Elections 2015 Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa...

Wanabodi,

3. CCM Haina zaidi ya EL na Upinzani hawana wa Kushindana Nae!.

Wanabodi ni mimi niliwahi kusema, CCM imechokwa na Chadema Haijajipanga, baadae nikasema CCM imechokwa mpaka basi!, Baada ya Chadema kuanza kujipanga nikasema Chadema, Njia Nyeupe Ikulu, lakini sasa baada ya kumsikia Edward Lowassa, kama ni kweli afya yake sii mgogoro kama anavyoonekana!, na CCM ikamsimamisha yeye, come 2015, then, mshindi wa uchaguzi wa 2015, ni CCM tena!, kinyume cha hapo, CCM ikimsimamisha mwingine yeyote, 2015, Chadema inachukuwa nchi kiulaini kama kumsukuma mlevi!.


Mwisho.

Namalizia kwa swali moja tuu, Jee CCM inaujasiri wa kuukubali ukweli huu mchungu wa kumsimamisha Edward Lowassa ili kuweza kujiokoa?! au itaendeleza kiburi uongozi na jeuri ya uchama tawala kusubiria kifo cha mende huki inajiangalia kwa kutegemea itaendeleza uking'ang'anizi wake kwa kuamini this time pia itashinda tena kwa kuutumia uwongo ule ule, na mbinu zile zile za uchakachuaji ule ule, kwa matarajio katiba mpya pia ita provide opportunities za aina ile ile ya miaka ya nyuma, kuwa ita endelea "to fool all the people all the times?!.

Asante.

Pasco.

Naendelea kutafakari nilisema nini 28th August 2012, nini kimetokea, na nasubiria kwa hamu nini kitatokea tarehe 25 October, 2015!.

Pasco.
 
Wanabodi,
Mwisho.

Namalizia kwa swali moja tuu, Jee CCM inaujasiri wa kuukubali ukweli huu mchungu wa kumsimamisha Edward Lowassa ili kuweza kujiokoa?! au itaendeleza kiburi uongozi na jeuri ya uchama tawala kusubiria kifo cha mende huki inajiangalia kwa kutegemea itaendeleza uking'ang'anizi wake kwa kuamini this time pia itashinda tena kwa kuutumia uwongo ule ule, na mbinu zile zile za uchakachuaji ule ule, kwa kuwa ita endelea "to fool all the people all the times?!.

Asante.

Pasco.


With just 7 days to come, hakuna kipya cha kuwaambia wanabodi, bali ni kukumbushana tuu, tulisema nini, nini kimefanyika, nini kinafanyika sasa, na nini kitafanyika hizo siku 7 zijazo, yaani tarehe 25 October, lets not let CCM to fool all the people all the times!.

kiukweli kabisa, sioni jinsi yoyote ya CCM kushinda tena!, Chadema inakwenda kuchukua nchi kiulaini kabisa kama imeokota!, yaani CCM inakwenda kuanguka chini kiulani kabisa kama kumsukuma mlevi!.

Lakini ili hili litimie, ni lazima kila aliyejiandikisha, ajitokeze hiyo tarehe 25, aende kupiga kura na kumchagua Edward Lowassa!.

If "Together wa can!", and "United we Stand", "Victory is ascertain!"

Nawatakia Jumapili njema!.

Pasco
 
Baada ya Lowassa kusifiwa na rais Magufuli kuwa ni super man, nimemkumbuka naomba nimdurusu kidogo, niliwaji kusema nini humu kumhusu mtu huyu.

P.
 
Mpaka sasa kuna kila dalili kuwa mgombea urais wa CCM 2015 huenda akawa Edward Lowassa kutokana na nguvu ya kisiasa aliyonayo ndani ya CCM kwa sasa hususani kwa wajumbe wengi wa vikao vikuu vya juu vya maamuzi ndani ya CCM(Kamati kuu, Halmashauri kuu na Mkutano Mkuu).
Wakati huo huo kama kuna jambo wanachama wa CHADEMA wangependa kuliona basi ni Lowassa kuwa mgombea urais wa CCM 2015.
Kwa sababu zifuatazo:

1/Moja ya hoja zilizoipa nguvu sana na Umaarufu mkubwa sana CHADEMA ni Vita dhidi ya Ufisadi, Lowassa ni mtu anaaminiwa kama fisadi zaidi kuwahi kutokea ndani ya CCM, hivyo kutaipa nguvu zaidi CHADEMA katika harakati zao.

2/Kumbukumbu isiyofutika ya kitendo cha Lowassa kujiuzuru uwaziri mkuu kutokana na kuhusika katika Ufisadi mkubwa wa mkataba tata wa kampuni ya kufua Umeme wa dharura(Richmond).

