Mzee Mwanakijiji,
Asante kwa kuja na mada nzuri kwa mara nyingine tena; Ningependa kuchangia katika maeneo makuu manne kama ifuatavyo:,
Kwanza ni muhimu tukatambua kwamba tofauti na CHADEMA, TANU haikuanza kama Chama Cha Siasa, bali a Nationalistic Movement; TANU iligeuka kuwa Chama Cha Siasa baadae; Kwa Chadema - ilianza kama Chama Cha Siasa na ni baadae sana Chama hiki kimekuja gundua umuhimu wa ku-incorporate elements za ‘Nationalistic Movement'; Tunaona uatmbuzi huo kupitia M4C; Kwa TANU, suala la M4C lilifanyiwa kazi mapema zaidi, hasa kupitia urithi wa TANU kutokea TAA; Tukumbuke kwamba TAA ilikuwepo Tanganyika kwa zaidi ya miaka 20 kabla ya ujio wa TANU. Ni vigumu kubaini iwapo TANU ingefanikiwa kutimiza malengo yake bila ya TAA; Kwahiyo hili suala la ‘Nationalistic Movement' Vis-à-vis ‘Political Party', pamoja na utofauti uliopo – in terms of effectiveness kuelekea kwenye mafanikio katika anga za kisiasa, ni eneo muhimu la kwanza kwa Chadema na wanachama wake to digest;
Pili, nje ya utofauti huu baina ya TANU na CHADEMA, kimsingi, vyama hivi vinafanana kwenye maeneo mengi, ingawa wapenzi wa Chadema hawapendi kusikia hili; Ni muhimu wanachadema wakagundua kwamba Chadema kukwepa kufananishwa na TANU itaendelea kuwa heri kwa CCM, vinginevyo CCM itaingia katika matatizo makubwa sana iwapo Chadema watatumia hoja kama vile:Sababu kubwa kwanini nchi Maskini ni kwamba CCM imesaliti historia yake yenyewe; Sisi Chadema sisi tupo hapa kufufua matumaini yenu ambayo kimsingi, mengi ni yale yale; Tofauti iliyopo labda ni kwenye tarehe na pia njia ya kufanikisha ndoto na matarajio yenu;
Kwa maana nyingine rahisi, ni muhimu Chadema wakagundua kwamba kufananishwa na TANU, For Chadema, this is a political asset than a political liability while the vice versa holds for CCM i.e. For CCM, it is more of a political liability than a political asset; Hii ni kwa sababu, the ‘Common Denominator' baina ya TANU na Chadema ni ile ile: A Growing demand for Change Among The Majority in Tanzania; Isitoshe, mwaka 1995, Nyerere alitamka ndani ya mkutano mkuu wa Taifa wa CCM Dodoma kwamba:
"Watanzania Wanahitaji Mabadiliko, Na Wasipoyapata Kupitia CCM, Watayatafuta Kupitia Chama Kingine."
Tatu, moja ya changamoto kubwa kwa Chadema katika nyakazi hizi ni jinsi gani wanaweza kutumia fursa iliyopo ambapo UMMA unahitaji mabadiliko ya haraka; Ni muhimu Chadema wakafahamu kwamba fursa hiyo kwa sasa ipo kupitia Chadema, LAKINI haina maana kwamba kiu hii ya mabadiliko itakufa na umma kuirudia CCM iwapo Chadema itawakatisha tamaa; UMMA umefikia hatua ya DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO, hivyo UMMA upo tayari kutafuta mabadiliko kupitia chama chochote cha siasa ambacho kitafanikiwa kuonyesha kwa vitendo kwamba ni mbadala wa kweli kwa CCM, lakini muhimu zaidi – ambacho kitakuwa tayari kuchukua mazuri ya CCM na kuachana na mabaya ya CCM;
Nne, kwa miaka zaidi ya 25 sasa CCM inatekeleza sera za uliberali, sera zile zile ambazo Chadema wataenda kuzitekeleza wakifanikiwa kuingia ikulu, tofauti kubwa ikiwa pengine ni tarehe; Isitoshe, itikadi ya Chadema ni Uliberali, huku itikadi ya CCM vitabuni ikiendelea kuwa Ujamaa kutokana na sensitivity ya kubadilisha hili, huku Chama kikiendelea kutekeleza sera za kiliberali, zile zile ambazo mzee Mtei alikuwa anahimiza na kutofautiana na Nyerere;
Kinachoimaliza CCM sasahivi na kuipa nguvu Chadema ni kwamba – CCM inatekeleza Uliberali katika mazingira tofauti na ya Ujamaa ambako nchi ilikuwa ina ‘a firm self – determined direction', nchi ilikuwa inamiliki its own development agenda, na pia maadili ya uongozi yalikuwa yanazingatiwa kwa vitendo; Katika hali ya sasa, nchi haina tena a self determined direction, nchi haimiliki tena its own development agenda (sasa ipo determined na World Bank, IMF, WTO…😉, na kilicho kibay zaidi, sera za uliberali zinatekelezwa katika mazingira ya Azimio la Zanzibar ambayo hayazingatii maadili ya uongozi kwa vitendo, hivyo kutengeneza mianya mingi sana ya Ufisadi;
