Kudandia Mafuso kukamponza binti wa Kifaransa……………! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kudandia Mafuso kukamponza binti wa Kifaransa……………!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Feb 16, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  profimedia-0015321356.jpg
  Dereva Roger Bouvier

  imagesCA5O30LT.jpg

  Ramani ya Tunnel lilipopita

  CELINE 003.jpg
  Celine Figard

  BERNARD FIGARD.jpg
  Baba wa Celine Bernard Figard

  Nimelazimika kuweka huu mkasa leo hii siku ya Alhamisi kwa sababu kesho Ijumaa nasafiri kwenda huko Kilwa Kipatimo na nimeambiwa huko hakuna Network kabisa.


  Mnamo Desemba 1995, Celine Figard binti wa Kifaransa aliyekuwa na umri wa miak 19 wakati huo na mwanafunzi wa uhasibu ambaye alikuwa akiishi na wazazi wake katika kijiji cha ferrieres-Les-Scey kilichopo mashariki mwa Ufaransa, alifunga safari kwenda nchini Uingereza ambapo alipanga kula sikukuu ya Krismasi na binamu yake ambaye alikuwa kiishi na kufanya kazi nchini humo.

  Mwaka mmoja nyuma, Celina alikwenda nchini humo na kuungana na mjomba wake katika kipindi cha majira ya joto ambapo pia alipata fursa ya kujifunza Kiingereza na hasa matamshi ambayo yalikuwa yakimpa tabu sana kutokana na mazingira aliyokulia.Safari hii pamoja na kula sikukuu ya Krismasi na binamu yake lakini pia alikusudia kuitumia kama nafasi nzuri ya kukinoa kiingereza chake.

  Kila mwaka maelfu ya vijana kati ya nchi hizi mbili, yaani Ufaransa na Uingereza hutumia njia ya barabara ipitayo katika daraja la chini ya bahari kwenye mkono wa bahari ya Atlantic unaotenganisha Uingereza na Ufaransa, kutembelea nchi nyingine. Njia hii hutumiwa na vijana wengi ambao husafiri na malori ya mizigo ambayo ndiyo yanayotumia njia hiyo kusafirisha mizigo kati ya nchi hizo mbili, hivyo kwa malipo kidogo huwawezesha vijana hao kusafiri kuingia nchini Uingereza au Ufaransa, wenyewe huita Hitching a ride.

  Ili kuhakikisha kuwa binti yao anasafiri kwa usalama zaidi kwa utaratibu huo wa kutumia malori, wazazi wake walimuomba dereva mmoja rafiki wa familia hiyo aitwae Guy Mailot ambaye alikuwa anasafiri kwenda nchini Uingereza ili asafiri na binti yao. Dereva huyo aliwakubalia na siku ya safari ilipofika waliondoka nchini Ufaransa mapema na ilipofika usiku walikuwa wameshafika kwenye ukingo wa bahari ambapo ndipo daraja hilo la chini ya bahari linalozitenganisha Uingereza na Ufaransa linapoanzia, Mailot na Celine waliamua kulala ndani ya gari wakisubiri kupambazuke ili wavuke na kuingia nchini Uingereza.Ilipofika asubuhi, walisafiri kupitia daraja hilo la chini ya bahari na kuingia nchini uingereza.

  Mailot alimuombea binti huyo lifti kwenye lori jingine lilokuwa likiendeshwa na na dereva mwingine raia wa Ufaransa aliyejulikana kwa jina la Roger Bouvier, kwa sababu Mailot alikuwa haendi kwenye njia ambayo Celine alikuwa akielekea. Wakiwa na dereva huyo, walisafiri hadi katika mji mwingine uitwao Chieveley Barkshire, ambapo ndipo celine angepokelewa na binamu yake. Roger alimshusha Celine ambapo alikwenda kwenye kibanda cha simu kulichokuwa karibu na kumpigia binamu yake simu ili kumjulisha kwamba ameshafika, lakini kutokana na kupiga namba ambayo haikuwa sahihi, Celine alishindwa kupata mwenyeji wake ambaye alikuwa anafanya kazi kwenye Hoteli moja iitwayo Southampton.