3/Vita ya kufa na kupona kati ya Lowassa dhidi ya makundi mengine ya wanaCCM wenzie wanaoutaka urais pia, ambao wamekuwa kila mara wakianikana baadhi ya maovu yao hadharani. Katika hili atakosa 'Support' muhimu kutoka kwa wanaCCM wengine 'muhimu' wanaomchukia.
Mkuu Concrete, nimekutana mahali na Tanganyika TANU, anakusalimia sana!.
P
 
Wanabodi,

Baada ya kumsikiliza kwa makini Waziri Mkuu "Mstaafu", Edward Lowassa katika two- series za kipindi cha Dakika 45 cha ITV, kwanza nimemkubali sana huyu jamaa!, pili kama yeye ndiye angekuwa rais, ile 2005, Tanzania tusingefikia hapa tulipofikishwa sasa na utawala wa JK!, ila kikubwa zaidi, (kama ni kweli afya yake sio mgogoro kama anavyodai mwenyewe kuwa yuko fit, japo he looks sick!), CCM ikimsimamisha yeye kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, then matokeo ya urais kwa 2015, ni CCM tena!. Mkubali!..., mkatae!.

Hizi ni baadhi tuu ya sababu, kwanini CCM itashinda tena kwa ushindi wa kishindo kikuu, endapo and only if itamsimamisha Edward Lowassa!.

1. Uwezo wa Kusema, Kupanga, Kutenda na Kusimamia!.
Viongozi karibu wote waliopo CCM, wana uwezo mkubwa sana kesema!, tutafanya hiki, tutafanya kile!, ni maneno tuu! na pia wana uwezo mkubwa wa kupanga mipango kwa maneno tuu na sii matendo, au usimamizi, mfano mipanga kamambe kama (Mkukuta, Mkuza, Mkumbita, Mkurabita, na sasa Dira 2025)!. Mipango yote hii ni mizuri kwa maneno tuu, lakini wengi hawana uwezo wa kutenda na kusimamia utekelezaji!. Mipango mingi iliyopangwa, inaishia kwenye maneno na mabuku na makabrasha tuu, lakini utekelezaji kwa vitendo ni sifuri!. Kwa Edward Lowassa, yeye sio msemaji sana, bali ni mtendaji kweli!, yeye sio mtu wa maneno mingi!, ni mtu wa vitendo virefu!, he is an action oriented man!. Mfano hai ni pale alipokutana na madudu ya City Waters!, aliwafurusha there and then!. Hata madudu ya Richmond, alitaka kuwafurusha na kutaifisha kila kitu ila alishindwa!, kutokana na "mwenye mitambo!".

Tulipopata uhuru miaka ya 60, maadui wetu wakuu watatu, walikuwa ni Ujinga, Umasikini na Maradhi, na tulijiwekea misingi yetu mikuu minne ya maendeleo kuwa ili tuendelee, tulihitaji vitu vinne: Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora!. Kwenye hiyo misingi, tulisema Pesa sio msingi, pesa ni matokeo!, hili ndilol lililokuwa kosa pekee la Mwalimu, kutofautiana na misingi ya ukweli ya uchumi, kama ilivyofundishwa na Adam Smith (land, labor, capital na interpreneureship)!. Kwenye ile misingi minne tulisahau capital kwa kudai "pesa sii msingi!".

Watu tunao na ardhi ya kutosha, yenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, madini, maliasili etc etc tunazo. Tulikuwa na tatizo kidogo la utekelezaji wa siasa safi ya Ujamaa na Kujitegemea na uongozi bora, ndio maana nchi tulizopata nazo uhuru, ile miaka ya 60, wao wakiwa ni masikini wa kutupwa kuliko sisi, with nothing, kana Tiger nations, leo wako mbali!, sababu pekee iliyowafikisha wenzetu pale walipo, wakati sisi tunaendelea kupiga mark time ni Elimu!. Sisi tulitaja tuu kuwa Ujinga ni adui, lakini we never invested on Elimu because we had no capital!. Nyerere aligombana na maprofesor wa uchumi, Kina Prof. Rweyemamu, wakajitimkia zao, akagombana Edwin Mtei na IMF, WB etc matokeo sote tunayajua!.

