Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa...

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Aug 28, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,467
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Baada ya kumsikiliza kwa makini Waziri Mkuu "Mstaafu", Edward Lowassa katika two- series za kipindi cha Dakika 45 cha ITV, kwanza nimemkubali sana huyu jamaa!, pili kama yeye ndiye angekuwa rais, ile 2005, Tanzania tusingefikia hapa tulipofikishwa sasa na utawala wa JK!, ila kikubwa zaidi, (kama ni kweli afya yake sio mgogoro kama anavyodai mwenyewe kuwa yuko fit, japo he looks sick!), CCM ikimsimamisha yeye kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, then matokeo ya urais kwa 2015, ni CCM tena!. Mkubali!..., mkatae!.

  Hizi ni baadhi tuu ya sababu, kwanini CCM itashinda tena kwa ushindi wa kishindo kikuu, endapo and only if itamsimamisha Edward Lowassa!.

  1. Uwezo wa Kusema, Kupanga, Kutenda na Kusimamia!.
  Viongozi karibu wote waliopo CCM, wana uwezo mkubwa sana kesema!, tutafanya hiki, tutafanya kile!, ni maneno tuu! na pia wana uwezo mkubwa wa kupanga mipango kwa maneno tuu na sii matendo, au usimamizi, mfano mipanga kamambe kama (Mkukuta, Mkuza, Mkumbita, Mkurabita, na sasa Dira 2025)!. Mipango yote hii ni mizuri kwa maneno tuu, lakini wengi hawana uwezo wa kutenda na kusimamia utekelezaji!. Mipango mingi iliyopangwa, inaishia kwenye maneno na mabuku na makabrasha tuu, lakini utekelezaji kwa vitendo ni sifuri!. Kwa Edward Lowassa, yeye sio msemaji sana, bali ni mtendaji kweli!, yeye sio mtu wa maneno mingi!, ni mtu wa vitendo virefu!, he is an action oriented man!. Mfano hai ni pale alipokutana na madudu ya City Waters!, aliwafurusha there and then!. Hata madudu ya Richmond, alitaka kuwafurusha na kutaifisha kila kitu ila alishindwa!, kutokana na "mwenye mitambo!".

  Tulipopata uhuru miaka ya 60, maadui wetu wakuu watatu, walikuwa ni Ujinga, Umasikini na Maradhi, na tulijiwekea misingi yetu mikuu minne ya maendeleo kuwa ili tuendelee, tulihitaji vitu vinne: Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora!. Kwenye hiyo misingi, tulisema Pesa sio msingi, pesa ni matokeo!, hili ndilol lililokuwa kosa pekee la Mwalimu, kutofautiana na misingi ya ukweli ya uchumi, kama ilivyofundishwa na Adam Smith (land, labor, capital na interpreneureship)!. Kwenye ile misingi minne tulisahau capital kwa kudai "pesa sii msingi!".

  Watu tunao na ardhi ya kutosha, yenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, madini, maliasili etc etc tunazo. Tulikuwa na tatizo kidogo la utekelezaji wa siasa safi ya Ujamaa na Kujitegemea na uongozi bora, ndio maana nchi tulizopata nazo uhuru, ile miaka ya 60, wao wakiwa ni masikini wa kutupwa kuliko sisi, with nothing, kana Tiger nations, leo wako mbali!, sababu pekee iliyowafikisha wenzetu pale walipo, wakati sisi tunaendelea kupiga mark time ni Elimu!. Sisi tulitaja tuu kuwa Ujinga ni adui, lakini we never invested on Elimu because we had no capital!. Nyerere aligombana na maprofesor wa uchumi, Kina Prof. Rweyemamu, wakajitimkia zao, akagombana Edwin Mtei na IMF, WB etc matokeo sote tunayajua!.

  Lowassa na timu yake ya Boys II Men, walipoingia tuu madarakani, EL akafanya study tour ya nchi tulizoanza nao wakati wa uhuru!, kwanini wao wamefanikiwa, wako mbali na sisi wametuacha nyuma sana!, akagundua wali invest kwenye elimu!. Akarudi nyumbani, akahamasisha kila kata iwe na shule ya sekondari ili kila Mtanzania apate kwanza elimu, mengine yote, yatafuatia!. Baada ya kujengwa shule, zilikuwa zipatiwe vifaa na waalimu wa kutosha!.