  Kwa hiyo aliamua kuomba lifti kwenye lori jingine linaloelekea katika eneo ilipo Hoteli hiyo. Hivyo Celine aliagana na Roger na kudandia lori jingine aina ya Mercedes-Benz ambalo lilikuwa likiendeshwa na dereva mmoja mtu mzima aliyekuwa na ndevu zenye rangi ya damu ya mzee na kuondoka naye. Huo ndio ulikuwa mwisho wa Celine kuonekana akiwa hai. Mnamo siku ya Jumatano ya Desemba 27, 1995, ikiwa ni siku saba tangu Celina kupotea, baba yake alisafiri hadi nchini Uingereza kuomba msaada kwa wananchi wa nchi hiyo kupitia kwenye vyombo vya habari hususan runinga.

  Baba wa binti huyo Bernard Figard aliwaomba raia wa nchi hiyo kusaidia kumtafuta binti yake huyo aliyepotelea kusikojulikana. akiongea na vyombo vya habari, kwa maneno yake mwenyewe mzee huyo alisema, ‘mtu yeyote aliye na taarifa kuhusu mahali mwanangu Celine alipo atujulishe au atoe taarifa kwenye vyombo vya usalama, pia ningependa kukuomba mwanangu mpendwa Celine kama unatusikia au unatuona kupitia runinga, huko ulipo, basi tunakuomba ujitokeze.’
  Mahali pa kuanzia ambapo Polisi walikuwa na uhakika kama, kungewawezesha kujua mahali alikopotelea binti huyo ni kulipata lori aina ya Mercedes-Benz jeupe ambalo ndilo Roger alimuona Celine akilipanda ambalo lilikuwa likiendeshwa dereva mwenye ndevu zenye rangi.

  Kwa mujibu wa maelezo ya Roger, alipokuwa akihojiwa na Polisi kuhusu kumfahamu dereva aliyempakia Celine kwa mara ya mwisho, alikiri kutomfahamu dereva huyo na pia alidai kwamba hata muonekano wake ulikuwa ni wa kutiliwa mashaka. ‘Hakuonekana kuwa mtu mwema.’ Alisema Roger.
  Lakini hata hivyo kulikuwa na ugumu wa kulipata lori hilo na dereva wake kutokana na kuwepo kwa mamia ya malori nyenye rangi hiyo yanayotumia barabara hiyo ya kuingia nchini uingereza. Hata hivyo, msemaji wa Polisi ambaye ndiye aliyekuwa na jukumu la kuongoza upelelezi wa kesi hiyo, Des Thomas, aliwahakikishia waandishi wa habari kwa kuwaambia, ‘hakuna mashaka kuwa tutamkamata dereva wa lori hilo, ingawa hatudhani kwamba tutamkamata kwa wakati ili atufahamishe alikompeleka Celine.’

  Siku mbili baadae tangu msemaji huyo atoe taarifa yake kwenye vyombo vya habari kuhusiana na mwenendo mzima wa kumtafuta Celine, mwili wake uliokotwa ukiwa uchi wa mnyama kando ya barabara, takriban kilomita 144 kutoka mahali alipopandia lori aina ya Merecedes-Benz jeupe. Uchunguzi wa awali ulionesha kwamba alikuwa amebakwa, kupigwa pamoja na kunyongwa shingo hadi kufa.Hakukuwa na dalili ya kuonekana kwa nguo zake na begi pamoja na vitu vyake vingine alivyosemekana kusafiri navyo. Hiyo ilidhihirisha kwamba, aliuawa mahali pengine siku chache zilizopita na kisha kuletwa na kutelekezwa pale.

  Mara baada ya mwili wa Celine kupatikana iliwachukuwa Polisi wa upelelezi saa moja kuanza upelelezi kwa kumhoji dereva mmoja aliyejulikana kwa jina la Stuart Morgan aliyekuwa na umri wa miaka 37 wakati huo, ambaye alikuwa akiendesha lori lake mwenyewe aina ya Mercedes-Benz jeupe ambalo lilikuwa likifanana kabisa na lori lililosemekana kufanana na lile lililompakia Celine kwa mara ya mwisho.
  Morgan alihojiwa na Polisi mnamo Desemba 31, 1995 akihusishwa na mauaji ya Celine ambapo alikanusha kuhusika na mauaji hayo. Morgan alikuwa ni mmojawapo wa wamiliki wa malori 1200 aina ya Mercedes-Benz yenye rangi nyeupe yaliyosajiliwa nchini Uingereza waliohojiwa tangu ulipopatikana mwili wa binti huyo.

