comte
JF-Expert Member
- Dec 11, 2011
- 8,226
- 5,948
PhD iwe ya kuingia darasani na kutoa andiko, kutoa andiko, au ya heshima zote zina sifa moja inayofanana. Sifa hiyo ni kutunukiwa na chuo husika baada ya kutimiza vigezo na masharti yao.
Walio na PhD baada ya kuingia darasani na kutoa andiko au kutoa andiko huenda mbele ya chuo husika na kusema tazama kama nimefikia vigezo. Kwa maneno mazuri hawa wanatimiza msemo wa kiswahili kibaya kinajitembeza au ukitaka cha uvunguni sharti uiname.
Kusema ukweli walionazo hizo PhD wanajitembeza na wanajitembeza kweli kwa unyenyekevu mkubwa mbele ya wahadhiri na wasimamaizi wao. Kwa upande mwingine wanaopewa PhD za heshima hutambuliwa na kuitwa na vyuo husika na kuambiwa tumeona unachofanya, umekidhi vigezo vyetu kwa hilo tunakuheshimu hivyo juu tukupe PhD ya heshima. Kwangu mimi hawa ndio wasomi wa kweli na wasomi bila sababu na wanatimiza msemo wa kizuri chajiuza chenyewe.
Zimetolewa lugha za kebehi ikiwemo kuwa wenye PhD za heshima wamezinunua kana kwamba wao waliosoma darasani hawakulipa ada ambayo ni sawa na kununua tu. Hii tabia ya kujigawa katika makundi ya wao na sisi imetamalaki sana.
Mfano wa Dar es Salaam wanawaita wengine wa mikoani kama kwamba Dar es Salaam siyo mkoa; waliosoma nje wanajiona bora kuliko waliosoma hapa ndani kama kwamba what is biology inajibiwa tofauti kati ya nje na ndani ya Tanzania. Kwa hapa Tanzania waliosoma UDSM wanajiona bora kulimo waliosoma vyuo vingine vya ndani; na wabunge wa majimbo wanajiona bora kulilo wabunge wa vitu maalumu.
Sasa huu ujivuni na kebehi umehamia kwenye PhD- kwangu ni kheri kuwa na PhD ya heshima kwa kununua kuliko PhD ya kunyenyekea wahadhiri wakutoe tena wakati mwingine kwa kutoa rushwa.