Kudhulumiwa na mtu unayemuheshimu

Kudhulumiwa na mtu unayemuheshimu

Baada ya kujua kuwa naweza kosana na marafiki au ndugu kisa pesa, nikiombwa mkopo naangalia kiwango ambacho hata nikidhulumiwa siwezi umia ndiyo nampa.

Akirejesha ni yeye asiporejesha pia safi
 
Huu uzi nimeuona muda mbaya sana.. kuna jamaa hapa anataka nimuazimishe kama 200k hivi.. mwisho wa huu mwezi atanipa.

Sasa.. mbona kama naanza kuogopa ogopa.. maana hapo ni kilo 20 za sato hizo. Kulaleki.
 
Pole sana, kuna watu sio waaminifu na ni matapeli wa chini chini.
Mtu unamuamini na kumsaidia anapokwama ila wakati wa kurudisha anajizima data.
Ahahaa Mimi huwa sisahau kama nadaiwa hata ipite miaka mingapi, sijui watu inakuwaje wanasahau kuwa wadaiwa.

Mmoja mwaka jana nimeokota vijisenti vya sensa, akaniomba mkopo nikampa. HAKURUDISHA.

Imepita miezi kadhaa, hatuongei ananipigia simu akaanza mbali story nyingi, akaomba tena mkop kwamba kapata ajari mataa ya mwenge, bodaboda imeharibika na ameporwa simu etc.

Wakati huo alikuwa kanipigia kwa namba ngeni, NIKAMKATAA TU sina hela nikampa pole
 
Ukiona nimekukopesha pesa ujue hiyo pesa niko tayari kuipoteza na incase ukitokomea nayo tunakuwa maadui kuanzia siku hiyo, unaweza usione baya lolote nitakalo kufanyia ila jua kamwe sintokuja kukusaidia katika jambo lolote linalohusu fedha hata uwe na shida namna gani
👏🏾👏🏾👏🏾 usiporejesha, umejipa redcard
 
Back
Top Bottom