  Si kwamba Polisi wa upelelezi walimhoji Morgan kwa sababu ya kumiliki lori aina ya Mercedes-Benzi jeupe, bali ni kwa sababu alikuwa na ndevu zenye rangi ya damu ya mzee ambazo zilionekana kufanana kabisa na ndevu zilizotajwa na Roger dereva aliyemshusha Celine kwa mara ya mwisho kabla hajapanda lori hilo jeupe aina ya Mercedes-Benz. Ingawa alikuwa amezinyoa siku ya Krismasi, ikiwa ni baada ya Roger kutoa maelezo ya kumtambua mtu aliyempakia Celine kwa mara ya mwisho kuwa alikuwa na ndevu zenye rangi ya damu ya mzee, lakini hiyo haikusababisha Polisi kutozitambua ndevu zake ambazo zilikuwa zimeanza kuota.

  Mnamo Januari 21, 1996 Celine alizikwa kijijini kwao nchini Ufaransa ambapo maelfu ya waombolezaji waliungana na familia yake katika mazishi ya mpedwa wao. Siku hiyo hiyo ya mazishi, huko nchini Uingereza, Polisi walimkamata kwa mara nyingine Stuart Morgan na kumhoji kuhusiana na mauaji ya Celine. Morgan alikanusha kabisa kuonana na Celine, hata hivyo safari hii Polisi walimuomba atoe vipimo vya DNA, kwa ajili ya kuvifananisha na vile vilivyopatikana kwenye mwili wa Celine ambavyo ilisemekana kuwa huenda vikawa ni vya muuaji.Polisi wa upelelezi walikuwa wameweka mkakati wa kuchukua vipimo vya DNA kwa madereva wote waliowahoji wanaoendesha malori aina ya Mercedes-Benz yenye rangi Nyeupe pamoja na kuchukua vipimo kwenye kifaa maalum kinachofungwa kwenye magari kwa ajili ya kurekodi mwenendo wa gari (tacograph).

  Hata hivyo, Morgan ambaye alikuwa akilindwa na sheria inayompa hiyari ya kuamua kutoa vipimo kutoa vipimo au la, kwa kujibu wa sheria za nchini Uingereza , alikataa kutoa vipimo vya DNA pamoja na vile vya tacograph. Kwa muda wa wiki tatu mfululizo, Morgan alikuwa kikamatwa na kuhojiwa kwa nyakati tofauti katika vizuizi vya Polisi vilivyowekwa mahususi kwa ajili ya kumsaka mtuhumiwa wa mauaji ya Celine Figard.Kuna wakati Morgan aliwahi kmweleza rafiki yake kwamba, kuna siku alikamatwa na kuhojiwa na maofisa wa Polisi akihusishwa na mauaji hayo zaidi ya mara 14, lakini polisi hawakupata ushahidi wa kina wa kumtia hatiani.

  Ni pale alipojitokeza dereva mwenzake wa malori aliyewadokeza Polisi kwamba Morgan alinyoa ndvu zake mapema siku ya mkesha wa Krismas, ndipo Polisi wa upelelezi walipomkamata mnamo Februari 17, 1996.
  Siku hiyo aliyokamatwa Polisi walikwenda nyumbani kwake katika eneo la Poole, eneo lilipo katika viunga vya Dorset na kuendesha uchunguzi katika nyumba yake. Katika uchunguzi wao Polisi walikuta picha na Barua za Celine zikiwa zimefichwa kwenye eneo la bustani. Pia polisi walikuta busati dogo la kwenye gari ambalo lilikuwa limefichwa kwenye gereji ya kuhifadhia gari ambalo lilikuwa na matone ya damu. Sambamba na hilo, Polisi pia walikuta matone ya damu kwenye gari lake ambapo yalipopimwa ilikuja kudhihirika kwamba, ilikuwa ni damu ya Celine.

  Ili kujiridhisha zaidi ilibidi Polisi waitishe gwaride la utambulisho ambapo Roger Bouvier alimtambua Morgan kuwa ndiye aliyempakia Celine kwa mara ya mwisho baada ya yeye kumshusha. Ushahidi mwingine uliopatikana ulikuwa ni wa chupa mbili za mvinyo ambazo zilikuwa ni adimu sana nchini Uingereza za aina ya Pascal Chretien, mvinyo huo ulikuwa ni wa Celine aliopewa zawadi na muuza duka la mvinyo nchini ufaransa walipokuwa njiani kuelekea nchini Uingereza wakati huo akiwa na dereva wa kwanza kumchukua kwa wazazi wake, Guy Maillot.