  Baada ya kujiuzulu, serikali ya JK ikazi abandon zile shule za EL ili kumkomoa!. Sasa zinaitwa St. Kayumba!. Mpango wa kufundisha waalimu wa ukweli, ukaachwa, nanachukulia wale failures wenye Div IV karibu na zero, na kuwa brush kwa miezi mitatu! (Waalimu wa Voda Faster!). Jana alipozungumzia umuhimu wa kuwaelimisha kwanza watu wetu, amenigusa sana!. Tungekuwa tumeelimika, tusingeibiwa hivi madini yetu!, tunaibiwa madini yetu huku tunaangalia kwa sababu hatuna elimu ya madini!, sasa tumegundua gesi,serikali inakimbilia kugawa vitalu kwa umiliki wa miaka 99 huku Watanzania hatuna hili wala lile kuhusu elimu ya gesi, hatuna sera wala sheria ya gesi!. Kwa kifupi, hutujui lolote wala chochote kuhusiana na gesi!, na tutaishia kuibiwa tena gesi yetu kwa kukosa elimu ya gesi!. Edward Lowassa ameshauri, hiyo gesi tuiache kwanza!, lets invest kwenye elimu kwanza kwa watu wetu, ili kuwa empower hawa watu wetu kielimu ndipo tuingie kwenye ambitious projects kama za kuvuna gesi, au kilimo kwanza etc!.

  Kwa hili pekee, CCM ikimsimamisha EL, Tanzania itapata ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.

  Nimesema, CCM ikimsimamisha EL, 2015, itakuwa ni CCM tena, kwa sababu katika wapinzani wote, hakuna hata mgombea mmoja anayeweza kusimama na Lowassa kwenye urais wa 2015 na bado akaambulia kura!, there is no one!, none!.

  Mwenye masikio na asikie!.

  2. Dhambi Kubwa ya Lowassa ni Richmond Tuu!.

  Najua wapinzani wa dhana ya ukweli, watakuja na hoja za dhambi kubwa ya Lowassa ni fisadi wa Richmond!, then time will tell, hiyo ni mizigo tuu ya watu, alijitolea kuibeba ili kwa kuteswa kwake, wao waokoke!, wakati muafaka ukifika, hili litawekwa wazi na Watanzania mtawafahamu wenye zigo lao haswa ni kina nani!. Wenye akili wameshang'amua ile metarmophosis process from Richmond -Dowans -Simbion na kwa msio jua, mkae mkijua Tanesco bado inailipa Simbion capacity charge ile ile ya dola 152 kama Richmond na Dowans, hivyo tumeruka majivu na kukanyaga moto, tumeruka maji na kukanyaga tope, na kwa usafi tumeruka nyasi, tukakanyaga ma..!.

  3. CCM Haina zaidi ya EL na Upinzani hawana wa Kushindana Nae!.

  Wanabodi ni mimi niliwahi kusema, CCM imechokwa na Chadema Haijajipanga, baadae nikasema CCM imechokwa mpaka basi!, Baada ya Chadema kuanza kujipanga nikasema Chadema, Njia Nyeupe Ikulu, lakini sasa baada ya kumsikia Edward Lowassa, kama ni kweli afya yake sii mgogoro kama anavyoonekana!, na CCM ikamsimamisha yeye, come 2015, then, mshindi wa uchaguzi wa 2015, ni CCM tena!, kinyume cha hapo, CCM ikimsimamisha mwingine yeyote, 2015, Chadema inachukuwa nchi kiulaini kama kumsukuma mlevi!.


  Mwisho.

  Namalizia kwa swali moja tuu, Jee CCM inaujasiri wa kuukubali ukweli huu mchungu wa kumsimamisha Edward Lowassa ili kuweza kujiokoa?! au itaendeleza kiburi uongozi na jeuri ya uchama tawala kusubiria kifo cha mende huki inajiangalia kwa kutegemea itaendeleza uking'ang'anizi wake kwa kuamini this time pia itashinda tena kwa kuutumia uwongo ule ule, na mbinu zile zile za uchakachuaji ule ule, kwa matarajio katiba mpya pia ita provide opportunities za aina ile ile ya miaka ya nyuma, kuwa ita endelea "to fool all the people all the times?!.

  Asante.

  Pasco.

  NB. Japo Pasco wa JF sio mwanachama wa Chama chochote cha siasa, kwa CCM ni Pro Lowassa, kwa Chadema ni Pro ZZK na kwa CUF ni Pro-Jussa!.

  Input ya Tanganyika Tanu.
  Mkuu Tanganyika Tanu, pole sana, hii kitu yako imeunganishwa kwangu!. Ili kukutendea haki, nimeiweka kule juu kwenye main post.
  Pasco.

   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Tanzania ina watu zaidi ya milioni 40. zoezi la sensa linaweza kutuambia tuko mil 50!
  Kuwa obsessed na mtu mmoja katika nchi yenye watu wengi kiasi hicho ni tatizo.
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Wakati unasema CHADEMA njia nyeupe Ikulu, Lowassa alikuwa holiday mwezini? Sasa amerudi and you've just realised you forgot he was still alive?
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  "Watanzania siyo mabwege tena", Harrison Mwakiembe (PhD).
   
