonekana kama naye bado anapiga kitu cha Tarime.
   
 13. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hawajavuta bangi ndio mazuzu hivi, je wakivuta si itakuwa balaa!!

  Nawashauri wavute tu, tena wamtume mkulu awaletee ya kufilter kutoka US.
   
 14. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Ndo maana mi huwa naamini sio kila mwenye pesa ana busara. Kuna madude mengine pesa yamazipata kwa njia za ajabu sana. Sasa dude kama hili li gachuma kwa ushauri kama huu, unafikiria hizo pesa limezipataje??? Duh!!! kwa kweli watanzania kazi tunayo. Kama dubwana la dizaini hii nalo eti ni li kiongozi, tutegemee Tanzania ya watu wasio na akili timamu. IS THIS THE ADVICE A LEADER OR A WISE MAN CAN GIVE TO YOUTH??? MY GOD......!!!!
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Kwani wameacha lini kuvuta bange, huwezi kuwa kwenye chama kile hama akili zako si ......... (Naogopa ban)
   
 16. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  maneno ya gachuma yanautofauti gani na ya wa-hasira
   
 17. M

  Maseto JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 721
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Inasemekana mara baada ya kusema maneno hayo vijana hao walianza kutekeleza agizo hilo kwa vitendo.walipigana balaa.nadhani walikuwa wamekwishavuta.waliongoza kosovo hilo ni wale wale vijana wa Tarime
   
 18. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  umejuaje muddy mtoi? waache waivute tu.
   
 19. c

  chigwiye JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndiyo tafsiri yenyewe, kama kiongozi anahamasisha live uvccm wavute BANGE ili ifikapo 2015 wawe fit na kwamba wahudhurie makambi ya kujifunza UKAKAMAVU ili kukabiliana na wapinzani.Hii inamaanisha CCM tayari wanajua hawataweza kushinda kupitia Box la kura, bali nguvu, mapigano na ghasia.

  Rejea pia kauli ya January Makamba kwamba CCM Haitakaa iachie madaraka 2015, ni wazi CCM inafanya maandalizi ya kubaki madarakani kwa namna yoyote. Kwa kauli zao, inamaanisha wako tayari kumwaga damu.

  Je! Tendwa anaziweka ktk kumbukumbu kauli hizi?
  Raisi JK hana cha kukemea?
  Hakuna mcha Mungu ndani ya CCM akakemea?
  Ama, Maaskofu,Mapadre,wachungaji,Masheikh, Hawana jukumu ktk hili?
  Wanahabari, hamna nafasi ya kusema kitu juu ya hili?

  OK! KUMBE MWASUBIRI YATOKEE NDIPO MNYANYUE VINYWA VYENU.OLE WENU MTAWAJIBIKA,KAMA SI HAPAHAPA BASI MBINGUNI.Sisi hatuna pa kuyasemea haya,bali nyie mmekasimiwa dhamana na hamfanyi mpaswayo.

  Dhamira zenu zimekua ngumu kama jiwe
   
 20. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #20
  Oct 10, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Hata hivyo kilimo cha bhange yeye ndo mnunuzi Tarime,anahamasisha walime kwa tractor na wanapewa pembejeo,
   
Loading...