  Chupa hizo mbili za Mvinyo Celine hakuzinywa njiani, bali aliamua kwenda nazo nchini Uingereza ili ampe binamu yake zawadi kwa ajili ya Krismas. Polisi walikuja kugundua kwamba, mara baada ya Celine kutoweka, Morgan alimpa jirani yake anayemiliki karakana ya kutengeneza magari iliyoko mkabala na nyumbani kwake ambapo ndipo anapoegesha gari lake, chupa mbili za mvinyo ambazo zinafanana kabisa na zile ambazo Celine alipewa zawadi.

  Alipouzwa na Polisi ni wapi alikozipata zile chupa za mvinyo, Morgana alijibu kuwa alizinunua njiani. Safari hii Polisi hawakuwa na shaka kabisa na ushahidi walioupata, hivyo walimfungulia Morgan mashtaka ya kuhusika na mauaji ya Celine. Mnamo Oktoba 1996, Stuart Morgan alifikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya kuhusika na mauaji Celine Figard. Kwa mujibu wa maelezo yaliyosomwa na mwendesha mashtaka pale mahakamani aliyejulikana kwa jina la David Farrer, alisema kwamba, mnamo Desemba 1995, mara baada ya Morgan kumpakia Celine katika kituo cha mafuta, alimbaka akiwa ndani ya gari lake kisha kumpiga na kumnyonga mpaka kufa.

  Mwendesha mashtaka huyo aliendelea kubainisha kwamba, kwa takriban siku kumi Morgan alikuwa akiendesha gari lake huku akiwa ameulaza mwili wa Celine kwenye Kitanda kilichopo ndani ya gri lake, huku akitafakari namna ya kuutelekeza mwili wa binti yule bila kujulikana.
  Kumbuka kwamba, mwezi wa Desemba ni kipindi cha baridi kali sana kiasi cha barafu kutanda hadi barabarani nchini Uingereza, hivyo haikuwa rahisi kwa mwili wa Celine kuharibika ukiwa ndani ya gari. Hivyo Morgan alisherehekea sikukuu ya Krismas na familia yake huku akiwa ameegesha gari lake mita chache kutoka nyumbani kwake likiwa na maiti ya Celine ndani.

  Kuna wakati alifikia hatua ya kununua msumeno na beleshi ambapo mwendesha mashtaka alimtuhumu kwamba lengo lake lilikuwa ni kukatakata mwili wa Celina na kuuzika bila kujulikana, lakini alisita kutekeleza wazo hilo, hivyo mnamo Desemba 29, 1995 alikata shauri kuutelekeza mwili huo kando ya barabara asubuhi na mapema na ndipo ukapatikana.
  Katika utetezi wake Morgan alidai kwamba ni kweli alimpakia Celine katika kituo cha mafuta cha Chieveley mnamo Desemba 19, 1995, lakini alikanusha kuhusika na mauaji. Morgan alikiri kufanya mapenzi na Celine ndani ya gari lake baada ya kumpa chai na kumwambia, ‘chai hii itakugharimu busu la Krismas.’

  Morgan aliendelea kudai kwamba baada ya nusu saa tangu ampakie alimfikisha mahali alipokuwa akienda na kumshusha akiwa salama na kuondoka zake. Alipoulizwa ilikuwaje vitu vya Celine vikutwe nyumbani kwake tena vikiwa vimefichwa, Morgan alijibu kwamba, Celine alisahau begi lake liliokuwa na chupa mbili za mvinyo, barua pamoja na picha zake kwenye gari. Alipata mshtuko baada ya kusikia kwamba Celine ametoweka na anatafutwa na wazazi wake, pia hakutaka mkewe ajue kuwa alifanya mapenzi na mwanamke mwingine, hivyo aliona ni busara kutupa ule ushahidi. Alipoulizwa kama anakawaida ya kufanya mapenzi na wanwake wanaotumia usafiri wa malori, maarufu kama Hitch a Ride, Morgan alikubali kuwa ana kawaida hiyo.

