Kudhulumiwa na mtu unayemuheshimu

Kudhulumiwa na mtu unayemuheshimu

Pesa ni shetani mkuu hata Mimi imewahi kunitokea nikadhulumiwa na MTU niliyekuwa namkubali sana kumuheshimu sana.

Akachukulia udogo wangu kama fimbo ya kunichapia alafu akanijibu hakuna mkamilifu. Kufupisha story pesa zangu alilipa na tukikutana yeye ndio hunipa heshima. Mshenzi sana yule nilimnyoosha akanyooka
 
Inapokuja ishu ya pesa hakuna anayestahili kuaminiwa. roho yangu inaniuma sana tena sana kwa mtu ambaye niliweka trust kwake kunipiga pesa ambayo kimsingi nilistahili kuipata kwa kuzingatia energy na time niliyowekeza katika kuhakikisha kila kitu kipo undercontrol.

Kuna roho inaniambia nikae kimya nimuachie mungu lakini roho nyingine inaniambia huo ni Ujinga kila nikifikiria amount aliyonipiga natamani kulia.

Wakuu najua hayawahusu ila nimeona niandike hata humu atleast nipate relief nipo namuandalia waraka hata kama hatonipa hiyo pesa hajue nimeumia sana tena sana.
Braza sikujui wala sijui umetapeliwa sh ngapi ila nina ushauri mmoja. Muombe Mungu neema ya kusamehe. Ukiiomba anakupa kabisa bila wasiwasi.

Samehe kwa moyo mmoja na kama ni mtu ambae umemzoea mwambie nimekusamehe na maanisha. Ukiwa na uwezo huo tu mara umalizapo tu Mungu huanzia hapo hapo kukulipizia kisasi.

Yeye anajua kipimo cha enegy na effort uliyoiweka na maumivu uliyoyapata. Ukishamaliza kusamehe mdai Mungu urudishiwe na yeye.

Huwa ukisamehe kwa uaminifu na yeye hurudisha ulivyopoteza vyote ikiwa utadai. Usipodai faili linaweza lisifunguliwe leo likafunguliwa kwa ajili ya watoto wako ila dai baada ya kusamehe na kusahau.
 
Marafiki wa kibongo sio. Niliwakopesha, kudai changu sikulipwa. Nikabadili formation ya kudai kwa kuwakopa ile kuwaektia nimekwa napo sikukopeshwa. Marafiki wa kibongo ni wakubishana nao mpira tu.
Vitu viwili vya kuvuruga urafiki wa wanaume, ni Pesa na kuibiana mademu.

Kuna mwana homeboy, wakat huo niko naenjoy hela ya HESLB nilimkopa pesa ndefu tu. Kwao life halikuwa zuri hivo pesa ya boom akawa anagawia na home.

Issue inakuja yanapita kama maboom ma3 mzee yuko kimya na hela yangu hanipi.

Kumdai naona soo, tunatoka wote sehem moja na tunaishi room moja, nikajitahdi tu kumueleza kwa sms ,mzee vp ile hea mbona maboom ndio yanaishia afu kaa kimya vile. Aaaah story zikawa nyingi ila alinirudishia sicne then sijawahi muamini kwenye pesa,
 
Halafu alivyo hana aibu mwenzi wa saba alinipigia simu nimkopeshe laki nne yaani nilitamani nimtukane😬😬
Kweli hana aibu au alikua anakuchora, ungemwambia kwenye ile hela nayokudai chukua hapo laki nne 😅.

Niliwahi kumwambia jamaa yangu hivyo mbona baada ya kutatua shida iliyokuwa inamsumbua akanilipa hela yangu kidogo kidogo.
 
Anasema hivyo kwa kuwa anajua siwezi na sio kwamba siwezi bali Mama hapendi kutuona tukigombana na ni mtu mwenye presha vinginevyo ningempeleka police[emoji51]
Ana umri huyo dada yako?

Hana bwana?

Kama ana bwana yeye anaenda kununua kiwanja kimsaidie nini?

Si wapambane na bwana ake watafute vyao?

Na wewe kwa nn haujamshirikisha mama na baba ili waliweke sawa hili suala!

Kudhulumiana ndani ya familia ipo sana hasa kaka na dada wanapenda kupiga vizinga kwa gia ya kukopa, vi laki 1 mpaka 5 ni kawaida. Ila hii ya milioni 5 hapana, hautakiwi kukaa kimya.
 
Kweli hana aibu au alikua anakuchora, ungemwambia kwenye ile hela nayokudai chukua hapo laki nne 😅.

Niliwahi kumwambia jamaa yangu hivyo mbona baada ya kutatua shida iliyokuwa inamsumbua akanilipa hela yangu kidogo kidogo.
Hakuwa ananichora alikuwa na shida kweli,Mkuu katika maisha yako ogopa sana dhuma ni mbaya yaani uta andamwa na mikosi kila siku.
 
Yaani unanikumbusha deni langu nna watu nilikuwa nawadai kwa vipind tofaut tofauti sasa kipindi kimefika nataka hizo hela zinipe support....
Mkuu nakushauri.

Kamwe Usithubutu kumkopesha Hela mwafrika hasa mtanzania.

Tena kiasi kikubwa cha pesa, Usithubutu

Mimi hata mtu anililie shida kiasi gani siwezi kumkopa.

Nitampa kiasi kidogo tu, kama msaada,Baada ya hapo kila mtu apite na hamsini zake.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Ana umri huyo dada yako?

Hana bwana?

Kama ana bwana yeye anaenda kununua kiwanja kimsaidie nini?

Si wapambane na bwana ake watafute vyao?

Na wewe kwa nn haujamshirikisha mama na baba ili waliweke sawa hili suala!

Kudhulumiana ndani ya familia ipo sana hasa kaka na dada wanapenda kupiga vizinga kwa gia ya kukopa, vi laki 1 mpaka 5 ni kawaida. Ila hii ya milioni 5 hapana, hautakiwi kukaa kimya.
Ana Mume,Kesi ilifika kwa Mama maana ni mzazi pekee tuliyebaki nae kauli yake ni samehe utapata nyingine.
 
Ukiona nimekukopesha pesa ujue hiyo pesa niko tayari kuipoteza na incase ukitokomea nayo tunakuwa maadui kuanzia siku hiyo, unaweza usione baya lolote nitakalo kufanyia ila jua kamwe sintokuja kukusaidia katika jambo lolote linalohusu fedha hata uwe na shida namna gani
Noted[emoji3578][emoji122]

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Ishu nilimuachia afanye negotiation na watoa huduma fulani afu mimi ni focus na kazi sasa amount aliyokuja kuniambia mimi nikakubali sasa katika kuuliza na kutaka kujua ile huduma ina cost kiasi gani nimegundua jamaa kaninyoosha pakubwa sana.
Kama ni hivyo hajakudhulumu! Amekula udalali nadhani potezea tu ingawa hakupaswa kukufanyia hivyo.
 
Back
Top Bottom