Lowassa na timu yake ya Boys II Men, walipoingia tuu madarakani, EL akafanya study tour ya nchi tulizoanza nao wakati wa uhuru!, kwanini wao wamefanikiwa, wako mbali na sisi wametuacha nyuma sana!, akagundua wali invest kwenye elimu!. Akarudi nyumbani, akahamasisha kila kata iwe na shule ya sekondari ili kila Mtanzania apate kwanza elimu, mengine yote, yatafuatia!. Baada ya kujengwa shule, zilikuwa zipatiwe vifaa na waalimu wa kutosha!.

Baada ya kujiuzulu, serikali ya JK ikazi abandon zile shule za EL ili kumkomoa!. Sasa zinaitwa St. Kayumba!. Mpango wa kufundisha waalimu wa ukweli, ukaachwa, nanachukulia wale failures wenye Div IV karibu na zero, na kuwa brush kwa miezi mitatu! (Waalimu wa Voda Faster!). Jana alipozungumzia umuhimu wa kuwaelimisha kwanza watu wetu, amenigusa sana!. Tungekuwa tumeelimika, tusingeibiwa hivi madini yetu!, tunaibiwa madini yetu huku tunaangalia kwa sababu hatuna elimu ya madini!, sasa tumegundua gesi,serikali inakimbilia kugawa vitalu kwa umiliki wa miaka 99 huku Watanzania hatuna hili wala lile kuhusu elimu ya gesi, hatuna sera wala sheria ya gesi!. Kwa kifupi, hutujui lolote wala chochote kuhusiana na gesi!, na tutaishia kuibiwa tena gesi yetu kwa kukosa elimu ya gesi!. Edward Lowassa ameshauri, hiyo gesi tuiache kwanza!, lets invest kwenye elimu kwanza kwa watu wetu, ili kuwa empower hawa watu wetu kielimu ndipo tuingie kwenye ambitious projects kama za kuvuna gesi, au kilimo kwanza etc!.

Kwa hili pekee, CCM ikimsimamisha EL, Tanzania itapata ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.

Nimesema, CCM ikimsimamisha EL, 2015, itakuwa ni CCM tena, kwa sababu katika wapinzani wote, hakuna hata mgombea mmoja anayeweza kusimama na Lowassa kwenye urais wa 2015 na bado akaambulia kura!, there is no one!, none!.

Mwenye masikio na asikie!.

2. Dhambi Kubwa ya Lowassa ni Richmond Tuu!.

Najua wapinzani wa dhana ya ukweli, watakuja na hoja za dhambi kubwa ya Lowassa ni fisadi wa Richmond!, then time will tell, hiyo ni mizigo tuu ya watu, alijitolea kuibeba ili kwa kuteswa kwake, wao waokoke!, wakati muafaka ukifika, hili litawekwa wazi na Watanzania mtawafahamu wenye zigo lao haswa ni kina nani!. Wenye akili wameshang'amua ile metarmophosis process from Richmond -Dowans -Simbion na kwa msio jua, mkae mkijua Tanesco bado inailipa Simbion capacity charge ile ile ya dola 152 kama Richmond na Dowans, hivyo tumeruka majivu na kukanyaga moto, tumeruka maji na kukanyaga tope, na kwa usafi tumeruka nyasi, tukakanyaga ma..!.

3. CCM Haina zaidi ya EL na Upinzani hawana wa Kushindana Nae!.

Wanabodi ni mimi niliwahi kusema, CCM imechokwa na Chadema Haijajipanga, baadae nikasema CCM imechokwa mpaka basi!, Baada ya Chadema kuanza kujipanga nikasema Chadema, Njia Nyeupe Ikulu, lakini sasa baada ya kumsikia Edward Lowassa, kama ni kweli afya yake sii mgogoro kama anavyoonekana!, na CCM ikamsimamisha yeye, come 2015, then, mshindi wa uchaguzi wa 2015, ni CCM tena!, kinyume cha hapo, CCM ikimsimamisha mwingine yeyote, 2015, Chadema inachukuwa nchi kiulaini kama kumsukuma mlevi, unless kama CCM itamtosa Lowassa na kulisimamisha jembe lake pekee, John Pombe Magufuli, tatizo la Magufuli anaweza kuja kuwa dikiteta wa ajabu hadi hao CCM wenyewe wakajuta!.

Mwisho.
Namalizia kwa swali moja tuu, Jee CCM inaujasiri wa kuukubali ukweli huu mchungu wa kumsimamisha Edward Lowassa ili kuweza kujiokoa?! au itaendeleza kiburi uongozi na jeuri ya uchama tawala kusubiria kifo cha mende, kwa kufa huku inajiangalia kwa kutegemea itaendeleza uking'ang'anizi wake kwa kuamini this time pia itashinda tena kwa kuutumia uwongo ule ule, na mbinu zile zile za uchakachuaji ule ule, kwa matarajio katiba mpya pia ita provide opportunities za aina ile ile ya miaka ya nyuma, kuwa ita endelea "to fool all the people all the times?!.