  Kwa maneno yake mwenyewe Morgan alisema, ‘ndiyo ninao udhaifu huo wa kufanya mapenzi na wanawake ninaowapakia kwenye gari langu.’ Alipoulizwa tena kuhusiana na matone ya damu yaliyokutwa kwenye busati la gari lake, Morgan alidai kwamba, matone yale ni ya dereva mwenzake aliyekuwa amejikata mguu kwa bahati mbaya.
  Mnamo Oktoba 16, 1996, Morgan alipatikana na hatia ya kumuua Celine Figard na kukumiwa kifungo cha maisha jela. Hata hivyo, mwendesha mashtaka alitangaza kuwa mamlaka ya Polisi wataendelea kumhoji Morgan kuhusiana na kesi nyingi za wanawake waliopoteza maisha katika mazingira kama ya Celine.

  Nao wazazi wa Celine, Bernard Figard na mkewe Martine Firgard ambao katika kipindi chote ambacho kesi ya mauaji ya mtoto wao ilipokuwa ikisikilizwa walikuwa nchini Uingereza wakifuatilia kesi hiyo, hawakuridhika na hukumu hiyo. Alipoulizwa kama angependa kulipiza kisasi kwa muuaji wa mwanae, Mzee Figard kupitia kwa mkalimani alikanusha kutaka kulipiza kisasi, kwani alidai kwamba, hakuna kitakachomrejeshwa mwanae duniani midhali ameshafariki, ingawa alikiri kutoridhishwa kwake na hukumu ya kifungo cha maisha kwa watuhumiwa wa mauaji kama Morgan.

  Hata hivyo Mzee Figard alionyesha kusikitishwa kwake na kitendo cha yule dereva wa lorry la pili Roger Bouvier kumuacha Celine apande lorry la Stuart Morgan wakati alishamtilia mashaka kutokana na mueonekano wake. Kwa maneno yake mwenyewe Mzee Figard alisema, ‘kama hakumuamini, kwa nini hakufanya Juhudi zozote kumzuia mwanangu kupanda lorry hilo?’ Na alipoulizwa kama yeye na mkewe wanajisikiaje baada ya kumpoteza binti yao, Mzee Figard alijibu, ‘tumeikubali changamoto hiyo, na bado tuna wajibu wa kuwalea watoto wetu watatu waliobaki.’ Aliwataja watoto hao kuwa ni Stephane, Nicolas na Karine.
   
 2. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,309
  Likes Received: 974
  Trophy Points: 280
  Mkuu, huu mkasa unasikitisha sana, tunamuombea kwa mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu celine figard.
   
 3. Typhoid

  Typhoid JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa tulio na watoto hii inatupa changamoto ya kuwa makini sana na wanetu hasa linapokuja suala la nani amuangalie mwanao kipindi haupo!
   
 4. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mbaya sana! Lo!
   
 5. JS

  JS JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2012
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Lift za usiowajua si nzuri ni bora utembee mara mia au upande mabasi hata kumi kuliko lift hizi. RIP Celine
   
 6. L

  LISAH Senior Member

  #6
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Gustavo!
  Kwakweli inasikitisha but i like your threads .
  Wasalim Kilwa.
   
 7. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  hii story inanikumbusha yule dada aliyelazimishwa kumnyonyesha kobe......
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Huu mkasa unasikitisha kwa kweli.
   
 9. n

  ngony Senior Member

  #9
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 153
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  inasikitisha sana.
   
 10. L

  Luluka JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  That very sad jaman!
   
 11. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Darasa kubwa hili!
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Baada ya kukisoma kisa, naona ungeandika ukweli, kudandia mabenzi...

  Unapotosha kutia uongo kwenye kisa cha kweli. mwandishi wa magazeti ya udaku hajifichi.
   
 13. ummu kulthum

  ummu kulthum JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 2,791
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  inatia uchungu jamani!
   
 14. vanmedy

  vanmedy JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 2,245
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Heart touching storry... Na wewe safalfari njema huko uendako
   
 15. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Nawe uwe makini na lifti huko uendako
   
 16. nimie

  nimie JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Imeniuma sana, simply like that! Mungu atusaidie ktk usalama wa watoto.
   
 17. Jt jr

  Jt jr Senior Member

  #17
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 182
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  duh! Inaonekana celine alikuwa mzuri sana, Lnp celine.
   
 18. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Du!RIP Cellina.
   
 19. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,108
  Likes Received: 6,581
  Trophy Points: 280
  midomo imenikauka, lol,
  R.I.P. Celine.
   
 20. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #20
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
  Heh!! Ipi hiyo?
   
Loading...