Kudai barua ya ajira kabla ya kulipwa mafao

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,590
4,277
Kutokana na maendeleo ya Technologia, ambapo zipo njia za kuaminika zaidi za kumtambua mtu; napendekeza Sheria ya Kudai mzee aliyekuwa mfanyakazi pengine kwa miaka 30 alete barua aliyopewa wakati anapata ajira kwa mara ya kwanza ili aweze kulipwa mafao yake iondolewe.

Nafikiri wanaweza kuweka taratibu zingine kama Nida, na kadi ya shirika husika (NSSF/PSSSF) au pengine wachukue alama za Vidole kabla mtu hajastaafu.

Kudai wazee barua hizo ni kuwapa usumbufu wastaafu na kutengeneza mazingira ya Rushwa
 
Hiyo ni namna iliyo wekwa mahsusi kwaajili ya kufanikisha upigaji
 
Kutokana na maendeleo ya Technologia, ambapo zipo njia za kuaminika zaidi za kumtambua mtu; napendekeza Sheria ya Kudai mzee aliyekuwa mfanyakazi pengine kwa miaka 30 alete barua aliyopewa wakati anapata ajira kwa mara ya kwanza ili aweze kulipwa mafao yake iondolewe.

Nafikiri wanaweza kuweka taratibu zingine kama Nida, na kadi ya shirika husika (NSSF/PSSSF) au pengine wachukue alama za Vidole kabla mtu hajastaafu.

Kudai wazee barua hizo ni kuwapa usumbufu wastaafu na kutengeneza mazingira ya Rushwa
Barua ya ajira n I muhimu sana,labda Sasa hivi mnaajiriwa bila barua ndo mnasema hivyo
 
Najua mfanyakazi hupewa barua wakati akiajiriwa
hata hivyo Barua inaumuhimu gani wakati wa kudai mafao uliyochangia mwenyewe kwa miaka 25 au 30?
Unamaanisha NSSF/PSSSF hawawezi kuwa na record tofauti ya kumtambua aliyekuwa anawawekea hela kwa miaka 25 hadi 30hivi hadi wamdai barua aliyopewa miaka 30 iliyopita?
Wenzetu walioendelea kwa miaka mingi hutumia national Identity/passport na finger print basi; natamani na sisi tuhamie huko au karibu na huko
 
Back
Top Bottom