Asante.

Pasco.

NB. Japo Pasco wa JF ni mwanachama wa Chama cha siasa, pia mshabiki wa wanasiasa mbalimbali, kwa CCM ni Pro Lowassa, kwa Chadema ni Pro ZZK na kwa CUF ni Pro-Jussa!.

Input ya Tanganyika Tanu.


Mkuu Tanganyika TANU (now Konkereti), pole sana, hii kitu yako imeunganishwa kwangu!. Ili kukutendea haki, nimeiweka kule juu kwenye main post.
Pasco.
Ingawa Lowasa asingefaa, lakini ya Magufuli wote tumeyashuhudia, alikuwa dikteta kweli mpaka ccm wenyewe akiwemo JK waliisoma namba na kujuta.
 
Wanabodi,

Baada ya kumsikiliza kwa makini Waziri Mkuu "Mstaafu", Edward Lowassa katika two- series za kipindi cha Dakika 45 cha ITV, kwanza nimemkubali sana huyu jamaa!, pili kama yeye ndiye angekuwa rais, ile 2005, Tanzania tusingefikia hapa tulipofikishwa sasa na utawala wa JK!, ila kikubwa zaidi, (kama ni kweli afya yake sio mgogoro kama anavyodai mwenyewe kuwa yuko fit, japo he looks sick!), CCM ikimsimamisha yeye kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, then matokeo ya urais kwa 2015, ni CCM tena!. Mkubali!..., mkatae!.
Pasco

He was an ideal president that never was!.
Kuanzia leo mpaka atakapo pumzishwa kwenye makao yake ya milele, as my tribute to this fallen hero, let's celebrate the life and the time of Edward Lowassa.

RIP Shujaa Edward Lowassa, umepigana vita vilivyo vitakatifu, imani umeilinda.
Bwana alileta Bwana ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.

Paskali
 

He was an ideal president that never was!.
Kuanzia leo mpaka atakapo pumzishwa kwenye makao yake ya milele, as my tribute to this fallen hero, let's celebrate the life and the time of Edward Lowassa.

RIP Shujaa Edward Lowassa, umepigana vita vilivyo vitakatifu, imani umeilinda.
Bwana alileta Bwana ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.

Paskali
Nasubiri tribute ya JK kwa ENL....sionfezi neno !! Nasubiri sana...!! Najua ENL hajaongea lolore kuhusu Richmond najua naamini amekufa nalo...subiri dhamira ya JK ...itamsuta ??
 
He was an ideal president that never was!.
Kuanzia leo mpaka atakapo pumzishwa kwenye makao yake ya milele, as my tribute to this fallen hero, let's celebrate the life and the time of Edward Lowassa.

RIP Shujaa Edward Lowassa, umepigana vita vilivyo vitakatifu, imani umeilinda.
Bwana alileta Bwana ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.

Paskali
Pole sana mkuu Pascal Mayalla kwa msiba huu mzito. Nifikishie salami zangu za pole kwa nguli kabisa Aboubakari Lyongo na timu nzima.

"He was an ideal president that never was!." [Not true].

"He was a hero" [Not true]

"He was a hero" + "on his own right" [True]

Alipigana "vita vilivyo vitakatifu", [Questionable]

"Imani ameilinda" [Questionable]

My take, like majority of Tanzanian politicians, Lowassa was dramatic, manipulative and opportunistic! His model of action had media house/s at its base.

He extensively used his performance art skills to dramatise and manipulate people.

Maisha yake ya kisiasa yanaacha maswali lukuki. Lakini mimi ni nani nisisamehe japo kusahau ni muhari?

Mwanga milele umuangazie ee Bwana, apumzike kwa amani mpendwa wetu. Amen
 
Nasubiri tribute ya JK kwa ENL....sionfezi neno !! Nasubiri sana...!! Najua ENL hajaongea lolore kuhusu Richmond najua naamini amekufa nalo...subiri dhamira ya JK ...itamsuta ??
JK asiposema yote kuhusu Richmond na ENL, lengo lao litakuwa ni nchi na watu wake wabaki kwenye hii vicious cycle ya ukosefu wa umeme generation after generation. Huu sio uungwana.

JK aseme ukweli uliobaki, nchi Ione inafanyaje kuvuka hapa. Hapo atasaidia pakubwa.
 
Edward Lowassa na Salim Ahmed Salim wajgefaa kuwa Marais wazuri sana katika nchi hii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom