Nakumbuka kuna tukio moja habari yake nililipata mtandaoni, kulikuwa na kigorofa, mwenye gorofa aliweka hidden camera katika vyumba ambavyo kawapangisha wapangaji wake, yeye(mwenye nyumba) kwake ni chini kule ground floor! kila wapangaji wakifanya mapenzi mwenye anapiga chabo kupitia kwenye screen na kulikuwa na screen kibao, kila screen kimeunganishwa na camera ya kila chumba.
Siku moja, mpangaji na mpenziwe ktk harakati za kutafuna raha zao, mwanamke aliliona camera dalini juu akiwa katika mkao wa 'Kifo cha Mende' akamshtua bwana wake kaona hidden camera dalini mechi ikakatika, yule bwana akaifuata camera dalini na kuichomoa kwa nguvu kumbe kulikuwa na waya uliounganishwa moja kwa moja hadi kwa mwenye nyumba.
Mwenye nyumba kuona screen moja imechomolewa cable hapo akatafuta upenyo wa kukimbia, bahati mbaya au nzuri kulikuwa na wapangaji wengine nje ya ghorofa nao walishtushwa na ile hamaki ya mwenye nyumba wao, baadae ndo wakatokea hao wapenzi waliokatishwa mechi na kueleza kilichowashtua na wapangaji kusikia hivyo nao wakasachi kama hidden camera kama mavyumbani mwao.
Bahati nzuri wakazikuta hidden camera, ndipo wakapiga simu polisi na kufanya ukaguzi wakagundua ni kweli mwenye nyumba aliwapiga chabo wapangaji wanaofanya mapenzi.
Hii stori sikumbuki vizuri source niliipata siku nyingi sana ila picha nzima naikumbuka vizuri, ilitokea Uingereza miaka ya nyuma.