Katika mazingira ya Sasa, Kiongozi akiamua kuwa msafi, basi ni kwamba tu anasukumwa na Uzalendo wake kwa Tanzania, lakini kama tunavyojua, Uzalendo pekee hautoshi, na hii sio kwa Tanzania tu, bali hata mataifa makubwa kama Marekani n.k yanayofuata mfumo wa kiliberali na ubepari ambapo individualism is the rule of the day; Kinachotenganisha private life na public life ya viongozi ni zaidi ya Uzalendo – ni uwepo wa maadili ya uongozi kwa mujibu wa Sheria zinazokuwa enforced na vyombo vyenye meno na pia independence from other organs of the state; Hapa ndio umuhimu wa katiba mpya unapoingia;
Vinginevyo tukiachana na mapungufu katika mfumo wetu wa utawala ambayo yanachangiwa sana na uhai wa Azimio La Zanzibar ambalo halina dira yoyote ya maana kukidhi matarajio ya wengi, mapungufu ambayo ndio yanaipa Chadema nguvu kubwa kisiasa i.e. VITA DHIDI YA UFISADI, nje ya hapo, kuna kila dalili kwamba Chadema ikienda Ikulu itaendeleza sera zile zile za Uliberali zinazotekelezwa na CCM hivi sasa, hasa ikizingatiwa kwamba itikadi ya Chadema ni Uliberali; Tofauti, again itakuwa ni tarehe, na pia efficiency hasa kwenye maeneo ya accountability n.k; lakini hili peke yake halitakuwa suluhisho kwa matatizo ya wananchi walio wengi, kwani hali zao hasa wale wa vijijini zitaendelea kuwa vile vile kutokana na inherent problems za uliberali katika mazingira ya nchi maskini;
Ni muhimu watanzania wakagundua kwamba, bila hata ya ufisadi, uliberali sio jibu kamili la kutatua matatizo ya wananchi walio wengi, na uliberali huu umechangia sana kuzorotesha maisha ya watanzania; Sababu kubwa ya hili kutokea ni kwamba – tofauti na enzi za Ujamaa, chini ya mfumo wa Uliberali, Serikali haina nafasi ya kuingilia nguvu za soko ili kulirekebisha pale linapoenda mrama na kuumiza wananchi walio wengi; Vile vile uliberali unaendeshwa chini ya nguzo kuu tatu: Privatization, Liberalization & Marketization;
Chini ya mfumo wa namna hii ambao Chadema wataenda kuupokea Ikulu kwa mikono miwili ni kwamba, uhalali wa serikali ni katika maeneo mawili tu: Kwanza, kusafishia foreign capital mazigira mazuri ya uwekezaji chini ya kanuni ya MGENI NJOO MWENYEJI APONE; Na pili, kuleta stability katika macro-economic environment, huku the most important goal of economic policy ikiwa ni kupunguza mfumuko wa bei; Hili sio tatizo, lakini tatizo linakuja pale ambapo sera za kudhibiti mfumuko wa bei haziendi sambamba na sera za kupunguza unemployment rate, na sera za kuleta economic growth ambayo ina trickle down to the masses kupitia improved welfare ya wananchi in terms of huduma za kijamii zilizokuwa bora, za bei nafuu na za uhakika;
Kanuni za uchumi zinahimiza umuhimu wa kushughulikia vitu hivi kwa pamoja: inflation, unemployment na economic growth, na hivi ndivyo nchi tajiri hufanya na kufanikiwa kuletea wananchi maisha bora, lakini katika nchi zetu, wakubwa hawa kupitia World Bank, IMF, WTO, ambao ndio wamiliki wa ‘our development agenda', kamwe hawalengi kufanya hivyo, kwani itakula kwao kwa maana ya kwamba – kutokomeza umaskini ni hasara kwao; Mbali ya suala la inflation, uhalali wa serikali chini ya mfumo huu unabakia pia katika fiscal and monetary policy discipline, hasa kupitia taxation, privatization na kupunguza matumizi ya serikali bila ya kujali ni katika maeneo gani; Economic deregulation, liberalization ya domestic financial system, liberalization ya capital account, formulation ya legal system inayokinga property rights n.k; Haya yote yanaonekana kuwa na GOOD FACE VALUE, lakini hayana INSTRINSIC VALUE kwa wananchi walio wengi kwa sababu yanatekelezwa kwa matakwa ya mataifa makubwa, na pia kinyume na jinsi mataifa haya yanavyotekeleza kwao; Ningependa kujadili haya kwa undani lakini naona hapa nitaenda nje ya mada;
Kwa mtazamo wangu, hizi ni baadhi ya changamoto kubwa zinazoikabili Chadema, na hata ikiingia ikulu, itakuwa inaingia kwa njia iliyotegenezwa na 'trays za mayai'; Bila uangalifu na umakini wa hali ya juu, wananchi watakata tamaa na Chadema ndani ya kipindi kifupi sana; CCM taratibu inaanza kukubali matokeo kwamba nguvu ya Chadema haiepukiki, Kwahiyo inaanza kuwekeza katika njia hii ya Chadema ya kwenda ikulu iliyojengwa kwa zege la tray za mayai;