 5. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  nilijua utakuwa wew tu...ni mawazo yako labda na familia yako....lakini watanzania wanjua nin wanahitaji katika hiki kipindi kigumu katika maisha yao...
   
 6. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Pasco

  Mbona kwenye thread za polisi kufanya mauaji morogoro sikuoni?

  au hizi thread za EL zina maslahi ?
   
 7. J

  JF-MBUNGE JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Anafaaa LKN......ajiulize waliomfikisha hapo pabaya ni kina nani kwanza wawe nao mbali
   
 8. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Pasco unatumia sabuni gani na brash gani na maji yenye kemikali hipi kusafisha hii kitu yenye kutu???Naomba jibu this is too late maana CCM wanajua kisasi alichonacho rohoni wamsimamishe apate uraisi awafanye kama Chiluba na Kenneth Kaunda??no way na haitakuja kuwa!!for your info!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #9
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Quote: NB. Japo Pasco wa JF sio mwanachama wa Chama chochote cha siasa, kwa CCM ni Pro Lowassa, kwa Chadema ni Pro ZZK na kwa CUF ni Pro-Jussa!.

  ..Leo ndio nimekusoma itikadi yako Brother Pasco!!. Leka Tutigite
   
 10. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #10
  Aug 28, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Anafaa sana, atatuletea mvua za kutengeneza wakati wa ukame kutoka Thailand!
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  You really need help Pasco
  seriously

  Wapo watu waliamini kwa asilimia 100 kuwa Rais aliefaa mwaka 1995 na 2005 alikuwa
  Salim A Salim
  Watu hao ni pamoja na Mwalimu Nyerere

  lakini hawakuwahi kuwa 'this crazy over one person'....

  Nahofia coming 2016 na Rais sio huyu unaemtaka
  unaweza usi recover mentally kwa kweli......You need help now
   
 12. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #12
  Aug 28, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,695
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Mkuu kama ni hivi bado safari ni ndefu sana ya kutusababisha tumwamini..Convincing yake inahitaji kuchukua miaka 20 ambapo umri wake utakuwa umeshaenda sana..kama nafasi alikuwa nayo akaichezea kuirudisha ni ngumu sana..Namshauri atafute mtu wa type yake amweke but not him.
   
 13. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #13
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  bado tupo msibani morogoro, wewe na lowasa wako hukohuko na alichokupa.
   
 14. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,695
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Leka Dutigite EL...!!!!
   
 15. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #15
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ..Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema aliwahi kuulizwa nini vitakuwa vipaumbele vitatu vya Chadema endapo itakamata Dola, alijibu:
  1. Elimu
  2. Elimu
  3. Elimu
  Nilimsikiliza Lowassa jana, nae anasisitiza haungi mkono Kilimo Kwanza, bali Elimu Kwanza.
  What a coincidence?
   
 16. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #16
  Aug 28, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Manywele juu, juu juu zaidi
   
 17. Ston Merchant

  Ston Merchant JF-Expert Member

  #17
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 395
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  binafsi nimeona kma EL afya yake mgogoro kidogo, alikua anaongea kwa shda shda af design memory yke imekaa kushoto kdg........

  reference nyingi za mambo aliyokua akijaribu kupambanua alikua hakumbuki...........
   
 18. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #18
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
 19. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #19
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,128
  Trophy Points: 280
  Hauko serious. Lowasa u-billionea wake ule unafikiri kapatia Richmond? Au unafikiri ni ali-save mshahara wake akawa bilionea wa kutisha? Uliza watu alifanya nini alipokuwa waziri pale wizara ya Ardhi. Kumbuka Nyerere alimkataa Lowasa kwamba hana ethics za uongozi KABLA ya hiyo Richmond. Kumbuka wahindi waliomwambia Lowasa ananuka rushwa KABLA ya hiyo Richmond. Yes, anajua sana kuongea na kupanga hoja, lakini hivi unamjua Lowasa wewe?
   
 20. c

  change is must Member

  #20
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 1, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kweli jamaa alikuwa msafi na anauchungu na wa TZ angewataja wa husika wa richmond ili wamuamini ni mtendaji na mtetezi. Bt jamaa kiukweli bila kuficha hafai tena hafai coz hakuona shida kuwasulubu wezi bali akabeba msalaba huo ambao hatautua kutoka mioyo ya watu up to the death. Namshauri ndoto hizo za mchana asiote tena. Wa TZ si maiti tena.
   
Loading...